Tahadhari kwa wanaoenda kumuaga Rais Magufuli

Compact

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,173
2,000
Wasalaam!

Wakati zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg John Pombe Magufuli likiendelea mkoani Dar es Salaam ni vema kila anayepanga kwenda kutoa heshima za mwisho achukue tahadhari zifuatazo.

a) Jitahidi uvae barakoa. Inakupasa kufahamu ya kuwa unaenda kwenye msongamano mkubwa wa watu na ukweli ni kuwa gonjwa hatari la COVID-19 lipo. Hivyo, chukua tahadhari kwa kuvaa barakoa yako ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa ama kuwaambukiza wengine..

b) Kama una shinikizo la juu la damu na matatizo mengine ya upumuaji kama Athma, pumu, kifafa, basi nakushauri ubaki nyumbani. Kumuona marehemu amelala inaweza kukusababisha mshtuko na kuzirai. Na huenda ikakusabisha matatizo mengine zaidi. Vema ubakie tu nyumbani kufatilia kwenye luninga.

c) Hakuna sababu yeyote ya kumpeleka mtoto mdogo kwenye shughuli kama hiyo. Kwanza ni kwa ajili ya usalama wake. Hewa ni nzito, jua ni kali na hakuna mantiki yeyote ya kumuonesha marehemu. Taswira ya marehemu hubaki sana kwenye kumbukumbu zao na siyo afya kwa ukuaji wake. Mtoto anaweza pia kukupotea. Ikakusababishia usumbufu zaidi. Watoto wabaki nyumbani.

d) Vaa viatu vya kufunika uendapo huko. Usipendelee kuvaa Sandals. Kuvaa viatu inakupa nafasi ya kutembea kwa uangalifu. Sandals zinaweza kukatika na kusababisha utembee peku. Kwa kuwa watu ni wengi, mnapotembea ni rahisi sana sandals kukanyagwa na kusababisha usumbufu.

e) Tunza vitu vyako kwa umakini. Kuibiwa na kupoteza mali ni jambo la kawaida katika makutano ya watu wengi kiasi hicho. Inaweza kukuletea hasara inayoepukika. Usibebe vitu vyenye ncha kali au vifaa vya moto. Huenda usiwe na nia mbaya lakini ikakugharimu.

f) Fuata maelekezo yote utakayopewa na wana usalama na waongozaji. Njia gani ya kupita, tumia muda mchache kutoa heshima. Ikibidi isizidi sekunde 10. Kama ni ishara ya msalaba, ifanye ukiwa unatembea. Kuchukua muda inasabisha usumbufu na ucheleweshaji.

g) Umalizapo kuaga, rudi nyumbani haraka na kaendelee na majukumu mengine ili kuwapa wengine fursa ya kuaga.. Haina haja ya kuendelea kubaki uwanjani na maeneo jirani.

Mungu atusimamie.
 
My Sons Legacy

JF-Expert Member
Feb 4, 2019
2,855
2,000
Naomba Tuambiwe hilo wimbi la watu hapo taifa leo na jana, Yalitumika Magari gani kuwasomba na kuwaleta hapo.

Yaani mpaka tunapewa Tahadhali ya kwenda Msibani kweli JPM alikua Kipenzi cha watu

Au unasemaje mama D ?
Wanatuambia huko Uhuru hakufai hewa nzito eti ? Kuna nyomi la watu
 
imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
28,227
2,000
2-Image-from-iOS-19.jpg
 
ram

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
8,287
2,000
Wasalaam!

Wakati zoezi la kumuaga aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ndg John Pombe Magufuli likiendelea mkoani Dar es Salaam ni vema kila anayepanga kwenda kutoa heshima za mwisho achukue tahadhari zifuatazo.

a) Jitahidi uvae barakoa. Inakupasa kufahamu ya kuwa unaenda kwenye msongamano mkubwa wa watu na ukweli ni kuwa gonjwa hatari la COVID-19 lipo. Hivyo, chukua tahadhari kwa kuvaa barakoa yako ili kupunguza uwezekano wa kuambukizwa ama kuwaambukiza wengine..

