KERO Chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere kitulipe refund zetu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Habari za wakati huu,

Asilimia kubwa ya Wanafunzi tunaohitimu masomo ya Shahada ya Kwanza katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA) ambacho kipo Kigamboni hatujalipwa fedha zetu za refund.

Uongozi wa chuo ulituahidi kuwa utakuwa umekamilisha malipo yetu kabla ya Siku ya Graduation ambayo itafanyika siku ya Ijumaa tarehe 24 mwezi huu Novemba 2023 lakini hadi sasa waliolipwa hawafiki hata nusu ya Wanafunzi tunaohitimu.

Awali tuliokuwa tunadai ni zaidi ya Wanafunzi 1,000 lakini hadi sasa ambao hawajalipwa ni zaidi ya 500.

Kwa ambao hawaelewi kuhusu refund tunazodai ni kuwa hizi ni zile fedha ambazo Wanafunzi tulilipa kwa ajili ya ada baada ya Bodi ya Mikopo (HESLB) kuchelewa kuingiza fedha zetu za mikopo, hivyo tukajilipia ili fedha za Bodi zikiingia turejeshewe za kwetu.

Tayari Bodi imeshaingiza fedha chuoni lakini chuo kimeuchuna hakijatupa mkwanja wetu na tayari tunaelekea kuondoka chuo.

Tunachojiuliza kama tunaenda kufanya sherehe ya kuhitimu chuo wataweza kutulipa tena baada ya hapo?

Kingine ambacho kinatupa hofu, ni kuwa wakati tukiendelea na mchakato wa madai uongozi wa Chuo ulifuta rekodi za madeni kwenye akaunti za Wanafunzi, tulipowauliza sababu za kufanya hivyo, wakadai kuwa watatulipa tusiwe na wasiwasi.

Hivyo, ikitokea mtu akaenda kulalamika nje ya Chuo na wakaja kuangalia kwenye mfumo itaonekana hakuna kiasi ambacho Wanafunzi wanadai lakini uhalisia wake ni tofauti.

Tunaomba ujumbe huu ufike hadi Wizara ya Elimu kuwa Wanafunzi tunaohitimu Chuo cha Mwalimu Nyerere hatujalipwa refund zetu na inavyoonekana chuo kinataka tumalize ili tuanze kupata shida kupata stahiki zetu.

Pia soma:
- TAKUKURU ichunguze malalamiko ya Wanafunzi wa Vyuo kutorudishiwa Fedha za 'Refund', kuna kitu hakiko sawa
 
Mbona kudai hawaelewi somo!kurefund wanakuwa wazito,noma hiyo.
 
Habari,

Kwa kiasi kikubwa, sisi wanafunzi tuliomaliza masomo ya Shahada ya Kwanza katika Chuo Kikuu cha St. John's University of Tanzania, Dodoma, hatujapokea marejesho ya fedha zetu.

Uongozi wa chuo ulituahidi kwamba malipo yetu yangeshughulikiwa ndani ya mwezi wa kumi, yaani Oktoba, lakini hadi sasa, hakuna mwanafunzi aliyepokea malipo yoyote.

Kuhusu marejesho ambayo tunadai, ni fedha tulizolipa kwa ada baada ya Bodi ya Mikopo (HESLB) kuchelewa kutoa fedha za mikopo. Tukajilipia ili turejeshewe fedha zetu mara Bodi itakapotoa mikopo yetu. Pia, kuna wale ambao hawakuwa na mikopo ya ada, lakini Bodi ililipa, na sisi tukawa wa kwanza kulipia ada, na chuo kikaahidi kufanya marejesho.

Tuna wasiwasi kuhusu jinsi mchakato wetu utavyofanyika baada ya kufanya sherehe ya kuhitimu. Je, itazingatiwa, huku muda uliotangazwa ukishapita, yapata miezi miwili na nusu sasa?

Tunaomba ujumbe huu uifikie Wizara ya Elimu ili kuwajulisha kuwa wanafunzi waliohitimu kutoka St. John's University hatujapokea marejesho yetu.
 
Naona ni vyuo vingi tu ata moshi co University hawaja lipwa hata mmoja zisha pigwa izo na serekari ya kiremba
 
Back
Top Bottom