Tahadhari kwa wanaoenda kumuaga Rais Magufuli

Barakoa si dawa ya Corona. Tumeishi kwa zaidi ya miezi 10 bila hizo barakoa na Mungu yupo pamoja nasi.

Corona haitibiki kwa kuvaa barakoa.
Mkuu Mbao Za Mawe, ni kweli barakoa si dawa ya covid lakini si ni njia mojawapo ya kinga? na mleta uzi kazungumzia kinga si dawa
 
Mkuu Mbao Za Mawe, ni kweli barakoa si dawa ya covid lakini si ni njia mojawapo ya kinga? na mleta uzi kazungumzia kinga si dawa
Juzi Brazil walirekodi visa vya vifo 3000 ndani ya masaa 24. Kati ya Brazil na Tanzania ni taifa lipi limepuuzia Corona?
 
Natazama umati uliofurika hapa uwanja wa Chato msibani naona ni 5% tu ndio wamevaa barakoa..hata..
watangazaji wa TBC Sam mahela na mwenzake hawana barakoa na wanazunguka kuongea na wananchi mbalimbali wakitumia mic hiyo hiyo moja..
acha kufuatilia watu we kama unavaa, vaa
 
Unategemea kuwa hai kwa miaka mingapi? Kuna maradhi zaidi ya 1000 duniani na yote yanaua.

Unajua ni kwa jinsi gani Malaria inateketeza ulimwengu au kwa vile vifo vya Malaria havirekodiwi?
Sitegemei kuwa hai zaidi ya miaka 70 ijayo,lakini habari gani nisichukue tahadhali kwa kitu ambacho ikiwa kitanipata kitaniondolea uhai kwa masaa machache yajayo,ndoto zote za maisha yangu nani atazitimiza?wanangu wadogo nani atawalea?elimu yangu na mahangaiko yangu ya utafutaji yatanifaidisha nini?wazazi, ndugu na jamaa watafurahia kifo changu?.

Umetaja Malaria,mbona unashauriwa matumizi ya vyadarua na dawa za kuuwa mbu?.

Ukimwi je,hutumii kondomu kisa hutaishi daima?.

Typhoid,Chorela,Amiba, nk huchemshi maji ya kunywa na kunawa mikono pindi ulapo vyakula,kwa maana tu hutaishi daima?.

Kwenye vyombo vya usafiri,hufungi seat belt na kuendesha kwa tahadhari kwa kuwa utakufa tu siku moja?.

Habari gani kwenye Corona,wanao vaa mask ni wajinga?hawana ufahamu,nani kakuaminisha hivyo?yuko wapi sasa?.

Ikiwa maisha yako hayana faida na huyathanini bimana tu utakufa,vipi uki contaminate virus ukafa kweli,lakini ukaacha umewaambukiza familia yako,na wanao,utafurahi kumuona mama,mwanao,mke na bibi yako wakifa sababu ya upumbavu wako?..

Hakika yapo mazingatio kwa wenye kufikiri.
 
Sitegemei kuwa hai zaidi ya miaka 70 ijayo,lakini habari gani nisichukue tahadhali kwa kitu ambacho ikiwa kitanipata kitaniondolea uhai kwa masaa machache yajayo,ndoto zote za maisha yangu nani atazitimiza?wanangu wadogo nani atawalea?elimu yangu na mahangaiko yangu ya utafutaji yatanifaidisha lini?wazazi, ndugu na jamaa watafurahia kifo changu?...
Nashukuru umeandika andiko refu kidogo kuonesha msisitizo ila sitoungana nawe kamwe na hili la Corona wala si ujanja wa barakoa. Mataifa makubwa dunia yamekuwa wahanga wa huu ugonjwa zaidi ya mataifa masikini ambayo raia wake lazima watoke ili kupata riziki.

Hatuna barakoa wala hatuna tahadhari ya Corona zaidi ya US, China, UK, France wala Italy ila kikubwa cha kujivunia ni kuwa Afrika ina idadi ndogo ya wazee na miili ya Waafrika wengi inaweza kupambana na magonjwa.
 
