Ubadhirifu Serikali za Wanafunzi wa Vyuo wakithiri, CCM yatajwa, Rais wa TAHLISO atakiwa kujiuzulu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Baada ya vyuo vingi ikiwemo DIT (Dar es salaam Institute of Technology) Sasa ni SAUT (St. Augustine University of Tanzania) Mwanza.

Huyu Anaitwa Kabado C. Kabado Rais wa Serikali ya Wafunzi SAUT Mwanza
20231124_140452.jpg
20231124_140455.jpg

Tar. 21 Nov, 2023 Usiku Nlipokea simu na Jumbe za Maandish nyingi kutoka kwa Wanafunzi wa SAUT MWANZA, hasa Wabunge na Baadhi ya Mawazri wa SAUTSO wakinieleza kuhusu hili.

Rais huyu ambaye pia ni Mteule wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)
1700824322243.png
1700824347863.png
Kama ilivyo Kwa Serikali za Vyuo vingi Nchini, Chanzo Kikuu cha Mapato ya Serikali hizi ni Michango ya Wanafunzi wote ikiwemo watoto wa Masikini wanaopata Mikopo na wasio pata.Hata yule Mwanafunzi anayelazimika kula mlo mmoja Kwa siku pia hutoa Michango hii Kila Mwaka.
1700824473288.png
Binafsi Ninaamini Mamilioni ya michango hii yalipaswa kuwa Sehemu ya Kuwanufaisha Wanafunzi wenyewe kwanza kama;> Wale wanaokwama kufanya Mitihani Kwa Kukosa Ada Kwa wakati> Kuwekeza Katika Miradi mbalimbali yenye Kulenga kuwanufaisha Wanafunzi Nk.Kinyume Chake, Fedha hizi

Zimekuwa zinatumika vibaya kwa Manufaa ya Wachache.

Kutokana na kwamba Wakuu wa Vyuo vingi Nchini ni Sehemu ya Waidhinishaji wa Fedha kutoka kwenye Akaunti za Benki za Serikali za Wanafunzi, kunaviashiria vya Baadhi yao kuhusika Kwa namna moja ama nyingine katika uovu huu.

1700824560275.png
Kwa Katiba za Serikali za Wanafunzi, Mabunge ndiyo yenye Mamlaka ya Kujadili na Kupitisha Bajeti zote.Lakini kutokana na vyuo vyetu vingi kuingiliwa na kutekwa na Mifumo ya Chama Cha Siasa Hasa, CCM. Jambo ambalo ni kinyume na Sheria ya Vyuo Vikuu ya 2005,

1700824602636.png
Pia ni kinyume na kanuni za Vyuo husika.Michakato ya Upatikanaji wa Wabunge na Viongozi wa Serikali za Wanafunzi,huendeshwa na Utawala wa Vyuo ambao unafuata Maelekezo ya CCM.Matokeo yake ni Serikali na Mabunge haya kujaa Vijana Wanaohitajika na Utawala wa Vyuo na CCM

1700824664876.png
Na sio Vijana wanaoweza kusimamia Maslahi ya Wanafunzi wenzao Kwa kufuata Taratibu Halali za Vyuo na Sheria za Nchi.

Inasikitisha kuona tawala za Vyuo vingi kutumia Nguvu kubwa kuweka Viongozi watakao saidiana nao Kupora Rasilimali za Wanafunzi, Ajabu zaidi hata Vyuo vya Dini

1700824749865.png
vingi ambavyo tulitarajia Uadilifu, Usawa na Haki kutamalaki. Navyo vimeangukia katika Mtego huu na Vinashiriki kuwaandaa Vijana Wezi, Wabinafsi na Wenye Uchu ili kuja kuongoza Taifa Baadae Kwa Mtindo Huu.Kijana Kabado C. Kabado, Kama ilivyo Kwa Marais wengi wa Serikali za Wanafunzi, Ametumia njia zilezile za Udanganyifu na Rushwa Kushinikiza kupitishwa kwa bajeti za miradi mitatu Ambayo ni Mradi wa;1.

WiFi2. Cafeteria3. StationaryYenye Thamani zaidi ya TSH Mil.50Baada ya Kukosekana Kwa maelewano ya Kimaslahi kati Viongozi waliokula njama za Kutengeneza Mazingira ya Kujinyakulia fedha baada ya Bajeti hii kupitishwa, Kwa kuwa ilionekana upande wa Kundi la Rais Kabado litanufaika zaidi kinyume na Makubaliano yao. Wabunge waliamua kuweka pingamizi la Kupitishwa Kwa Bajeti hiyo.

