Ndoto iliyobeba ufunuo au maono

Surya

JF-Expert Member
Jun 7, 2015
8,378
12,573
Zaidi ya asilimia 80 % Mungu huzungumza kupitia ndoto, ujumbe wa picha na alama ambazo zinakua zimebeba ujumbe au maagizo fulani.

Mungu huzungumza kwa mafumbo, ishara na picha tunaweza kuziona katika ulimwengu wa ndoto.

Mungu hutuma Malakia zake hapa duniani kushirikiana na Roho za wacha Mungu wake.
mfano. Tunajua Elisha alikua akifanya mambo mengi akisaidia na Jeshi la Malaika.
Unaweza kuzungumza na malaika katika ndoto, mfano Yusufu mumewe Mariamu.

Sitazungumzia ulimwengu wa kuonana na Malaika, lakini nitabaki katika kipengele cha ndoto ambazo ni ishara na maono ya kutupa taarifa ya nini cha kufanya katika maisha.

Maisha (life) huanzia rohoni.
Life is spiritual.
Roho upokea taarifa ya mambo yajayo na mambo ya kuzingatia ili kuwa na maisha ambayo Mungu kakupangia hapa Dunia.

Maono ya Usingizini / Ndoto.

Tafsiri ya Ndoto kuhusu...
i. Kuogelea
ii. Kuogelea kwa shida.
iii. Kuogelea bila shida yoyote.
iv. Kuogelea katika Maji machafu.
v. Kuogelea katika maji safi.

nini maana yake ?
................
Ndoto hizi sio ngeni kwa walio wacha Mungu na wasio wacha Mungu. twende Pamoja kwenye tafsiri na nini cha Kufanya.

Chapter 01.
Binadamu ni
i. Roho
iii. Nafsi
iii. Mwili

Katika nafsi ndani yake hukaa Akili(mind)
Nafsi imepewa uhuru wa kuchagua kutii amri ya mwili au amri ya Roho.

Mungu alimuumba mwanadamu aishi kwa kufata Roho (Kuishi kiroho)

Ukiishi kimwili unakua unakosea.

Mwili wako una macho mawali.
Roho yako ina jicho pia.
Mwili unamasikio mawili.
Roho pia ina sikio.

Kusikia na kuona kwa mwilini sio shida wote tunaelewa.

Roho.
Kama ilivyo katika ulimwengu wa mwili unaitaji macho na mwanga kuweza kuona. (ndiomaana wakati wa usiku tunawasha Taa ndani ) nuru iendelee kuwepo.

Pia katika ulimwengu wa roho, jicho la roho yako linaitaji mwanga kuweza kuona.

*NURU *
Nuru katika ulimwengu wa roho inapatikana vipi ?????
Kusudi kuweza kuona mambo ya rohoni.
Kumbuka katika ulimwengu wa roho ndiko kwenye uhuru wa kuona pasipo mwisho, kusikia chochote unachotaka kusikia. kila jamba linalotokea katika Mwili kwanza linaanza katika ulimwengu wa roho.
Roho inanguvu kuliko mwili.
Katika ulimwengu wa roho unaweza akasema chochote na kikawa.
Katika ulimwengu wa roho hakuna kudanganya, roho zinasikilizana bila kuficha.

Ukiwa mjuzi wa mambo ya rohoni huwezi kudanganywa na mwanadamu mfano katika mapenz bila kujua.

Fungua jicho la Tatu.

Nuru katika jicho la Ndani ...
Watu wanaangamia kwa kukosa maarifa. hasa ya kiroho.

Nitaendelea na Elimu ya Ndoto.
Ndoto ambazo ni ujumbe unaoletwa katika picha(image) na alama (symbols) and sign tofauti tofauti pindi mwili unapokua katika hadi ya kulala (subconscious)

Mwili unapokua katika hali ya utulivu sana ndipo Roho uweza kutawala na kupata nafasi ya kusikia na kuona kwani macho ya mwili ambayo yanatumika sana yanakua yamefumbwa.

Vyanzo vya ndoto.
i. Chanzo ni wewe mwenyewe shughuli zako na tabia yako. (Huletwa na Mungu pia)
ii. Kutoka kwa Mungu.
iii. Kutoka kwa Shetani.

Chanzo cha ndoto za kutoka kwa shetani ni kwa wale ambao Hawana Mungu wa Kweli. Aliye na Mungu wa kweli hapati ndoto kutoka kwa shetani, ila hupata shambulio pia linalotoka ulimwengu wa giza na kujikuta katika mapambo katika ulimwengu wa roho.

Kwa wakristo wa kweli.. Karibu natamani tujifunze tafsiri ya ndoto tofauti tofauti kwa pamoja.

Kwani kupitia ndoto ndipo roho zetu hupokea ujumbe au maagizo kutoka kwa Mungu wetu.
mfano taafira ya Jambo litakalotokea baadae katika ulimwengu wa mwili.
Huwezi kumtumikia Mungu kama huwezi kusikia sauti yake na kuitii.

by dr Surya The Prophet
 
Kuna kitabu kimoja nilikisoma 2012 Tafsiri za ndoto aisee kizuri sana kile. Nilikiazima waliweka namba za simu kuwa kinapatiķana mwengi lakini nilipofika hapo sikufakikiwa kukipata. Kizuri mno mno nilijifunza mengi sana mle.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom