Nkasi: Wananchi wa Kabwe wadaiwa kuandamana kupinga kuongozwa na upinzani

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568

Wananchi wa kata ya Kabwe jimbo la Nkasi Mashariki mkoani Rukwa wameandamana kukataa kuongozwa na upinzani baada ya diwani wa kata hiyo kufariki huku madai yao ni kuongozwa na upinzani kwa miaka 27 bila maendeleo katika eneo hilo.

Kata hiyo ni miongoni mwa kata ambazo tume ya taifa ya uchaguzi NEC imetangaza kurudiwa kwa uchaguzi baada ya diwani wake kufariki na sasa vyama vya siasa vimeanza kampeni kwa ajili ya kumpata diwani mpya atakayeziba nafasi iliyo wazi.

Akizungumza mbele ya wananchi hao mwenyekiti wa umoja wa vijana wa Chama Cha Mapinduzi UVCCM taifa @comrade_kawaida amesema ni wakati wa CCM kupewa nafasi katika kata hiyo ili walete maendeleo ambayo kwa muda mrefu yamekosekana katika eneo hilo.

Aidha amewataka vijana na wananchi wote kujitokeza siku ya uchaguzi kutimiza jukumu lao la kikatiba la kuchagua kiongozi atakayefaa katika kuleta maendeleo.
 
Wananchi wa kata ya Kabwe huko Wilaya ya Nkasi.wameandamana kupinga Kuongozwa na Chadema Kwa miaka 27 wakidai Kwa mda wote huo hakuna maendeleo waliyoyapata.

My Take
Kuchagua Upinzani wakati hawana uwezo wa kupata Serikali ni kujitia kitanzi Cha Kukosa Maendeleo.

Nawaunga mkono hoja.CCM hawawezi leta maendeleo sehemu ambayo Kuna upinzani,kama Wananchi wamejitambua ni jambo zuri.
 
Ngoja ifike 2025,ndo watatambua kuwa Kirando Republic na Kabwe,CCM huwa na hali mbaya.wapambane na ACT.
Sasa hapo watakuwa wanamkomoa nani? Maana CCM Huwa haileti maendeleo Kwa Wapinzani.

Uchague upinzani utegemee ccm wakuletee maendeleo? Kila mtu ashinde mechi zake
 
..ambao hajaletewa maendeleo na Cdm waachwe waandamane, na ikiwezekana wachague chama chochote kingine.

..ambao wameongozwa na Ccm kwa muda mrefu na hakuna maendeleo nao wasichague Ccm tena, wabadilishe chama cha kuwaongoza.
 
Back
Top Bottom