Tafsiri na uchambuzi wa matokeo ya udiwani

washindwa na walegee hahahaha.. By the way sina chama cha siasa na hata kitambulisho cha kupiga kura sijachukua na sitochukua mpaka kije chama cha sheria za kiislam coz ni hicho pekee kinachoweza kuleta haki na usawa kwa wananchi wote mbali na hapo hapana, raisi aliyepita alikuwa mwizi na mkewe kaiba sana, huyu wa sasa watu wanasema mdini ila hana udini wowote ule ni brazameni tu na mshamba ndio maana kila siku anatembea duniani, mbowe brazameni pia akajenge madisco tu, silaha ana udini nd atatumikia mno kanisa, lipumba msomi mzuri bt ndio wale wale so sioni wa kumchagua

Wewe bado unasaidiwa kufikira that why unaongea kama pwaguzi.

NB: weka mbali na watoto.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
In any case there is nothing to celebrate from these results for CCM lovers.

Mzee, wana CCM watasherehekea kuwa CDM haikufanya vizuri zaidi. Si unakumbuka kuwa Kikwete alijivunia kuwa pamoja na wapinzani kufanya vizuri bado wao walirudishwa madarakani wakiwa bado na wabunge wengi? Kama pipa lilikuwa linavuja kwa swababu ya tundu kubwa na watu wakajitahidi kuliziba likabakia tundu dogo, watashukuru kuwa "angalau sasa halivuji sana". CCM ilikuwa inahofia kuwa labda ingeambulia viti 3 au vitano tu lakini kama inachukua 'majority" ya viti vilivyogombaniwa bado wao watakuwa na sababu ya kufurahia.

Hoja inaweza kujengwa labda CDM hawahitaji kushangilia sana kwa sababu hawakufanya vizuri sana 'as expected'.
 
Kuna haja ya kuangalia upya matumizi ya mikutano ya hadhara. They are good, but not enough by themselves in the context of TZ politics.

Kitila labda niulize a very telling question: baada ya kampeni za 2010 na harakati za maandamano na M4C za sasa CDM ina jumla ya wanachama wangapi ambao wako active?
 
Shule ya kata haikukufundisha hesabu au wewe ni wa Visiwa vya Zimbabwe?

Kutoka viti viwili mpaka vitano ni ongezeko la asilimia 60.

3/5 x 100 = 60%

CCM, walikuwa na viti 27 wamenyang'anywa vitatu na hilo ni anguko kwa asilimia 11.1

3/27 x 100 = 11.1%

Bado huelewi?
CDM walikuwa na viti vingapi? ... halafu ndio viti vitatu viwe juu ya hiyo idadi ... CCM wamechukua cha CUF, usisahau hilo ... halafu ndo uje na hesabu zako za international school.
 
Namna nyingine ya kuangalia ni kuwa labda ujumbe wa CDM bado haujaeleweka sana, haujakubalika, au haujafikika vizuri kwa wananchi. Kama watu wangekuwa wanapima hamasa, na mikutano ya watu na jinsi ambavyo CDM jina lake limekuwa saturated kwenye jamii ya Watanzania ni wazi kuwa matokeo haya yalitakiwa yawe CCM viti 5 na CDM viti hivyo vingine. Matokeo haya yanaakisi yale ya Uchaguzi Mkuu ambapo pamoja na mengi sana CDM haikuweza hata kushinda viti 50 vya ubunge licha ya jina lake kutangaa sana mwaka 2010.

Jambo ambalo ni la hatari (kwa chama cha siasa) ni kuangalia "nje" yake kama sababu ya kutofanya vizuri zaidi. Kama CCM ikiwa dhaifu namna hii bado inaweza kushinda, itakuwaje ikija kupata nguvu?
Hivi mnapoisifia ccm kuwa bado ina nguvu mbona hamzungumzii rafu zake?kupiga wananchi na mambo mengine machafu ila kubwa zaidi ni JE?TUME YA UCHAGUZI IMEANDIKISHA LINI WAPIGA KURA WAPYA???
 
Mkuu Invisible kwa wataalamu wa lugha hii tunaiita kejeli. Yaan umeauliza swali ambalo lenyewe ndio jibu. Kifupi mhadhiri mwenzangu alipaswa afanye hayo uliyomuuliza na si kuja na visingizio vya Chama chake kushindwa.
Kama wewe kweli ni mhadhiri usingekuwa mropakaji kiasi hichi.
Wakati nyie mnachampana makonde sisi tunatafuta mbinu za kuzidi kupambana na nyie.