b) Kama una shinikizo la juu la damu na matatizo mengine ya upumuaji kama Athma, pumu, kifafa, basi nakushauri ubaki nyumbani. Kumuona marehemu amelala inaweza kukusababisha mshtuko na kuzirai. Na huenda ikakusabisha matatizo mengine zaidi. Vema ubakie tu nyumbani kufatilia kwenye luninga.

c) Hakuna sababu yeyote ya kumpeleka mtoto mdogo kwenye shughuli kama hiyo. Kwanza ni kwa ajili ya usalama wake. Hewa ni nzito, jua ni kali na hakuna mantiki yeyote ya kumuonesha marehemu. Taswira ya marehemu hubaki sana kwenye kumbukumbu zao na siyo afya kwa ukuaji wake. Mtoto anaweza pia kukupotea. Ikakusababishia usumbufu zaidi. Watoto wabaki nyumbani.

d) Vaa viatu vya kufunika uendapo huko. Usipendelee kuvaa Sandals. Kuvaa viatu inakupa nafasi ya kutembea kwa uangalifu. Sandals zinaweza kukatika na kusababisha utembee peku. Kwa kuwa watu ni wengi, mnapotembea ni rahisi sana sandals kukanyagwa na kusababisha usumbufu.

e) Tunza vitu vyako kwa umakini. Kuibiwa na kupoteza mali ni jambo la kawaida katika makutano ya watu wengi kiasi hicho. Inaweza kukuletea hasara inayoepukika. Usibebe vitu vyenye ncha kali au vifaa vya moto. Huenda usiwe na nia mbaya lakini ikakugharimu.

f) Fuata maelekezo yote utakayopewa na wana usalama na waongozaji. Njia gani ya kupita, tumia muda mchache kutoa heshima. Ikibidi isizidi sekunde 10. Kama ni ishara ya msalaba, ifanye ukiwa unatembea. Kuchukua muda inasabisha usumbufu na ucheleweshaji.

g) Umalizapo kuaga, rudi nyumbani haraka na kaendelee na majukumu mengine ili kuwapa wengine fursa ya kuaga.. Haina haja ya kuendelea kubaki uwanjani na maeneo jirani.

Mungu atusimamie.
Nadhani watazingatia, RIP Magufuli!
 
Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
18,192
2,000
Niko hapa kuangalia mbashara,nazidi kuwashangaa ndugu zangu waloenda na watoto tena wengine wananyanyuliwa kumuangalia marehemu,.hawana barakoa wala gloves..aisee Mungu aturehemu watz,ni huzuni mnoo😔
 
Cpp

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
429
1,000
Kwa lile nyomi la leo pale uhuru stadium aisee 🦠 ataishi nasi vizuri tu. Asilimia kubwa hawajavaa mask na social distance hakuna.
 
ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
5,177
2,000
Natazama umati uliofurika hapa uwanja wa Chato msibani naona ni 5% tu ndio wamevaa barakoa hata.

Watangazaji wa TBC Sam Mahela na mwenzake hawana barakoa na wanazunguka kuongea na wananchi mbalimbali wakitumia mic hiyo hiyo moja

Hofu yangu tusije tukawa ndio tunakuza au kuhamasisha rate ya maambukizi ambayo pengine yalikua chini mno, isije tokea maambukizi na vifo vikafumuka soon.

Mungu atusaidie Watanzania, ukiangalia vyombo vya nje unaona jinsi gani wenzetu wanavyochukua tahadhari dhidi ya covid na hasa linapokuja jambo la mkusanyiko.

Tuchukue tahadhari jamani, tuoshe mikono mara kwa mara na kuvaa barakoa.
 
Mbao za Mawe

JF-Expert Member
May 11, 2015
22,967
2,000
Barakoa si dawa ya Corona. Tumeishi kwa zaidi ya miezi 10 bila hizo barakoa na Mungu yupo pamoja nasi.

Corona haitibiki kwa kuvaa barakoa.
 
Invigilator

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
2,348
2,000
Tanzania hatuna Corona, kunywa Tangawizi na limao, weka na pilipili kichaa ndani yake ikolee sana. (Hao wasiochukua tahadhali ya juu ya uhai wao ndio wazelendo kweli kweli).

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom