Tafiti za wasomi zisaidie Taifa

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,512
4,129
Tumekuwa na wasomi wangazi za juu (Masters na phd) wengi sana wana maliza kila mwaka; Ila inavyo onekana kuna baadhi ya tafiti hazina umuhimu wowote wa maana kwa maisha ya watanzania
Natamani:

1. Vyuo viwe na maono ya kufanya tafiti nyingi za kutatua changamoto za watanzania kwa sasa tuachane na copy paste ya vya wazungu kwani mengi hayaendani kabisa na watanzania (waafrica) (culture, uchumi, elimu, mazingira nk)

2. Serikali iweke TV channel au niseme ukurasa rasmi wa tafiti Bora labda 50 kila mwaka zilizopitishwa na zenye manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania ili watu wazifuatilie . Itaweza kuwa kama discovery channel ya Tz

3. Kwa umuhimu hatuna haja ya mtanzania aliyepo hapa nyumbani kupoteza muda kutafiti kwenda mbingu ya pili (juu ya jua) wakati hata utafiti wa kawaida kabisa bado

4. Huwa napata aibu kusikia msomi wa chuo kikuu anajisifia amegundua kutengeneza helcopter ya mabati ya msouth au pengine gari nk tena lenye ufanisi wa chini pengine niseme 25%
Ningetamani kusikia amegundua gari lenye ufanisi wa hali ya juu ukilinganisha na yaliyopo sokoni kwa sasa mf: Fuso inayotumia mafuta lita moja kwa umbali wa kilometa 25 huku ikiwa imebeba tani 7 nk.

5. Pengine niseme, wajikite katika ugunduzi wa machine rahisi za kusaidia wananchi kama; kuonesha samaki walipo kwenye maziwa, au pengine Nguo zisizo ungua kwa ajili ya watu wa faya, Baiskeli za walemavu za kutumia umeme wa jua, Baiskeli za kuchage, ukuzaji wa mazao bila mbolea au niseme mbolea kidogo nk. Bandari yetu imekosa wasomi wa kushauri wakati kuna vyuo vya bandani nk hata sijui wanatafiti nini? nk nk nk

6. Ushauri wangu: Wasomi wafanye tafiti kwa masomo ambayo wana msingi nayo kuanzia level ya chini (Diploma/ bachelor) ndio tutapata tafiti muafaka na sio zile za copy edit
Unakuta mtu kasoma kozi zake za arts (barchelor & masters) eti kaja kufanya kautafiti kautalii (Tourism) sijui ilikuwa culture in tourism eti tayari anachukuliwa ni mbobezi wa utalii wakati kimsingi anajua labda 15% ya biashara ya utalii; Shame!
 
Nakubaliana na wewe mkuu.

Nafikiri pia kuwepo na desturi ya kuandaa conference mbali mbali ili watu wapate nafasi za kuprent tafiti zao (hizo presentations za tafiti zirushwe live kwenye television ili watanzania waweze kujifunza zaidi)

Au Serikali ije na mpango wa kuanzisha channel maalumu kwa ajili ya kuonyesha tafiti za wataalam mbali mbali kama ilivyo channel ya Tanzania Safari inayoonesha shughuli za utalii.
 
Tafiti hizi za watu Kama wakina prof.dump (Kabudi) zitasaidia nini taifa mkuu na zile za SUA za panya
Kuna tafiti zinagusa maisha ya mwanadamu directly mfano ule utafiti uliofanyika mwanza kwenye juice ya miwa na kujulikana kuwa ile juice ina Bacteria.
Tayari hiyo ni advantage kwa watu ili kupunguza magonjwa.
 
" ukuzaji wa mazao bila mbolea, gari lenye ufanisi 125%" Wewe Mwandishi utakuwa mmoja wa wasomi unaowalalamikia.
Kuelewa mawazo makubwa unatakiwa uwe na uwezo mkubwa pia wa kuona next century
Nakumbuka Guglielmo Marconi alivyo kuwa anafanya utafiti uliopelekea ugunduzi wa radio, watu wengi wa mawazo madogo walimuona kichaa kuwa sauti itawezaje kufika upande wa pili bila kiunganishi; the same to mobile phones tena miaka 1960s pengine baba yako akiwa shule!
Umewahi kufikiria ajali nyingi za nyumba kuungua kwa mawaya ya umeme kuchubuka au pengine kuliwa na panya; hebu fikiria utafiti wa kusambaza umeme kwenye nyumba bila kutumia nyaya? Engineers tunao kibao tena kila siku utasikia masters, phd, doctorate, nk? Think Big Brother, sio kila kitu kusubiri wazungu wagundue!!!
 
Kuna tafiti zinagusa maisha ya mwanadamu directly mfano ule utafiti uliofanyika mwanza kwenye juice ya miwa na kujulikana kuwa ile juice ina Bacteria.
Tayari hiyo ni advantage kwa watu ili kupunguza magonjwa.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
Miwa mingi inalimwa kwenye maji taka au madimbwi yanayozunguka makazi unategemea usikute hao wadudu???
 
Tafiti zao hazitasaidia sababu siasa ndiyo inayoendesha maisha yetu...
 
Zaidi ya 99% ya tafiti za wasomi wa kitanzania ni quantitative kind of; kutembeza madodoso. Qualitative researches ndio hasa zinazoipeleka dunia mbele; kuibua theories mpya etc.
 
