Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,638
- 697,938
Neno la utangulizi: TULIKOSEA PAKUBWA MNO TULIPOIPA SIASA THAMANI KUBWA KULIKO TAALUMA! Leo hii wanasiasa wana nguvu kubwa kuliko wanataaluma wetu.
Jambo linapokuwa kubwa huja na makubwa mengi pia. Corona imetuletea mengi, mazuri na mabaya ya kushangaza na ya kutia simanzi pia.
Vita ya maneno bado inaendelea kati ya wanasiasa wetu na wafadhili wetu wadau wa maendeleo yetu hawa mabwana wakubwa tunaowaita mabeberu.
Tunajaribu kuwatisha na kuwaaminisha wananchi wetu kuwa chanjo ya Corona ni mbaya na haifai lakini kamwe hatuwaoneshi ithibati thabiti ya kitaalam kuhusu ubaya wa chanjo.
Tunatumia nguvu nyingi kisiasa kupinga chanjo eti zina madhara kiafya lakini kuna maeneo mengi muhimu yanayohusika na afya ya mtanzania tumeyafumbia macho.
1. Viwango vyetu vya tiba ni hafifu na vya hali ya chini mno: Hatujawekeza vya kutosha kwenye hili eneo. Wananchi wanaathiriwa pakubwa na huduma mbovu za afya, madawa bandia na madawa yasiyokidhi viwango. Wataalam wasio na ujuzi kamili na watoa huduma wasiokidhu viwango.
2. Vyakula na vinywaji: Kila wakati tunaletewa aina mpya ya vyakula na vinywaji vinavyorembwa na kila aina ya uzuri lakini baada ya muda watu wanapoanza kupata madhara serikali ndio huchukua hatua. Mwanzoni kodi na mapato ndio kipaumbele sio afya na usalama wa Mtanzania.
3. Vipodozi na mapambo ya mwili. Hili ni eneo hatarishi mno kwa afya zetu lakini mkono wa serikali uko wapi hapa? Watu wanaathirika mno. Vipodozi bandia na vyenye kemikali za sumu viko kila mahali, lakini kipaumbele ni kodi na mapato
4. Vinywaji: Hapa hata sijui nisemeje..kila siku tunawaangamiza vijana wetu nguvu kazi ya taifa kwa vinywaji vikali vibaya kwa afya, lakini vipo madukani na vina stakabadhi ya kodi za serikali.
5. Vyakula vya wanyama: Nani alisejua haya makuku tunayoita ya kizungu yalivyo na madhara makubwa kiafya. Shida inaanzia kwenye vyakula, lakini hatuoni serikali yetu ikipiga kelele hapa.
Tuna vingi vingi vibaya vinavyotuangamiza kila siku mbele ya macho ya serikali. Mitumba ya kila aina toka ulaya kuanzia mavazi vyombo vya usafiri mpaka vyombo vya ndani.
Zaidi ya asilia sabini ya madawa na vifaa tiba vinatoka nje. Pembejeo za kilimo pia. Sisi ni tegemezi wa hao watoa chanjo kwa asilimia 95. Kukataa chanjo kwa kisingizio cha madhara na bila ithibati hatuwatendei haki wananchi wengi wanaoangamia na mengi kila uchao
Huduma za kijamii ni mbovu. Maji safi na salama ni wangapi tunapata?
Sisi ni wafu hata kabla hatujauawa