TAHADHARI: Kuna matapeli! Fuata taratibu hizi...

Status
Not open for further replies.
"Mods wanauwezo hata waku locate ip add za watu so mkiona mtumiaji ID nyingi tapeli toka pale pale mshughulike"

Kama Mods wana uwezo huo na kama kuna wanaTISS wamejipenyeza katika hao Mods, tuna uhakika gani na usalama wa identity ya members wa JF!! Just an observation.
 

Nahisi tuanze na huyu mtaje!!
 

Asante kwa angalizo.

Nimeweka tangazo, kweli ninamhitaji huyu mtaalam na wala si utapeli. JF itanisaidiaje?
 
Watakaothibitishwa kuwa ni matapeli wawe banned kwa manufaa ya wanajamii
 

Sorry kuna wengne ni wageni Jf itakuwa vizuri kama ukatuambia namna ya kuwahusisha pindi tufanyapo biashara.
 

Hapo sawa !!
 
duh! kweli wajinga hawaishi ngoja nami niangilie naweza kumtapeli nani hapa ili niweze kupata pesa za kuweza kutoa huo mchango wa Tsh 30,000/=
Nalog off
 
Ni kweli kabisa mm nishatapeliwa kimapenzi na dasa furan wa humu jf.ila naoja aibu kuweka kisa chenyewe lakini haki ndiyo hiyo wa kuu
 
Katika kukabiliana na ili swala la utapeli! Ni vyema wana JF, yani uongozi wa JF ukaanzisha jukwaa maalum kwa ajiri ya kuprocess matangazo na iwe kwa premium member alone! Na pia mnavyokuwa mnapokea matangazo kutoka kwenye makampuni au watu binafsi ni vyema kujua at least address za hiyo kampuni na pia ID au cheti maaulum kinachomtabulisha mtu binafsi ambaye anataka kufanya tangazo, hizo information lazima ziwe zipataikana kwenye office zenu phyisically na siyo online kwenye website yenu.Hii itasaidia kuepesha utapeli kupitia hili jukwaa lenu, kwasababu mtu akitapeliwa kupitia ili jukwaa lenu lazima atawalaumu nyie atakama hatawafuata na kuwambia.Na pia matepeli wakizidi kwenye JF ni sawa na kuwakimbiza watu kutoka kwenye ili jukwaa lenu.

Ni vyema ili swala mkalifanyia ufumbuzi kabla alijakomaa wakuu.

Traders Easy Way-We Supply According to your Budget - Projectors and Screens

Asanteni!
 
kama imethibitika ni tapeli, ifungwe akaunti yake, na ndo dawa pekee,na baada ya kufungiwa account yake awekwe hadharani ili iwe fundisho kwa watu wengine..Naunga mkono hoja :A S thumbs_up::A S thumbs_up:
 

Aibu sio kutapeliwa, mtu yoyote anaweza kutapeliwa, angekuwa amebakwa hapo kweli na bado wapo watu wenye ujasiri wa kusema wanasema na wala hakuna aibu, aibu kubwa ni kumuona yule aliyekufanyia ushenzi akitamba.
 

Ni kweli kabisa kuna member humu ndani si waaminifu kabisa.Kuna mmoja januari mwaka huu aliniahidi kunipatia gari kwa Tsh. 3.5 m hadi leo sijaipata na fedha nilishampatia zaidi ya Tsh.3.8 m.Nimefadhaishwa sana na nasikitika sana na nimemwachia Mungu,maana nimepata tayari Gari lingine.Nina hakika haitamsaidia zaidi ya kumwongezea mateso na dhiki kuu ili ajue Mungu hajaribiwi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…