Naamini hizo tafiti zikiwekwa wazi kila mwaka kwenye Live channel, tutaona vitu vya ajabu na hapo wataalam watapata changamoto ya kujirekebisha na kufanya tafiti za kuletea watu maendeleo
Mimi natamani twende na tafiti rahisi za kusaidia wananchi na kukuza uchumi fasta; mfano;
Ukienda kilimanjaro na hata bukoba, ndizi mshale zinapungua kwa kasi; hakuna mtalaam amekwenda kule kufanya utafiti na kupendekeza nini kifanyike au pengine kuja na aina mbadala inayohimili mabadiliko ya hali ya hewa na magonjwa. Lakini muhimu zaidi matokeo ya hizo tafiti yawafikie wananchi nasio kuishia kwenye makabrasha
Tafiti za kutengeneza ndege za kutumia mwanga wa jua na nyingine kama hizo, tungeweka pembeni kwanza. Tuanze na haya yanayo tuongezea umasikini, tuki improve huku chini hayo mengine yatakuja yenyewe...hatuoni china?
 
Tafiti hizi za watu Kama wakina prof.dump (Kabudi) zitasaidia nini taifa mkuu na zile za SUA za panya
Tafiti za panya pale SUA zimefadhiliwa na mabeberu na ndio maana wanafanya yale waliyo ambiwa na mabeberu.

Sasa nikupe swali wewe serikali yako imechangia kiasi gani kwenye tafiti?
 
Tumekuwa na wasomi wangazi za juu (Masters na phd) wengi sana wana maliza kila mwaka; Ila inavyo onekana kuna baadhi ya tafiti hazina umuhimu wowote wa maana kwa maisha ya watanzania
Natamani:

1. Vyuo viwe na maono ya kufanya tafiti nyingi za kutatua changamoto za watanzania kwa sasa tuachane na copy paste ya vya wazungu kwani mengi hayaendani kabisa na watanzania (waafrica) (culture, uchumi, elimu, mazingira nk)

2. Serikali iweke TV channel au niseme ukurasa rasmi wa tafiti Bora labda 50 kila mwaka zilizopitishwa na zenye manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania ili watu wazifuatilie . Itaweza kuwa kama discovery channel ya Tz

3. Kwa umuhimu hatuna haja ya mtanzania aliyepo hapa nyumbani kupoteza muda kutafiti kwenda mbingu ya pili (juu ya jua) wakati hata utafiti wa kawaida kabisa bado

4. Huwa napata aibu kusikia msomi wa chuo kikuu anajisifia amegundua kutengeneza helcopter ya mabati ya msouth au pengine gari nk tena lenye ufanisi wa chini pengine niseme 25%
Ningetamani kusikia amegundua gari lenye ufanisi wa hali ya juu ukilinganisha na yaliyopo sokoni kwa sasa mf: Fuso inayotumia mafuta lita moja kwa umbali wa kilometa 25 huku ikiwa imebeba tani 7 nk.

5. Pengine niseme, wajikite katika ugunduzi wa machine rahisi za kusaidia wananchi kama; kuonesha samaki walipo kwenye maziwa, au pengine Nguo zisizo ungua kwa ajili ya watu wa faya, Baiskeli za walemavu za kutumia umeme wa jua, Baiskeli za kuchage, ukuzaji wa mazao bila mbolea au niseme mbolea kidogo nk. Bandari yetu imekosa wasomi wa kushauri wakati kuna vyuo vya bandani nk hata sijui wanatafiti nini? nk nk nk

6. Ushauri wangu: Wasomi wafanye tafiti kwa masomo ambayo wana msingi nayo kuanzia level ya chini (Diploma/ bachelor) ndio tutapata tafiti muafaka na sio zile za copy edit
Unakuta mtu kasoma kozi zake za arts (barchelor & masters) eti kaja kufanya kautafiti kautalii (Tourism) sijui ilikuwa culture in tourism eti tayari anachukuliwa ni mbobezi wa utalii wakati kimsingi anajua labda 15% ya biashara ya utalii; Shame!
Ukisoma zile docs ni partial fulfillment , mtu amejilipia ada yake anasoma,

Ukitaka research za unachokisema ww bas serikali si budi iweke fungu ku fund izo study,
 
Hahaha! Masters! Phd ° haya.
 
Naamini hizo tafiti zikiwekwa wazi kila mwaka kwenye Live channel, tutaona vitu vya ajabu na hapo wataalam watapata changamoto ya kujirekebisha na kufanya tafiti za kuletea watu maendeleo
Mimi natamani twende na tafiti rahisi za kusaidia wananchi na kukuza uchumi fasta; mfano;
Ukienda kilimanjaro na hata bukoba, ndizi mshale zinapungua kwa kasi; hakuna mtalaam amekwenda kule kufanya utafiti na kupendekeza nini kifanyike au pengine kuja na aina mbadala inayohimili mabadiliko ya hali ya hewa na magonjwa. Lakini muhimu zaidi matokeo ya hizo tafiti yawafikie wananchi nasio kuishia kwenye makabrasha
Tafiti za kutengeneza ndege za kutumia mwanga wa jua na nyingine kama hizo, tungeweka pembeni kwanza. Tuanze na haya yanayo tuongezea umasikini, tuki improve huku chini hayo mengine yatakuja yenyewe...hatuoni china?
Mkuu tafiti inahitaji bajeti kubwa sana, kuna tafiti moja ya shirika tulifanya unapewa siku 2 ukusanye na kuchakata data za field husika unadhani hapo utapata meaningful findings zaidi ya kulipua tu!!

Bajeti ya utafiti ilikubaliwa iwe 1% ya bajeti ya serikali yaani walau 300 B!! Lakini unakuta imetengewa maybe 20 B unadhani hapo tafiti Gani itafanyika? Hapo Bado vibali kama vyote Ili ukusanye data!! Sheria ya takwimu nayo ikubane!!

Nadhani barriers ni nyingi hasa bajeti na sheria zetu ila kulaumu wasomi sidhani kama ni njia sahihi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom