Je, wajua jina lako ni Taarifa Binafsi? Fahamu na elewa maana ya Taarifa Binafsi

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
626
938
Taarifa Binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na namna ya kumtambulisha au anavyotambulika mtu.

Mfano wa Taarifa Binafsi unaweza kujumuisha Jina, Anwani, Barua pepe, Nambari ya Kitambulisho Binafsi, Nambari ya Usajili, Picha, Alama za Vidole, Nyenzo za Kibaolojia, au taarifa nyingine zozote zinazoweza kumtambulisha mtu, zenyewe au kwa kuunganisha na taarifa nyingine.

Siku hizi baadhi ya Wakusanya taarifa wamekuwa wakibadilisha taarifa za kuhusu jina au anwani kwa kuweka ‘code’ (pseudonymize information), kama vile AB123, lakini hiyo bado ni Taarifa Binafsi ikiwa tu ‘code’ hiyo inaweza kufuatiliwa na kuonesha taarifa halisi za mtu.

Utazitambuaje taarifa binafsi za Watu?
Sheria ya Tanzania ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022 imeanisha kuwa Taarifa binafsi maana yake ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote, ikiwa ni pamoja na;
  • Taarifa binafsi zinazohusu rangi, asili ya kitaifa au kikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu binafsi;
  • Taarifa binafsi zinazohusu elimu, historia ya matibabu, jinai au ajira;
  • Namba yoyote ya utambulisho, alama au namna nyingine maalum inayomtambulisha mtu binafsi;
  • Anwani, alama za vidole au kundi la damu la mtu binafsi;
  • Jina la mtu binafsi linaloonekana katika taarifa binafsi za mtu mwingine anayehusiana naye au pale ambapo ufichuzi wa jina hilo utadhihirisha taarifa binafsi za mtu;
  • Taarifa iliyotumwa kwa mkusanyaji wa taarifa binafsi na mtu, ambayo ni wazi kuwa taarifa hiyo ni binafsi au ya siri, na majibu kwa taarifa hiyo yanaweza kufichua maudhui ya taarifa ya awali, na mtazamo au maoni ya mtu mwingine yeyote kuhusu mhusika wa taarifa;
Je, wajua kuna taarifa binafsi nyeti zaidi?
Lakini pia kwa Mujibu wa Sheria hiyo ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya mwaka 2022, Baadhi ya Taarifa Binafsi ni nyeti zaidi na zinahitaji kiwanngo cha juu cha ulinzi. Taarifa hizo ni Pamoja na zile zinazohusiana na;
  • Taarifa ya vinasaba, taarifa inayohusu watoto, taarifa inayohusu makosa, miamala ya kifedha ya mtu binafsi au hatua za kiusalama, taarifa za kibayometriki;
  • Ikiwa imechakatwa, ni taarifa binafsi inayoonesha asili ya rangi au kabila, itikadi za kisiasa, imani za kidini au kifalsafa, ushirika, uanachama wa vyama vya wafanyakazi, jinsia na taarifa za kiafya au mahusiano ya kingono; na
  • Taarifa binafsi yoyote ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi inachukuliwa kuwa ina athari kubwa kwa haki na maslahi ya mhusika wa taarifa
Tanzania ina Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inayojulikana kama “Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022” iliyoanza kutumika Mei 01, 2023 kwa ajili ya kuweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi wa taarifa binafsi kwa lengo la kuweka kiwango cha chini cha matakwa ya ukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kuimarisha ulinzi wa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali na vyombo binafsi, na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
 
Taarifa Binafsi ni taarifa zozote zinazohusiana na namna yakumtambulisha au anavyotambulika mtu.

Mfano wa Taarifa Binafsi unaweza kujumuisha Jina, Anwani, Barua pepe, Nambari ya Kitambulisho Binafsi, Nambari yaUsajili, Picha, Alama za Vidole, Nyenzo za Kibaolojia, au taarifa nyingine zozote zinazoweza kumtambulisha mtuzenyewe au kwa kuunganisha na taarifa nyingine.

Siku hizi baadhi ya Wakusanya taarifa wamekuwakubadilisha taarifa za kuhusu jina au anwani kwa kuweka‘code’ (pseudonymize information), kama vile AB123, lakinihiyo bado ni Taarifa Binafsi ikiwa tu ‘code’ hiyo inawezakufuatiliwa na kuonesha taarifa asili za mtu.

