Taifa kwanza: Rais na mawaziri 2015

hii point haiendani na umri wako
 

ha! ha! ha! ha! ha! poa mkuu, nimejaribu kutoa wazo tu.
 
Jaman slaa na wenzie waachen kwenye madaraka yao ili waendelee kutuelimisha na kukosoa,mkiwapa uongozi watabadilika na hamtaamin wote na tutarudi kulekule na itakuwa mbaya zaidi!
 

- Kuna uwezekano mkubwa sana 2015 tukawa na wagombea huru, ndio maana pia hapa tunajaribu kuwapa nguvu wale ambao hawatapewa nafasi ya kugombea na vyama vyao.

Willie @ NYC, USA.
 

- Hata Mrema alitoa tongo tongo nyingi sana mkuu, vipi Dr. Slaa hana skills zingine ni hii tu ya kutoa tongo tongo?

Willie @ NYC, USA.
 
- Mh. Regia Mtema: My very dear Friend huyu anafaa sana kuwa Waziri wa Katiba na Maendeleo ya kina Mama.

Willie @ NYC, USA.
 

- Afadhali sana hii imetoka kwako wewe mkuu wa JF, duh! bado siamini kumbe unayajua haya?

Willie @ NYC, USA.
 
Nashangaa aliyeanzisha thread kutuomba tupendekeze lakini ndiye amekuwa mpendekezaji mkuu
na mpingaji mkuu wa mapendekezo ya wengine Dah!
 
@NYC hawezi kuja kuwa kiongozi kwenye nchi yenye kipindupindu, malaria, pepopunda, foleni, rushwa aache maisha yake ya raha huko aliko yaliotokana na jasho letu watanzania maskini

- Hapo umekosea sana maana haya maisha niliyonayo hapa nimeyatafuta mwenyewe kwa jasho na my blood, hii bongo unayoiona sasa wengine tumetoka nayo mbaali sana, sema ni masiha ayako wewe ambayo yanatokana na jasho la wananchi, hapo umeenda nje kabisa ya mstari maana evidence na mashahidi wapo ! ha! ha! ha! ha! kwa hiyo nitakapoamua nitarudi kugombea anything hakuna wa kunizuia, ukitaka tukutane kwenye majukwaaa1 ha! ha! ha!

Willie @ NYC, USA.
 
W.J. Malecela,

Utaomba kila unachoomba na kuchambua watu kama karanga lakini the fact remains tunahitaji kwanza kuwaondoa Mtandao - the cartel, ambao najua fika haitakuwa kazi rahisi.

Labda nikukumbushe tena kwamba hawa jamaa wamechukua madaraka wakijua fika kwamba watatawala milele na sii kwa awamu moja ama mbili na ndio maana wamemweka JK kiti kikubwa kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala tulokuwa nao. Sasa pigeni mahesabu ya rais sijui mawaziri mtakavyo lakini mfumo wanchi hii unamilikiwa na kiti kikubwa na kwa maarifa makubwa mtandao yaa hii cartel imehakikisha kiti kikubwa kinashikwa na kabuntas! mtu ambaye wananchi hawawezi kumhusisha na Ufisadi, mwenye roho mbaya, asiyeuzika na kadhalika, wakati wao wakiwa behind the scene..

Kwa hiyo, tukirudi na kujifunza kutokana na historia, Mtandao upande wa serikali wachezaji wakubwa ni RACHEL na bila kumsahau Six ambaye leo tunamwona kaokoka, lakini nawataarifu tu kwamba ktk mahesabu ya bao langu namwona Sitta kama ndiye mgombea atakayesimamishwa mwaka 2015 kama mgombea urais wa CCM kwa sababu amekoshwa tayari kwa wananchi kumpokea mwaka 2015 wakidhania ni msafi kama tulivyofikiria kwa JK.

Mimi nadhani Sitta ameondolewa makusudi na kusafishwa ili kusubiri 2015, hivyo itakuwa kazi kubwa sana kuwashinda mtandao kwa dhana ya kujiandaa kutafuta Utaifa kwanza kabla hatujamshinda adui aliyepo mbele yetu. Uzalendo ni ari ya kupambana na adui aliyepo na kumwondoa kurudisha usalama na viongozi bora ni wale watakaokuwa mstari wa mbele kupambana na adui huyo kifikra na kimwili. Dr.Slaa, Zitto, Kigoda, Mwandosya, Lipumba wote hawa sii lolote sii chochote ikiwa hatuelekezi nguvu zetu ktk kumwondoa adui yetu - Mtandao madarakani, na haitawezekana kwa kupitia sanduku la kura kwani Mtandano wamejipanga wanajipanga na wataendelea kujipanga ktk maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015.
 
