Black Butterfly
Member
- Aug 31, 2022
- 54
- 99
Kwa takriban miezi miwili sasa kumekuwa na Malalamiko mfululizo kutoka Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu kutoka maeneo mbalimbali nchini ambao wanadai Fedha zao za Refund walizolipa wakati wa kujisajili kisha kuahidiwa kurejeshewa wakati wa kuingizwa fedha za Mikopo lakini hadi sasa wengi hawalipwa, vyuo vingine vimelipa baadhi ya wanafunzi na vingine vimelipa fedha chache.
Vyuo ambavyo hadi sasa vimelalamikiwa kutolipa Fedha za Refund ni Mzumbe, Chuo cha Mwalimu Nyerere, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma, DIT, UDOM, IFM, MZUMBE, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini (IRDP) na vingine ambavyo sijavitaja hapa. Hivi vyote vinalalamikiwa kutolipa Fedha za Refund kwa Wanafunzi na havisemi sababu nini.
Nashauri Serikali ifanye uchunguzi wa suala hili ikibidi TAKUKURU wafuatilie nini kinakwamisha malipo hayo huku baadhi ya wanafunzi wakiambiwa watalipwa fedha hizo kwenye mwaka wao wa mwisho wa masomo, kitu ambacho sio haki.