Mparee2
JF-Expert Member
- Sep 2, 2012
- 2,590
- 4,277
Tumekuwa na wasomi wangazi za juu (Masters na phd) wengi sana wana maliza kila mwaka; Ila inavyo onekana kuna baadhi ya tafiti hazina umuhimu wowote wa maana kwa maisha ya watanzania
Natamani:
1. Vyuo viwe na maono ya kufanya tafiti nyingi za kutatua changamoto za watanzania kwa sasa tuachane na copy paste ya vya wazungu kwani mengi hayaendani kabisa na watanzania (waafrica) (culture, uchumi, elimu, mazingira nk)
2. Serikali iweke TV channel au niseme ukurasa rasmi wa tafiti Bora labda 50 kila mwaka zilizopitishwa na zenye manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania ili watu wazifuatilie . Itaweza kuwa kama discovery channel ya Tz
3. Kwa umuhimu hatuna haja ya mtanzania aliyepo hapa nyumbani kupoteza muda kutafiti kwenda mbingu ya pili (juu ya jua) wakati hata utafiti wa kawaida kabisa bado
4. Huwa napata aibu kusikia msomi wa chuo kikuu anajisifia amegundua kutengeneza helcopter ya mabati ya msouth au pengine gari nk tena lenye ufanisi wa chini pengine niseme 25%
Ningetamani kusikia amegundua gari lenye ufanisi wa hali ya juu ukilinganisha na yaliyopo sokoni kwa sasa mf: Fuso inayotumia mafuta lita moja kwa umbali wa kilometa 25 huku ikiwa imebeba tani 7 nk.
5. Pengine niseme, wajikite katika ugunduzi wa machine rahisi za kusaidia wananchi kama; kuonesha samaki walipo kwenye maziwa, au pengine Nguo zisizo ungua kwa ajili ya watu wa faya, Baiskeli za walemavu za kutumia umeme wa jua, Baiskeli za kuchage, ukuzaji wa mazao bila mbolea au niseme mbolea kidogo nk. Bandari yetu imekosa wasomi wa kushauri wakati kuna vyuo vya bandani nk hata sijui wanatafiti nini? nk nk nk
6. Ushauri wangu: Wasomi wafanye tafiti kwa masomo ambayo wana msingi nayo kuanzia level ya chini (Diploma/ bachelor) ndio tutapata tafiti muafaka na sio zile za copy edit
Unakuta mtu kasoma kozi zake za arts (barchelor & masters) eti kaja kufanya kautafiti kautalii (Tourism) sijui ilikuwa culture in tourism eti tayari anachukuliwa ni mbobezi wa utalii wakati kimsingi anajua labda 15% ya biashara ya utalii; Shame!