- Mh. Ben Membe: anafaa sana kuwa Rais na Waziri Mkuu pia 2015; kwa sababu ni msomi, mfuatiliaji, mtendaji, anajali sheria, na ni mkali sana.

Willie @ NYC, USA.
Usisahau sifa yake nyingine muhimu ya kudai chenji ya rada kwa hisia kali bila kueleza mkakati wa kuwashughurikia waliohusika na ufisadi huo.
 

ubarikiwe sana mkuu.
 

Mkuu twende mbele turudi nyuma huyu EL kwa maamuzi na usimamizi hakuna wa kumlinganisha naye. Uamuzi wa kuwapuuza Waaarabu katika kuwapatia wasukuma maji toka Lake Victoria ulikuwa ni mgumu; usimamizi wa ujenzi wa shule za kata ulikuwa wa kuigwa nadhani kama angeendelea kuwepo basi kila kata ingekuwa na kituo cha afya kama serikali ya CCM ilivyoahidi wakati inaingia madarakani mwaka 2005.
 
Zitto kama urais itashindikana basi apewe ata wizara ya fedha hili fedha zetu ziwe na mipango thabiti na yenye maendeleo kwetu sisi wanachi, Makamba Jr anafit sana kwenye mambo ya ndani.

brain zero
 

Nachukia Ufisadi: Matusi, Uongo, Tetesi na Majungu pia ni Ufisadi; Tujitenge Navyo:rain: LOWASA NI FISADI
 
- Kuna uwezekano mkubwa sana 2015 tukawa na wagombea huru, ndio maana pia hapa tunajaribu kuwapa nguvu wale ambao hawatapewa nafasi ya kugombea na vyama vyao.

Willie @ NYC, USA.

Hizi ndio ndoto! Haya, tuseme tuwe na wagombea huru, je atatoa wapi baraza la mawaziri? Atateua marafiki? How will they be accountable? Waziri Mkuu atatoka wapi apate support ya bunge zima? Upende, usipende, lazima kutakuwa na coalition na chama kimoja. Which means lazima afuate sera au ajenda za hicho chama. Ivi unadhani kikwete ni zaidi ya ccm kwa vile ni rais? wakimtosa leo unadhani ataweza kubaki hapo? Ninaishi katika nchi inayoruhusu wagombea huru. Its all just a facade. Msingi wa siasi ni vyama. Hii ni politics101 ndugu yangu.
Endeleeni kutaja majina! Kila la kheri...
 

sio kweli, nakataa kata kata.
 
Nimegunduwa tukijijengea misingi mizuri,basi kupata mtu mwaminifu wa kutuongoza na kuisimamia siyo shida hata kidogo.Kwasababu tukimpima kwa hayo,hata akichemsha tunamwondoa.Tupate katiba itakayotuwezesha kuwawajibisha pale tunapotaka sisi wananchi.Mataifa ambayo demokrasia yao imekua wana badili marais lakini hata kama wakichemsha,bado madhara yake si makubwa kuliko marais ama viongozi wabinafsi wenye kufanya mambo yao binafsi badala ya kuwatumikia wananchi kama ilivyo kwenye mataifa mengi ya Afrika hususan Taanzania.

@ William,nimeipenda hii thread mkuu,however ningeomba pia kuwepo na thread yenye kujadili kuwa ni mambo gani yawe kwenye katiba yetu ambayo ni muhimu sana.Tuweke misingi ambayo tunataka isimamiwe na viongozi hao tunaowataka.(Naomba usinitake kuianzisha).

Zaidi ya hapo itakuwa ni same ol shit,just a different day ama same ol shit just a different shovel or toilet.Ni kama kuvua gambas na kubandika gambas.Hata hao tunaowatetea wa ccm kuwa ni wazalendo,wameshindwa kufanya mabadiliko chini ya system wanayoitumikia.Ubinafsi umewapiga ganzi.Wanalipwa vyema na ni rahisi kusahau.Mfano kina Mwakyembe kama walivyosema wengine.Njia za panya ni njia za panya tu na si vinginevyo.Panya watakuwa tofauti na watazaliana,lakini njia ni zile zile,nuttin will change...Kwasababu movement ndani yake zinategemea zaidi mazoea badala ya ubunifu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…