Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 236
- 249
ISIDORI Temba yupo kitandani ghorofa na pili Hospital ya rufaa ya Kanda ya KCMC akiendelea na matibabu ya jeraha la risasi analodaiwa kupigwa na mfanyabiashara muuza vifaa vya kielektloniki la Temba Watch lililopo Double Road mjini moshi.
mfanyabiashara huyo kwa sasa yupo mikononi mwa polisi kuhusiana na tukio ambalo limekuwa gumzo mjini moshi kutokana na umaarufu wa mfanyabiashara huyo mkazi wa Rau Madukani.
Inadaiwa kijana huyo alikumbwa na mkasa huo muda mfupi mara baada ya kuamua ugomvi wa mfanyabiashara huyo na mke wake .
Inaelezwa kwamba majeruhi huyo baada ya kuamua ugomvi huo na kurejea nyumbani kwake,muda mfupi mfanyabiashara huyo alimfuata kijana huyo nyumbani kwake akiwa na silaha na kumpiga begani.
Inaelezwa kwamba kijana huyo alipambana kunusuru maisha yake na kufanikiwa kumpokonya silaha mfanyabiashara huyo na kwenda kuisalimisha kituo kikuu cha polsi mjini moshi.
Temba Watch amekuwa akilalamikiwa kwa matumizi mabaya ya silaha na inaelezwa katika miaka ya hivi karibuni aliwahi kumjeruhi kwa risasi mkewe lakini hadi sasa bado hajaponywa silaha yake na mamlaka husika.
Nitarudi baadae kukuletea mkasa mzima na maendeleo ya majeruhi hapo KCMC kwani kwa sasa anachukuliwa na madaktari kwa ajili ya kipimo cha X-Ray