Tahadhari: Utumiaji wa ‘BCC’ katika kutuma barua pepe yaweza kuwa sababu ya uvujaji mkubwa wa Taarifa Binafsi

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Ofisi ya Kamishna wa Taarifa huko Uingereza ametahadharisha kuwa Matumizi mabaya ya ‘BCC - Blind Carbon Copy’ katika utumaji wa barua pepe ni miongoni mwa sababu kubwa za Uvujaji wa Taarifa katika Sekta mbalimbali

BCC - Blind Carbon Copy (Nakala ya Kaboni isiyoonekana) ni kitufe kinachokuwezesha kutuma barua pepe kwa Wapokeaji wengi bila kufichua utambulisho wa Wapokeaji wengine kwenye orodha

IMG_7752.png

Ofisi hiyo imeainisha kuwa utumiaji mbaya wa ‘BCC’ wakati wa kutuma barua pepe kwa watu wengi umesababisha kuvuja kwa zaidi ya Taarifa 1,000 za watu ambazo hizo ni zile tu zilizoripotiwa katika Ofisi hiyo

Ofisi hiyo imeeleza kuwa inatarajia kuona utumiaji wa ‘BCC’ iliyojumuishwa katika Vifurushi Vikuu ya kutuma barua pepe unapotea kabisa hivi karibuni kwa sababu inaweza kuepukika vinginevyo kwani unaweza kusababisha kuvuja kwa taarifa nyeti binafsi na kusababisha madhara makubwa ya kutisha

Haishauriwi kutumka ‘BCC’ unapotuma barua pepe nyingi kwa Wapokeaji wengi na/au ikiwa barua pepe inaweza kufichua maelezo nyeti kuhusu wapokeaji. Badala yake ushauri ni kutumia njia zingine salama, kama vile huduma za barua pepe nyingi. Hii itazuia uwezekano wa makosa kufanywa.

ICO inasema pia inatarajia Wafanyabiashara, Kampuni na Sekta mbalimbali kuzingatia kuwa na sera na mafunzo kuhusiana na mawasiliano ya barua pepe
 
Back
Top Bottom