Utazitambuaje taarifa binafsi za Watu?
Taarifa binafsi maana yake ni taarifa kuhusu mtu anayetambulika ambazo zimetunzwa kwa namna yoyote, ikiwa ni pamoja na;
  • Taarifa binafsi zinazohusu rangi, asili ya kitaifa aukikabila, dini, umri au hali ya ndoa ya mtu binafsi;
  • Taarifa binafsi zinazohusu elimu, historia ya matibabu, jinai au ajira;
  • Namba yoyote ya utambulisho, alama au namna nyinginemaalum inayomtambulisha mtu binafsi;
  • Anwani, alama za vidole au kundi la damu la mtu binafsi;
  • Jina la mtu binafsi linaloonekana katika taarifa binafsi za mtu mwingine anayehusiana naye au pale ambapoufichuzi wa jina hilo utadhihirisha taarifa binafsi za mtu;
  • Taarifa iliyotumwa kwa mkusanyaji wa taarifa binafsi namtu, ambayo ni wazi kuwa taarifa hiyo ni binafsi au yasiri, na majibu kwa taarifa hiyo yanaweza kufichuamaudhui ya taarifa ya awali, na mtazamo au maoni yamtu mwingine yeyote kuhusu mhusika wa taarifa;
Je, wajua kuna taarifa binafsi nyeti zaidi?
Kwa Mujibu wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yam waka 2022, Baadhi ya Taarifa Binafsi ni nyeti zaidi nazinahitaji kiwanngo cha juu cha ulinzi. Taarifa hizo ni Pamoja na zile zinazohusiana na;
  • Taarifa ya vinasaba, taarifa inayohusu watoto, taarifainayohusu makosa, miamala ya kifedha ya mtu binafsi au hatua za kiusalama, taarifa za kibayometriki;
  • Ikiwa imechakatwa, ni taarifa binafsi inayoonyesha asiliya rangi au kabila, itikadi za kisiasa, imani za kidini au kifalsafa, ushirika, uanachama wa vyama vyawafanyakazi, jinsia na taarifa za kiafya au mahusiano yakingono; na
  • Taarifa binafsi yoyote ambayo kwa mujibu wa sheria za nchi inachukuliwa kuwa ina athari kubwa kwa haki namaslahi ya mhusika wa taarifa

Tanzania ina Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsiinayojulikana kama “Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi yaMwaka 2022” iliyoanza kutumika Mei 01, 2023 kwa ajili yakuweka masharti kuhusu misingi ya ulinzi wa taarifa binafsikwa lengo la kuweka kiwango cha chini cha matakwa yaukusanyaji na uchakataji wa taarifa binafsi, kuimarisha ulinziwa taarifa binafsi zinazochakatwa na vyombo vya Serikali navyombo binafsi, na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
0bcf622f099b07c881d684c8a23e0680.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JE ni Sawa kwa vyama vya siasa kukusanya taarifa zifuatazo toka kwa wanachama wao: majina yao; namba zao za NIDA, namba za kitambulisho cha kupigia kura; nasubiri majibu.
 
Mh, huyo aliyeandika habari sasa ndio kivumbi
yani unasoma hadi kichwa kinauma
na sisi tukituma zetu mnazihariri vizuri tu.
Rekebesheni isomeke vyema.
 
JE ni Sawa kwa vyama vya siasa kukusanya taarifa zifuatazo toka kwa wanachama wao: majina yao; namba zao za NIDA, namba za kitambulisho cha kupigia kura; nasubiri majibu.
Nadhani kwa idhini yako unaweza kuwapa ila si kwa kulazimishwa.
Na wao wanapaswa kuzilinda wasizitoe kwa mtu mwingine bila idhini yako.
Sijaelewa hivi hii Sheria ikisimamiwa vyombo vya udaku vitabaki kweli kwa jinsi huwa wanajadili Maisha ya watu kwa kutoa taarifa zao binafsi?
 
  • Thanks
Reactions: _ID
JE ni Sawa kwa vyama vya siasa kukusanya taarifa zifuatazo toka kwa wanachama wao: majina yao; namba zao za NIDA, namba za kitambulisho cha kupigia kura; nasubiri majibu.

Ni sahihi lakini inatakiwa kufuata misingi ya sheria ambapo katika Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ya Mwaka 2022 Kifungu cha 23 (2) kinataka Mkusanyaji wa Taarifa ahakikishe Mhusika anafahamu madhumuni ya kukusanya taarifa hizo na pia anawafahamu wapokeaji wa taarifa hizo waliokusudiwa.

Akishakueleza/fafanulia hayo nawe ukaridhia basi anaweza kuchukua taarifa zako.
 
  • Thanks
Reactions: _ID
Back
Top Bottom