trudie
JF-Expert Member
- Jan 15, 2014
- 3,335
- 7,662
Mara nyingi kuna ndoto hizi zinajirudia sanaHabarini wakuu,
kwa siku za karibuni nimeona thread nyingi humu watu wakiwa na kiu ya kutaka kujua maana ya ndoto mbalimbali, lakini imekuwa ngumu kwao.
Wengi wamekimbilia kutisha wakiamini kuwa ndoto zote zina uhusiano wa uchawi, mashetani na ulozi, jambo ambalo si kweli.
Leo nataka nitoe somo la bure hapa. Ila kwa kuwa ndoto ziko nyingi nami nimeona kila mwenye uhitaji aniulize nami nitamjibu ktk thread hii hii.
Asanteni na karibuni sana..
Kwanza huwa naota either nimewachokoza watu au nimeiba kitu wanavyonikimbiza napaa juu naenda umbali mrefu sana natua sehemu baadae naendelea kupaa naenda mbali sana
Ya pili huwa naota nipo na mtu nnaemfahamu lakini baadae anakuja kugeuka sura anakuwa mtu wa kutisha na huwa nasali mpaka hanidhuru au nakutana na kundi la watu nywele zinasisimka kabisa naanza kusali pia watu hao wanageuka kuwa wa kutisha wanashindwa kunidhuru msaada