Tafakuri yangu juu ya chanjo ya Corona

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,606
696,729
Neno la utangulizi: TULIKOSEA PAKUBWA MNO TULIPOIPA SIASA THAMANI KUBWA KULIKO TAALUMA! Leo hii wanasiasa wana nguvu kubwa kuliko wanataaluma wetu.

Jambo linapokuwa kubwa huja na makubwa mengi pia. Corona imetuletea mengi, mazuri na mabaya ya kushangaza na ya kutia simanzi pia.

Vita ya maneno bado inaendelea kati ya wanasiasa wetu na wafadhili wetu wadau wa maendeleo yetu hawa mabwana wakubwa tunaowaita mabeberu.

Tunajaribu kuwatisha na kuwaaminisha wananchi wetu kuwa chanjo ya Corona ni mbaya na haifai lakini kamwe hatuwaoneshi ithibati thabiti ya kitaalam kuhusu ubaya wa chanjo.

Tunatumia nguvu nyingi kisiasa kupinga chanjo eti zina madhara kiafya lakini kuna maeneo mengi muhimu yanayohusika na afya ya mtanzania tumeyafumbia macho.

1. Viwango vyetu vya tiba ni hafifu na vya hali ya chini mno: Hatujawekeza vya kutosha kwenye hili eneo. Wananchi wanaathiriwa pakubwa na huduma mbovu za afya, madawa bandia na madawa yasiyokidhi viwango. Wataalam wasio na ujuzi kamili na watoa huduma wasiokidhu viwango.

2. Vyakula na vinywaji: Kila wakati tunaletewa aina mpya ya vyakula na vinywaji vinavyorembwa na kila aina ya uzuri lakini baada ya muda watu wanapoanza kupata madhara serikali ndio huchukua hatua. Mwanzoni kodi na mapato ndio kipaumbele sio afya na usalama wa Mtanzania.

3. Vipodozi na mapambo ya mwili. Hili ni eneo hatarishi mno kwa afya zetu lakini mkono wa serikali uko wapi hapa? Watu wanaathirika mno. Vipodozi bandia na vyenye kemikali za sumu viko kila mahali, lakini kipaumbele ni kodi na mapato

4. Vinywaji: Hapa hata sijui nisemeje..kila siku tunawaangamiza vijana wetu nguvu kazi ya taifa kwa vinywaji vikali vibaya kwa afya, lakini vipo madukani na vina stakabadhi ya kodi za serikali.

5. Vyakula vya wanyama: Nani alisejua haya makuku tunayoita ya kizungu yalivyo na madhara makubwa kiafya. Shida inaanzia kwenye vyakula, lakini hatuoni serikali yetu ikipiga kelele hapa.

Tuna vingi vingi vibaya vinavyotuangamiza kila siku mbele ya macho ya serikali. Mitumba ya kila aina toka ulaya kuanzia mavazi vyombo vya usafiri mpaka vyombo vya ndani.

Zaidi ya asilia sabini ya madawa na vifaa tiba vinatoka nje. Pembejeo za kilimo pia. Sisi ni tegemezi wa hao watoa chanjo kwa asilimia 95. Kukataa chanjo kwa kisingizio cha madhara na bila ithibati hatuwatendei haki wananchi wengi wanaoangamia na mengi kila uchao

Huduma za kijamii ni mbovu. Maji safi na salama ni wangapi tunapata?

Sisi ni wafu hata kabla hatujauawa
 
Nadhani huyo jamaa yenu ana shida kwenye reasoning.

Viatu alivyovaa ni vikubwa sana.
 
Leo asubuhi wakati nasubiri usafiri nikaskia wananchi wakimpongeza mkulu ati amedhibiti dawa za mabeberu ati ya kua amewastukia mabeberu mapema hivyo anastahili pongezi. Lakini hapohapo wakaanza kugusia vile gonjwa linakua na hali za ndgu jamaa na marafiki zao kiafya kua kuna muda wanajihisi wana huo ugonjwa lakini kwa kudra za M/Mungu anawaweka hai.

Hapo nikaamini apa nchini kitu kikisemwa na mtu wa ngazi za juu kama Mr. Mitano tena aisee watu wanaamini 100% kwa moyo wote hata kama wanaona kuna vikasoro ila wapi wanalazimisha mioyo na akili zao zikubali alichosema mkulu. Wataunganisha dots za uongo na ukweli ili tu alichosema kionekane ni kweli.
 
Tulipokosea ni Pale tulipoipa siasa hadhi na thamani kubwa kuliko taaluma..leo hii mwanasiasa anasilikizwa na ana nguvu kuliko daktari bingwa
 
Upo sahihi mkuu, raisi wa zamani wa south Africa Thabo Mbeki aliwahi kuzungumzia kuhusu UKIMWI unakumbuka kilichotokea?
 
Na sio Kila kitu unacholetewa ukubali.
Vita ya chanjo sio Tanzania tu hata huko ulaya na marekani ipo.
Kuna watu wanamlaumu bill gates kuwa katengeneza Corona ili apige hela.
huu ugonjwa sio wa mungu ni wa binadamu ameutengeneza makusudi kwa maslahi yake binafsi
Leo wanakata CHANJO. kesho wanaagiza dawa kutoka huko huko,

Baniani mbaya ila kiatu chake dawa

"Only time will tell"
 
Tulipokosea ni Pale tulipoipa siasa hadhi na thamani kubwa kuliko taaluma..leo hii mwanasiasa anasilikizwa na ana nguvu kuliko daktari bingwa
Mgosi hii sentensi ina uzito wa kipekee. Yaani Mbunge anayejua tu kusoma na kuandika analipwa mshahara mkubwa kuliko Profesa wa chuo kikuu!!

Binadamu mmoja tu ana maamuzi makubwa na ya mwisho ndani ya nchi kuliko watu milioni 50!! Kiasi cha kufananishwa na mungu mtu!! Kazi kweli kweli.
 
Yah Zuma kwenye ile skendo yake ya kubaka, walimpima demu akakutwa na ngoma. Walivyo mpima Zuma hakukutwa nayo, wakamuulizi Mr President imekuwaje umemtia demu mwenye ngoma alafu we unjaipata!!... Akajibu nilipomaliza nilienda kuoga maji ya moto,
African presidents
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom