Tafiti za kisayansi

fredyyboy

Member
Jan 26, 2021
23
40
Habari zenu wakuu

Nimekuja kwenu nikiamini hapa Kuna wataalamu Wana sayansi bomba wenye ujuzi na maarifa mengi
Nilikua naomba ushauri kwenu nipo chuo na nimetumia muda mwingi kufanya tafiti na Moja ya tafiti ninayoifanya ni namna Gani nitafanya niweze badili Karatasi kuwa mbolea? Kwenye karatasi kuna carbon nyingi hapa naitaji mbinu ya kuongeza ammonia kwenye hayo makaratasi Kuna watu hapa wametengeneza Kwa kuchanganya makaratasi na mikojo mbolea yao ndo inaongoza kusifika Kwa saivi me nataka nije na kitu kipya!

huku Kuna watu wamebuni kutengeneza biskuti za asali
Sabuni za maji na kipande
Wengine wamegundua hormone za kuangualia mayai ya samaki
Water cycling
Mafuta ya parachich
Soya meat
Automated sperm collector

Vitu vingo hivyo ninachoitaji kutoka kwenu Wana jamii muweze kuchangia mawazo yenu je ni tafiti Gani ya sayansi tunaweza buni na kutengeneza kitu Mniambie tu Mimi ntafanyia kazi Kila mawazo yenu muhimu tuunde kitu cha kueleweka na chenye manufaa kwa jamii yetu.

Ahsante.
 
Aisee kwanza ningekutandika Kofi ili akili ikae sawa..Karatasi(Paper) to Manure kisa ina Carbon? Je ni aina gani ya Carbon ni Chemical au Solid ama Gas..Je ukichambua Molecule ya Paper unaona kuna uwezekano wa kuongeza Ammonium kwenye hiyo molecule?

Je unaongelea karatasi zipi hizi za Madaftari na white A4? Labda uifanyie ile process ya kuchachusha inaitwaje?Nimesahau chemistry siku nyingi sana ila Karatasi ukiizika inaoza na kuwa fossil hivyo hapo ndo unaweza kupata wazo la ku-recycle na kuwa Mbolea
 
Nimekuja mbio mbio, Nimejua labda ni tafiti za mambalo ya energy, nuclear power, NL kumbe bado tupo kwenye kubadilisha karatasi kua mbolea na mambo ta asali

Sio mbaya. Scientific research mara nyingi ni paper. Je umeandika paper kuhusi hizo tafiti?, Siku ukipotea na tafiti zako ninapotea au zipo wapi?, Nikitaka kubadilisha karatasi kuwa mbolea mpaka nikutafute unifundishe, hamana sehemu umeandia process, procedures etc?

Kuna kipindi niliona Nigeria watu wanabadilisha mihogo kua mkaa, ladba anzia hapa
 
Aisee kwanza ningekutandika Kofi ili akili ikae sawa..Karatasi(Paper) to Manure kisa ina Carbon? Je ni aina gani ya Carbon ni Chemical au Solid ama Gas..Je ukichambua Molecule ya Paper unaona kuna uwezekano wa kuongeza Ammonium kwenye hiyo molecule?

Je unaongelea karatasi zipi hizi za Madaftari na white A4? Labda uifanyie ile process ya kuchachusha inaitwaje?Nimesahau chemistry siku nyingi sana ila Karatasi ukiizika inaoza na kuwa fossil hivyo hapo ndo unaweza kupata wazo la ku-recycle na kuwa Mbolea
Sawa mkuu lakini umeelewa nilichimaanisha inshort naitaji idea zenu wadau.
 
Back
Top Bottom