Salaam, Shalom,
Baada ya tarehe 17 march 2021, Mh Samia Suluhu Hassan kutangaza kifo Cha HAYATI Magufuli, Nchi ilizizima.
Binafsi, nilikuwa naendelea kufuatilia tetesi za kifo hicho baada ya taarifa nyingi kusambaa kutokana na ufinyu wa taarifa sahihi. Ilipothibitishwa taarifa hiyo, simanzi ilianza Rasmi.
Ilipowadia siku ya kusafirisha mwili baada ya kuaga pale uhuru, safari ya kuelekea Airport ilianza, mwili ulikuwa unapelekwa Airport Ili uende Zanzibar, Kisha Mwanza, kisha Chato Kwa maziko.
Wananchi sijui waliingiwa na nini, jamani sijui nini kiliwapata vijana wale baada ya kuambiwa kuwa hawaruhusiwi kuingia ndani ya uwanja wa ndege wa Dar Kwa sababu za kiusalama.
Nilichokishuhudia kwa muda mfupi ni uwanja wa ndege kujaa vijana wengi sana na hakuna aliyeweza kuwazuia, walikuwa wamelivunja gate Kwa sekunde chache Kisha kujaa ndani ya runways za airport na ndani ya uwanja wa ndege!
Kila mahala ulipopitishwa mwili wa HAYATI Magu, wananchi walitaka waone Kwa macho ndipo waamini Kweli Magu ameenda.
Niliona kijana mmoja akikimbiza jeneza lile, na alikiambia Kwa umbali mrefu sana, nilijiuliza Kwa jinsi chato kulivyo mbali, kijana yule asingeweza kufika Kwa kukimbia Kwa miguu. Ni kama aliona, tumaini na Imani alivyokuwa nayo kupitia kwa kiongozi wake linaondoka mbele ya macho yake😪
Nililia Kwa huzuni kuu, ndipo nikajua kuwa KAZI ya mtu Huwa inamfuata na kupaza sauti.
Alipofariki Mwl Nyerere, nilishuhudia vilio vile vya wananchi. Tofauti na msiba wa Mwl Nyerere na Magufuli ni kuwa Magufuli alifariki akiwa madarakani na ndoto alizopanga kuzitimiza hakuwa amekamilisha.
Asikwambie mtu, Nchi kuondolewa na Rais aliyepo madarakani, uchungu na taharuki Kwa wananchi Huwa haielezeki.
Taifa lilivuka salama katika msiba Ule, na hiyo ni Ishara kuwa Mungu anaipenda sana Nchi yetu.
Ahsante Mungu Kwa zawadi ya Rais na HAYATI Magufuli.
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
Amen