NB: weka mbali na watoto
.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Binafsi natazama CHADEMA kama chama ambacho kinakua hivyo bado kina nafasi ya kujitathmini na kuona ni kwa jinsi gani kinaweza kukabliana na changamoto mbalimbali.Ukitazama kwa uangalifu pengo la kura kwenye kata nyingi ambazo CCM imeshinda utagundua kwamba CDM inazidi kuimarika. Yapo maeneo ambayo CDM ilikuwa haina nguvu kabisa kipindi cha nyuma lakini matokeo haya yanadhihirisha kwamba nguvu ya CDM inazidi kuimarika.

Hoja ya Mabadiliko yapi ambayo CHADEMA inayaongoza ni jambo ambalo viongozi wa CHADEMA wanapaswa kuyapa kipaumbele ili hatimaye yaweze kuingia kwenye bongo za watanzania. Lazima mikutano ya CDM katika operesheni za chama ibebe hoja mahususi ambazo zitasimamiwa na kufafanuliwa kwa ufanisi,lazima tujenge agenda za kitaifa ambazo zitasimamia maslahi mapana ya wananchi na ambayo yataeleweka kwa mwananchi wa chini...
 
Shule ya kata haikukufundisha hesabu au wewe ni wa Visiwa vya Zimbabwe?

Kutoka viti viwili mpaka vitano ni ongezeko la asilimia 60.

3/5 x 100 = 60%

CCM, walikuwa na viti 27 wamenyang'anywa vitatu na hilo ni anguko kwa asilimia 11.1

3/27 x 100 = 11.1%

Bado huelewi?
Huwezi kusema chama kimepanda au kushuka kijumla kwa kutumia takwimu hizo za Kata 29. Kama uchaguzi ungefanyika kwenye kata zote nchi ndiyo angekuja na asilimia hizo. Kiufasaha alitakiwa kusema "kwenye uchaguzi huu CHADEMA imeongeza viti vya udiwani kwa asilimia 60 na CCM imepungukiwa viti vya udiwani kwa asilimia 11.1" kuliko kusema kiujumla kwamba hawa wamepanda au kushuka kwa asilimia fulani.

Halafu wakati mimi nasoma hizo shule zenu za Kata hazikuwepo!!
 
CDM walikuwa na viti vingapi? ... halafu ndio viti vitatu viwe juu ya hiyo idadi ... CCM wamechukua cha CUF, usisahau hilo ... halafu ndo uje na hesabu zako za international school.

Shida yako ni kubishana badala ya kulenga kuelewa.

Kutoka viti viwili mpaka vitano ni ongezeko la asilimia 60.
Au hiki ni kihindi?

Ongezeko la viti 3 linafanya jumla iwe viti vitano ambayo ni sawa na ongezeko la 60% au nini usichoelewa hapo?

Haya ngoja nikwambie ki-Kata School.

CDM walikuwa na viti 2 na baadaye vikaongezeka viti 3 kwa hiyo jumla ni viti 5.

Viti 3 kati ya jumla ya viti 5 ni ongezeko la 60%.

Karibu international school
 
Kitila labda niulize a very telling question: baada ya kampeni za 2010 na harakati za maandamano na M4C za sasa CDM ina jumla ya wanachama wangapi ambao wako active?

MM, hata kama chadema tumeongeza wanachama active mara kumi ya wale wa 2010 bado tuna wapiga kura wachache kwa sababu daftari la kudumu la wapiga kura halijafanyiwa marekebisho.
Unazani tangu 2010 mpaka sasa ni wangapi wametimiza maika 18 hasa ukizingatia chadema inaungwa mkono na vijana zaidi??

NB: weka mbali na watoto.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Huwezi kusema chama kimepanda au kushuka kijumla kwa kutumia takwimu hizo za Kata 29. Kama uchaguzi ungefanyika kwenye kata zote nchi ndiyo angekuja na asilimia hizo. Kiufasaha alitakiwa kusema "kwenye uchaguzi huu CHADEMA imeongeza viti vya udiwani kwa asilimia 60 na CCM imepungukiwa viti vya udiwani kwa asilimia 11.1" kuliko kusema kiujumla kwamba hawa wamepanda au kushuka kwa asilimia fulani.

Halafu wakati mimi nasoma hizo shule zenu za Kata hazikuwepo!!

Kwa hiyo wewe ndio umerekebisha eti?

Kwa hiyo ukipoteza jimbo kwenye uchaguzi mdogo unakuwa hujashuka hadi lipotee kwenye uchaguzi mkuu?
 
