Wakuu habari za weekend..
Niende kwenye mada yangu moja kwa moja.
Juzi usiku nikiwa katika rundo la usingizi, niliota ndoto iliyonipa tafakuri bila majibu.
Ilikuwa hivi, nilikuwa kwenye shamba mimi pamoja na mzee wangu.
Wakati tunatembea gafla akatokea nyoka aina ya kobra kimo cha wastani, mzee alikuwa nyuma mimi nilikuwa mbele yake. Lakini pia nilikuwa ana kwa ana na kobra.
Kwa bahati nzuri nilikuwa nimeshikilia kagongo kama kile kisukumio cha chapati, kwa kasi ya ajabu nikamtwanga kichwani na akapoteza uhai hapo hapo bila kuleta madhara yeyote, Mzee alishangazwa na ushupavu ule.
Tukaendelea na mwendo wetu, gafla tena kwenye uchafu wa shambani, akatijitokeza kobra mkubwa kuliko yule wa awali.
Sikusita, nikamtwanga kichwani akatapatapa na kupoteza uhai. ( mzee alikuwa nyuma yangu tena).
Baada ya hilo tukio tukarudi nyumbani salama. Nikashituka na kujiuliza maswali mengi, huenda inaweza kuwa na maana kwenye maisha halisi.
Je, ndoto yangu ina tafsiri gani? Naombeni mnijuze, Ahsante.
NB: Mzee bado yupo hai.