Juzi Brazil walirekodi visa vya vifo 3000 ndani ya masaa 24. Kati ya Brazil na Tanzania ni taifa lipi limepuuzia Corona?
Shida mnapenda sana kujilinganisha,unaijua population ya Brazil?inalingana na hapa kwetu umefahamu kuwa juzi wamekufa 3000 kwa sababu ya uwazi wao katika kutoa taarifa kwa usahihi.

Hapa nchini mara ya mwisho kutoa taarifa juu ya Corona ilikuwa lini?ni kweli kuwa watu hawafi?una ushahidi gani ikiwa watu hawafi?huo ugonjwa unaoua kila siku ukapewa jina MATATIZO YA KUPUMUA ni upi?

Askofu wa kanisa Katoriki aliyetoka hadharani na kudai kuwa wamepoteza zaidi ya mapadiri na masister 75 kwa Corona ndani ya mwezi mmoja(February pekee)ni muongo?.
 
Shida mnapenda sana kujilinganisha,unaijua population ya Brazil?inalingana na hapa kwenu?umefahamu kuwa juzi wamekufa 3000 kwa sababu ya uwazi wao katika kutoa taarifa kwa usahihi?Hapa nchini mara ya mwisho kutoa taarifa juu ya Corona ilikuwa lini?ni kweli kuwa watu hawafi?una ushahidi gani ikiwa watu hawafi,huo ugonjwa unaoua kila siku ukapewa jina MATATIZO YA KUPUMUA ni upi?.Askofu aliyetoka hadharani na kudai kuwa wamepoteza zaidi ya mapadiri na masister 75 kwa Corona ni muongo?.
Tangu Corona ianze kurindima kwenye ukoo au eneo lako umepoteza watu wangapi. Nijibu nikuulize swali la msingi.
 
Nashukuru umeandika andiko refu kidogo kuonesha msisitizo ila sitoungana nawe kamwe na hili la Corona wala si ujanja wa barakoa. Mataifa makubwa dunia yamekuwa wahanga wa huu ugonjwa zaidi ya mataifa masikini ambayo raia wake lazima watoke ili kupata riziki....
Mkuu acha fikra hizi,yaani Afrika iliyojaa watu wenye Kisukari, Typhoid, Malaria,Utapia mlo,Surua,Kichocho,Ebola,Dengue,Polio,unyafuvi, Ukimwi, Kansa, Magonjwa ya figo na Ini, Tb, Safura, kaswende, Kisonono, Uti, kipindupindi, ushirikina, ujinga, umaskini na mengine mengi,watu wake wawe na strong immunity system kuliko wa nchi zilizoendelea kabisa?umewaza au umeandika tu?.
 
Mkuu acha fikra hizi,yaani Afrika iliyojaa watu wenye Kisukari, Typhoid, Malaria,Utapia mlo,Surua,Kichocho,Ebola,Dengue,Polio,unyafuvi, Ukimwi,Kansa,Magonjwa ya figo na Ini,Tb,Safura,kaswende,Kisonono,Uti,kipindupindi,ushirikina,ujinga, umaskini na mengine mengi,watu wake wawe na strong immunity system kuliko wa nchi zilizoendelea kabisa?umewaza au umeandika tu?.
Hujaelewa kwa sababu nawe una ugonjwa wa kisonono huo unaotesa Waafrika. Lifestyle ya Waafrika ni tofauti kabisa na wazungu naomba ujue hilo.

Ulaji wa Waafrika ni tofauti na wa wazungu bado tunaishi vyema kuliko wao na miili yetu ni imara zaidi kuliko wao.
 
Honestly speaking watu wangu wa karibu ni zaidi ya sita,watatu wahudumu wa afya!!.
Kwahiyo unapenda uone kila eneo limetapakaa maiti za wafu wa Corona? Tusilazimishe kufa kwa Corona tuache mkono na Mungu uonekane juu yetu pia.
 
Back
Top Bottom