Mkuu Kitila,

Mimi nilitegemea CHADEMA kwa wakati huu na kwenye hizi chaguzi ndogo wawe wanashinda viti vingi kuliko ilivyotokea leo. Sababu kubwa ni kwamba tokea uchaguzi mkuu uishe 2010 CHADEMA imefanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha wananchi na CCM imekuwa ikikumbwa na mabalaa mengi tu.

Ni vigumu sana kuongelea kumetokea swing ya asilimia ngapi kwasababu Tanzania ya leo bado vyama vya upinzani havijawa na base yake. Ndio kwanza vinaitengeneza sasa. Tunaweza kusema kwamba sasa positioning ndio kwanza inachukua nafasi. Wanachama wanajipanga huku na kule na kufikia 2015 vyama vitakuwa na base yake na baada ya hapo itakuwa rahisi kuongelea wanachama kiasi gani wamebadilisha position.

Ni rahisi sana kwenye hizi chaguzi ndogo kwa CHADEMA kutumia resources zote kuweza kuziendesha. Slaa na Mbowe wamekuwa wakizunguka kila sehemu pamoja na akina Zitto na wabunge wengine. Ikifika uchaguzi wa 2015 kila mtu atakuwa busy kwake na hivyo utakuwa mgumu hata zaidi.

Kwa haya matokeo ya leo sio siri CCM watafurahi sana. Kwa kuangalia uwingi wa watu wanaohudhuria mikutano ya CHADEMA, kulikuwa na uwezekano wa CCM kupoteza karibu kata zote hizi na hapo domino effect ingechukua nafasi yake. Lakini kwasababu ambazo wachunguzi wa mambo ya siasa wanaweza kuzitafuta, hilo halijatokea na kwa CCM wengi hili litawatia nguvu sana. Ni kama somehow wamefanikiwa kulisimamisha gurudumu la kuwaporomosha chini ya mwamba.

Siasa ni ngumu sana na bado tuna safari ndefu kabla ya kufikia mahali ambapo wananchi wetu watakuwa huru zaidi na kuweza kuchagua sera ambazo zina mshiko zaidi kwao na sio ushabiki wa kisiasa kama ilivyo sasa.
 
MM, hata kama chadema tumeongeza wanachama active mara kumi ya wale wa 2010 bado tuna wapiga kura wachache kwa sababu daftari la kudumu la wapiga kura halijafanyiwa marekebisho.

Unazani tangu 2010 mpaka sasa ni wangapi wametimiza maika 18 hasa ukizingatia chadema inaungwa mkono na vijana zaidi??

NB: weka mbali na watoto.

...Na ukweli ni kwamba CCM ina mtaji mkubwa wa wanachama/wafuasi ambao hawako tayari kuona mabadiliko na wako well committed katika kupiga kura tofauti na CDM.
 
Mi nadhani sababu kubwa ya CHADEMA kutofanya vizuri zaidi ni moja Kuu

1. DAFTARI LA WAPIGA KURA HALIJABORESHWA TOKA UCHAGUZI WA 2010 HIVYO WAPIGA KURA NI WALE WALE WANAOPIGA KURA KWA MAZOEA

2.Nadhani CHADEMA WAMEONGEZA WAPIGA KURA WENGI WAPYA KUTOKANA NA OPERATION A
MBAO NI VIJANA AMBAO HAWJAPATA NAFASI YA KUANDIKISHWA KUTOKANA NA KUTOBORESHWA KWA DAFTARI LA WAPIGA KURA HIVYO WALIKUWA WANAGOMBANIA WAPIGA KURA WALE WALE AMBAO NI CCM HOME TURF

CHADEMA WATAFANYA MAKUBWA IKIWA IT'S BASE AMBAO NI VIJANA WATAWEZA KUANDIKISHWA LAKINI KWA DAFTARI HILI LA SASA NI KUPAPATUANA NA MAGAMBA.
 
Nikiangalia margin ya kule chadema ilikoshindwa bado inatia matumaini. Hadi sasa au kwa makusudi au kwa bahati mbaya bado tume ya uchaguzi haitaki kuboresha daftari la kupiga kura.
Nategemea wajinga watapungua kadri daftari hilo litakavyoboreshwa. Na wengi wa walioamka hawakuwa katika daftari hiyo. All the fortune Chadema.
Pole Chama cha migumi tanzania
 
Mkuu Kitila,

Mimi nilitegemea CHADEMA kwa wakati huu na kwenye hizi chaguzi ndogo wawe wanashinda viti vingi kuliko ilivyotokea leo. Sababu kubwa ni kwamba tokea uchaguzi mkuu uishe 2010 CHADEMA imefanya kazi kubwa sana ya kuhamasisha wananchi na CCM imekuwa ikikumbwa na mabalaa mengi tu.

