Kwa waliochanja Chanjo ya CORONA Njoni mtoe uzoefu Ili tupime ufanisi.

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
15,106
22,554
Salaam, Shalom.

Kwa mara ya kwanza, Nchi yetu ilipokea Rasmi Chanjo ya CORONA virus Kutoka nje aina ya Johnson Johnson mnamo July 24, 2021.

Na Chanjo Ile sie tulipewa Bure tofauti na Nchi zingine kama DRC, wao wakinunua Chanjo Kwa kugombania kuhofia kufa Kwa Corona.

Hadi sasa imebaki miezi 4, yaani July 2024, kukamilisha miaka mitatu tangu kuingia Chanjo na kuanza zoezi Hilo la Chanjo nchini.

Asilimia kubwa ya walipinga Chanjo hizo walidai kuwa,madhara ya Chanjo hizo yataanza kuonekana dhahiri baada ya miaka mitatu tangu kupata Chanjo hizo.

Ni ombi LANGU, Kwa wote mliopata Chanjo hizo, piteni hapa na Kutoa uzoefu wa MAISHA kabla ya Chanjo na maisha baada ya Chanjo ya CORONA.

Tusaidieni kujibu maswali yafuatayo;

1. Ulichanja Chanjo ya coronavirus?

2. Je, AFYA zenu na za ndugu zenu zimeimarika zaidi na kuepuka kuugua kama zamani kabla ya Kupata Chanjo?

3. Changamoto mlizozipata ndani ya muda wa Chanjo Kwa miaka hii karibia mitatu ni zipi?

4. Faida mlizopata baada ya kuchanja kiafya ni zipi kulinganisha na kabla ya kuchanja?

Karibuni 🙏
 
Mimi nililaImkika kuchanja kwa kuwa nilikuwa na safari nje ya Tanzania kwa hiyo sikuwa namna.

Ukweli ni kwamba hakuna madhara yoyote niliyopata au nayapata. Nina miaka takribani 15 sijawahi kwenda hospital kwa tatizo lolote la kiafya
Chanjo ya CORONA Haina miaka 15,

Labda tuseme una AFYA njema inayochaguzwa na blood group na Ulinzi wa Mungu.

Hujaona tofauti yoyote mwilini ukilinganisha time uliyochanja na kabla ya kuchanja?
 
Salaam, Shalom.

Kwa mara ya kwanza, Nchi yetu ilipokea Rasmi Chanjo ya CORONA virus Kutoka nje aina ya Johnson Johnson mnamo July 24, 2021.

Hadi sasa imebaki miezi 4 kukamilisha miaka mitatu tangu kuingia Chanjo nchini na kuanza zoezi Hilo la Chanjo nchini.

Asilimia kubwa ya walipinga Chanjo hizo walidai kuwa,madhara ya Chanjo hizo yataanza kuonekana dhahiri baada ya miaka mitatu tangu kupata Chanjo hizo.

Ni ombi LANGU, Kwa wote mliopata Chanjo hizo, piteni hapa na Kutoa uzoefu wa MAISHA kabla ya Chanjo na maisha baada ya Chanjo ya CORONA.

Tusaidieni kujibu maswali yafuatayo;

1. Je, AFYA zenu na za ndugu zenu zimeimarika zaidi na kuepuka kuugua kama zamani kabla ya Kupata Chanjo?

2. Changamoto mlizozipata ndani ya muda wa Chanjo Kwa miaka hii karibia mitatu ni zipi?

3. Faida mlizopata baada ya kuchanja kiafya ni zipi kulinganisha na kabla ya kuchanja?

Karibuni 🙏
Sijapata madhara yyte sanasana trending yangu ya kupata maambukizi ya mafua imepungua before ilikuwa kila mwaka angalau mara mbili nitapata mafua ila sasa ni mara moja tu..na wala hayakai sana siku nne kwisha.
 
Back
Top Bottom