Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,890
- 6,898
Labda niulize swali ambalo niliuliza mwaka jana lakini hakuna aliyejibu. Why in just five years, President Sata managed to built an admirably big party, attracting huge crowds at campaign rallies and paid off in the 2006 election, raising 44 legislators in the 150-member National Assembly kabla ya kushinda urais mwaka jana? Kwa nini Chadema na vyama vingine vya upinzani Tanzania vimeshindwa kufanya hivyo tokea mwaka 1995?
Swali zuri sana. Lakini bila kufanya utafiti kwa mtazamo wangu naweza kuona alichofanikiwa ni kwanza umoja kati ya vyama vya upinzani. Hilo ni tatizo ambalo naliona linasumbua vyama vya upinzania Tanzania. Mwai Kibaki naye alifanikiwa kuking'oa KANU kwa utaratibu huo wa kuunganisha nguvu.
Nimejaribu kuangalia kura zilizopigwa katika uchaguzi huu mdogo, nimekuja kugundua kitu kimoja ambacho CCM imenufaika ni divide and rule. Utaona CUF, CHADEMA na kila cha Kafulila wangeweza kuwanyang'anya CCM viti vingi tu kwani walichoshindwa wapinzani ni kugawana kura ambapo CCM imenufaika na mpango huo walioukamilisha.
Ndoto zangu ni kuona hasa vyama vyenye uwakilishi bungeni kuunda jopo la pamoja katika uchaguzi hasa uchaguzi mkuu ujao, kwani tofauti walizo nazo wasipozizika kitakachotokea uchaguzi Mkuu ujao utakuwa mshangao wa wengi wasivyotegemea.
Viongozi wa Chadema taifa wateremke kutoka pale walipo wawafikie viongozi wanzao wa vyama vya upinzani wawe na jiko moja na meza moja chakula kitakuwa kitamu.