Ni vigumu sana kuongelea kumetokea swing ya asilimia ngapi kwasababu Tanzania ya leo bado vyama vya upinzani havijawa na base yake. Ndio kwanza vinaitengeneza sasa. Tunaweza kusema kwamba sasa positioning ndio kwanza inachukua nafasi. Wanachama wanajipanga huku na kule na kufikia 2015 vyama vitakuwa na base yake na baada ya hapo itakuwa rahisi kuongelea wanachama kiasi gani wamebadilisha position.

Ni rahisi sana kwenye hizi chaguzi ndogo kwa CHADEMA kutumia resources zote kuweza kuziendesha. Slaa na Mbowe wamekuwa wakizunguka kila sehemu pamoja na akina Zitto na wabunge wengine. Ikifika uchaguzi wa 2015 kila mtu atakuwa busy kwake na hivyo utakuwa mgumu hata zaidi.

Kwa haya matokeo ya leo sio siri CCM watafurahi sana. Kwa kuangalia uwingi wa watu wanaohudhuria mikutano ya CHADEMA, kulikuwa na uwezekano wa CCM kupoteza karibu kata zote hizi na hapo domino effect ingechukua nafasi yake. Lakini kwasababu ambazo wachunguzi wa mambo ya siasa wanaweza kuzitafuta, hilo halijatokea na kwa CCM wengi hili litawatia nguvu sana. Ni kama somehow wamefanikiwa kulisimamisha gurudumu la kuwaporomosha chini ya mwamba.

Siasa ni ngumu sana na bado tuna safari ndefu kabla ya kufikia mahali ambapo wananchi wetu watakuwa huru zaidi na kuweza kuchagua sera ambazo zina mshiko zaidi kwao na sio ushabiki wa kisiasa kama ilivyo sasa.

Nafikiri kinachokwamisha ni maboresho ya daftari la wapiga kura. Ongezeko ambalo CDM inalitegemea ni la vijana. Kwa siasa zetu na moyo wa Watanzania, wale waliokuwa pro-CCM hawahamii CDM, badala yake baada ya kuuelewa ukweli, wanakuwa disappointed na kususia suala zima la siasa
 
Namna nyingine ya kuangalia ni kuwa labda ujumbe wa CDM bado haujaeleweka sana, haujakubalika, au haujafikika vizuri kwa wananchi.

Kama watu wangekuwa wanapima hamasa, na mikutano ya watu na jinsi ambavyo CDM jina lake limekuwa saturated kwenye jamii ya Watanzania ni wazi kuwa matokeo haya yalitakiwa yawe CCM viti 5 na CDM viti hivyo vingine. Matokeo haya yanaakisi yale ya Uchaguzi Mkuu ambapo pamoja na mengi sana CDM haikuweza hata kushinda viti 50 vya ubunge licha ya jina lake kutangaa sana mwaka 2010.

Jambo ambalo ni la hatari (kwa chama cha siasa) ni kuangalia "nje" yake kama sababu ya kutofanya vizuri zaidi. Kama CCM ikiwa dhaifu namna hii bado inaweza kushinda, itakuwaje ikija kupata nguvu?

Mzee Mwanakijiji umefanya Political Analysis, Kitila Mkumbo amefanya Poritical Analiziz ambayo haipo mahala popote duniani, yaani ukweli anauona halafu anajitahidi kuukimbia
 
Hivi mnapoisifia ccm kuwa bado ina nguvu mbona hamzungumzii rafu zake?kupiga wananchi na mambo mengine machafu ila kubwa zaidi ni JE?TUME YA UCHAGUZI IMEANDIKISHA LINI WAPIGA KURA WAPYA???

CDM ilipoenda kwenye uchaguzi ilikuwa haijui hili?
 
Mtanzania,

Kazi ya kujenga upinzani katika mazingira ya kwetu ni kubwa na ngumu kuliko tunavyoiona. Huko tulikotoka ilikuwa ni miujiza kushinda udiwani kwa sehemu kama Mvomero. Leo tumefikia hatua ya kuwanyang'anya CCM viti vya udiwani pamoja na mateso, uhuni na hila zote si jambo dogo. Safari bado lakini ni kweli pia tumetoka mbali.
 
Back
Top Bottom