Msaada wa kutafsiri Ndoto

TAI DUME

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
8,991
23,541
Wakuu habari ya mihangaiko

Ni kwamba nimekuwa nikiota nipo uwanjani nacheza mpira (football). Inaweza ikawa katika nafasi tofauti tofauti ila mara nyingi nacheza forward. Kinachonikwaza/Kushangaza katika ndoto hizo ni pale ninaposhindwa kutumia nafasi muhimu, let say kumalizia tuu kufunga goli. Yaani nakuwa najiposition vizuri, naomba pasi ya mwisho, napewa hiyo pasi ambapo kila mtu anategea nitafunga goli.

Kinachotokea sasa, miguu inakuwa mizito, siwezi kuukuta ule mpira, au hata nikiukuta huo mpira napiga kijishuti ambacho hakina madhara kabisa, Au naweza nikawa kwenye nafasi ya kutoa pasi ya mwisho, yaani mwenzangu anakuwa anasubiri tuu nimwekee pasi afunge, lakini utakuta siwezi kuufikia ule mpira au nikitoa pasi basi inapotelea kwa adui,

Usiku wa kuamkia leo imekuwa kiboko. Kwanza nilianza kucheza beki, yaani nilishindwa kuutoa golini mpira ambao nilikuwa kwenye nafas kubwa ya kuokoa goli. Nikasema nibadili namba nikaenda kucheza namba tisa. Basi nikapewa pasi ambayo ilikuwa ni ya kutupia tuu mpira golini, asee nilitoa boko ambalo kila mtu alishika kichwa, maana mpira niliugusa kwa tabu sana na haukwenda popote.

Ndoto za namna hii zimekuwa zikijirudia mara kwa mara. Sio muumini sana wa kuamini katika ndoto maana nilielezwa ni imaginations tuu za mtu anazowaza sana mchanana zinaweza zikajirudia kwa mtindo wa ndoto. Ila hii sasa imekuwa too much maana simalizi miezi miwili lazima nitaota mara mbili au tatu mfululizo,

Hii hali nimeanza kuiona huu ni kama mwaka wa pili sasa. By the way kwenye maisha yangu halisi mimi ni footballer mzuri tuu si wa kushindwa kufunga kwa nafasi kama zile.

Nimeanza kuhofia hii hali kwakweli.

WAZEE WA KUTAFSIRI HIZI MAMBO, MSAADA TAFADHALI
 
Isije ikawa mpira unakupenda mbona mzize alikuwa boda boda ila saiz ni forward wa Utopolo
 
Wataalam watakuja ila kwa uelewa wangu mdogo naona maisha unayoishi sio unayotakiwa nikimaanisha kama una gari/nyumba moja ulitakiwa sasa hivi uwe nazaidi hata 3 kuendelea..!

Angalia tabia au mambo yapi yanayokurudisha nyuma ili urekebishe
 
Sasa kama kila mara unacheza mpira, ulitegemea uote unachoma nyama?
Achana na mambo ya kutafsiri, ndoto ni matokeo ya maisha yako ya kila siku achana na imani za kutafsiri. BTW ukilala usikunje miguu utakua unafunga vizuri tu.
 
Attachments

  • the-four-stages-of-sleep-2795920_FINAL-5c05c2fc46e0fb00018dac3d.png
    the-four-stages-of-sleep-2795920_FINAL-5c05c2fc46e0fb00018dac3d.png
    44.4 KB · Views: 2
Kuna hofu unayo bila kujua, jitahidi kuwa na mtazamo chanya na ndoto kama hizo zitapotea.
 
Kuna mtu anachukua nyota yako tafuta mbuzi mmoja , mchele kilo 25 kwaajili ya matambiko na elfu 50 nifate Dm ili nikusaidie usipo wahi utakua kwenye ngumu sana
 
Sasa kama kila mara unacheza mpira, ulitegemea uote unachoma nyama?
Achana na mambo ya kutafsiri, ndoto ni matokeo ya maisha yako ya kila siku achana na imani za kutafsiri. BTW ukilala usikunje miguu utakua unafunga vizuri tu.
Mara ya mwisho kucheza mpira ni kama 7 yrs iliyopita. Kwa Sasa mazoezi nayofanya ni jogging tuu hususani wéekends. Ningekuwa bado nacheza futbol ningesema ni imagination tuu. Huwa sikunji miguu ninapolala nauhakika na hilo mkuu
 
Kuna hofu unayo bila kujua, jitahidi kuwa na mtazamo chanya na ndoto kama hizo zitapotea.
Nilikuwa siweki usiriasi sana kwenye hii ndio lakni kutokana na trend za kujirudia rudia nimeanza kuhisi Kuna kitu. Labda niitafute iyo hofu ila Nina ishi MAISHA ya kawaida tuu
 
Kuna mtu anachukua nyota yako tafuta mbuzi mmoja , mchele kilo 25 kwaajili ya matambiko na elfu 50 nifate Dm ili nikusaidie usipo wahi utakua kwenye ngumu sana
Tutapika na kufanya sherehe ama? Jokes.
 
Ntaelezea kwa ufahamu wa juu kidogo ili kila MTU aelewe.

Ndoto zinazohusu destiny yako huwa zinakuja katika MFUMO au muundo wa
Wa symbolic

Na ndoto ambazo hazina uhusiano na destiny yako huwa hazina symbolic.

Hivyo ili uweze kuizingatia ndoto au kuipuuza jikite hapo .

Ikiwa ndoto yako umeota IPO symbolic.

Ntarudi kuendelea......
 
Tunakusubiri kwa hamu mkuu, just take your time ili uje na madini ya kutosha
 
Iko Hivi:
Unapata ugumu kwenye kuweka vipaumbele vyako na umeshindwa kuweka msukumo/umakini kwenye kufikia malengo yako.
Zingatia hayo na utaanza kufunga magoli/kufanikiwa.
TAI DUME
 
Ntaelezea kwa ufahamu wa juu kidogo ili kila MTU aelewe.

Ndoto zinazohusu destiny yako huwa zinakuja katika MFUMO au muundo wa
Wa symbolic

Na ndoto ambazo hazina uhusiano na destiny yako huwa hazina symbolic.

Hivyo ili uweze kuizingatia ndoto au kuipuuza jikite hapo .

Ikiwa ndoto yako umeota IPO symbolic.

Ntarudi kuendelea......
Tunakusubiri
 
Back
Top Bottom