Na Ndipo Rais Kabado alipoamua kutumia Njia za Udanganyifu zaid kuanzia Hatua ya Kupga Kura za Kupitishwa Kwa Bajet hiyo.Hii n Sehemu ya mawasiliano ya Rais Kabado na Katibu wa Bunge ambaye, Bila Kutarajia sim yake ilitua mikononi mwa wenzao wa Kundi la pil lililoonekana Kunufaika kdogo, na Habar hizi wakazivujisha.

1700824895215.png
1700824918744.png

1700824932680.png
1700824946728.png


Ninachojiuliza ni, kama kweli Bajeti hizi zingelikuwa zinalenga Kuwanufaisha Wanafunzi; Kwanini utumike Udanganyifu na nguvu kubwa kiasi hiki mpaka Polisi..!?

Nchi hii imeoza Kila Kona, Fikiria Hawa Ndiyo wanaoandaliwa kuiongoza CCM Leo na Kesho. Sasa naamini Kupe huzaa Kupe.
1700825607985.png
1700825614401.png

1700825625206.png
1700825632599.png

Maspika wa Mabunge ya Wanafunzi na Makatibu wao, Wabunge na Mawaziri wengi Katika Vyuo vingi hizi ndizo Biashara zao.Bila kupepesa macho, Wala kupaka rangi maelezo. Viongozi wengi wa Vyuo si waadilifu na Kutokana na Kwamba wengi wao ndiyo walezi wa Umoja wa Vijana wa CCM Vyuoni
1700825657387.png

(UVCCM), Si rahisi kuwatenganisha na Ubadhirifu wa Fedha hizi Unaofanywa na Vijana wao.Kwa kuwa wao Ndio wamekuwa Mstari wa Mbele kuhakikisha Vijana wanaopata Uongozi Vyuoni ni wale watakao kuja kutii Maelekezo yao hata kama yanawaathiri Wanafunzi na Taasisi za Vyuo Kwa Ujumla.



Video hii inaonesha namna Ambavyo Rais huyu anavyo kiri Udanganyifu wake katika hili. Lakini pia Kujigamba kuwa hakuna wa kumchukulia Hatua yoyote Kwa kuwa Yeye n Mtoto wa mfumo.Haitoshi, Anaamua kutumia Rushwa nyingine Kutaka kufichwe Ushahid huu wa Rushwa na Udanganyifu wake.


Vyuo vyetu vimekuwa kama Shule za Msingi Kwa sababu za Ukoloni wa Chama Tawala (CCM) na Wafuasi wake.Badala ya Vyuo vyetu kutujenga na kutuandaa kulitumikia Taifa Kwa Uzalendo, Wivu na Uadilifu! Leo Vyuo hivi Vimekuwa Vichaka vya kuwafuga Vibaka na Wafuasi wa Uovu. INAUMIZA

Nitoe Wito kwa Uongozi wa Chuo Cha SAUT Mwanza na Vyuo vingine vyote, Kurejea Misingi na madhumuni ya kuanzishwa Kwao na Viyasimamie hayo Ili Kulinda Heshma na Hadhi zao. Vilevile Kuliponya Taifa Letu.Zaidi naishauri TAKUKURU Kuongeza Urefu wa Mkona wake Katika Vyuo vyetu.

Developing Story
 
Baada ya vyuo vingi ikiwemo DIT (Dar es salaam Institute of Technology) Sasa ni SAUT (St. Augustine University of Tanzania) Mwanza.

Huyu Anaitwa Kabado C. Kabado Rais wa Serikali ya Wafunzi SAUT Mwanza
View attachment 2823235View attachment 2823236
Tar. 21 Nov, 2023 Usiku Nlipokea simu na Jumbe za Maandish nyingi kutoka kwa Wanafunzi wa SAUT MWANZA, hasa Wabunge na Baadhi ya Mawazri wa SAUTSO wakinieleza kuhusu hili.

Rais huyu ambaye pia ni Mteule wa Rais wa Jumuiya ya Wanafunzi Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO)

Developing Story
Ukiona kiongozi mla rushwa ngazi za juu usije kuzani kaanza kulwa rushwa alipopata hicho cheo cha juu. Viongozi huanza kupractice kula rushwa/kuiba/kufanya uchafu ngazi za chini kabisaa tena wengine ngazi za shule ya msingi by the time anakuwa waziri, au kiongozi sehemu nyingine unakuta alishakubuhu. Ndiyo maana rushwa kubwa kubwa wizi mkubwa na uchafu mwingine wa viongozi wa Afrika ni utamaduni kabisaa na hauonewi haya na hawataki kuacha.

Huyu anayesemwa hapa baadae utashangaa ni rais wa nchi!
 
Back
Top Bottom