Baba Vladmir
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 413
- 725
Namna ambavyo watu hutumia madawa kujitibu ni kama vile kutumia nyundo kubwa kuua buibui.Siku hizi watu wengi wananunua madawa kutoka katika maduka ya dawa bila kuwaendea wataalamu wa afya waliobobea.Wakati mwingine madawa ya kawaida kwenye maduka ya dawa yanaweza yasiwe mazuri na hata kuwa na athari mbaya mno.
Katika ulimwengu wa tiba madawa mapya yanagundulika na kuingizwa sokoni kila siku wakati yale ya zamani huboreshwa na kusindikwa upya. Hata hivyo bado dawa kamilifu haijatengenezwa (ile ambayo itafanya kazi yake bila kuleta madhara)
Zingatia madawa ya kushughulikia shinikizo la damu.Haya ni madawa yatolewayo zaidi na wataalamu wa afya na miongoni mwa madawa yenye ufanisi. Hata hivyo yanasababisha madhara mengi makubwa.Yanaweza kuwa ni pamoja na udhaifu, uchovu, usingizi, kuumwa kichwa, mfadhaiko wa akili, kizunguzungu, kuvimbiwa, kutokwa jasho, kushindwa kumeng'enya chakula, hisia zisizotabirika, kuongea kwa shida, kuongezeka kwa kiwango cha lehemu na upungufu wa nguvu za kiume.
Watu wanaohitaji dawa hizo lazima wajaribu aina mbalimbali kabla ya kupata ile wanayoweza kuivumilia.Wazo la msingi ni kuwa hakuna dawa iliyo salama kabisa. Hata dawa za kuokoa maisha kama viua bakteria(antibiotic) huweza kuleta matatizo kama vile kichefuchefu, kutapika, kuharisha, mizio na mashambulizi ya fangasi.
KWA NINI WATU HUHARAKISHA KUTUMIA DAWA?
Wakati ambapo magonjwa mengi leo huitikia mabadiliko ya mitindo ya mitindo ya maisha(kama vile mlo bora na mazoezi ya kila siku),madaktari na wataalamu wengine tunaofundisha kanuni hizi mara nyingi tunakabiliwa na changamoto. Watu wengi sana ambao ni wagonjwa hawana uvumilivu. Wanahitaji tiba ya hapo kwa papo badala ya ufumbuzi halisi. Kwa maneno mengine, mara nyingi siku hizi watu wanahitaji kuamini kuwa kuna kidonge au maji yanayotibu tatizo walilonalo. Mara nyingi watu wanameza dawa ili kuongeza nguvu,kusaidia kupata usingizi,kutuliza maumivu,na kukinga dhidi ya maumivi yasiyofikrika,dawa nyingi zinazomezwa si kiponya tatizo bali kutuliza dalili.
KUNA MIONGOZO GANI YA KUTUMIA MADAWA KWA BUSARA?
Pata ushauri kutoka kwa mtaalamu wa afya anayestahili wakati unapodhani unahitaji dawa kwa ugonjwa fulani.Ushauri mzuri ni kutumia madawa kulingana na mahitaji maalum,yaliyotambuliwq ambayo hayawezi kushughulikiwa kwa njia zingine rahisi.Usitumie marawa yenye nguvu kama vile viua bakteria kwa ajili ya tatizo rahisi kama mafua ambayo husababishwa na kirusi.
Vilevile, kuoga maji ya vuguvugu au chai iliyotengenezwa kwa majani maalumi ya miti ni bora kuliko vidonge vya usingizi ikiwa huwezi kupata usingizi. Unapotumia dawa fulani, hakikisha unaijua jina lake,dozi,na kile hasa kinachopaswa kutibu. Elewa hatari zake na madhara,namna na wakati wa kuitumia na dalili za kuzidisha dozi.
Kama una daktari zaidi ya mmoja, hakikisha daktari mkuu anafahamu madawa yote unayoyatumia.
Kwa ufupi, kuwa makini zaidi juu ya matumizi ya madawa.Yatunze madawa hayo hadi wakati yatakapokuwa yanahitajika kwelikweli. Unaweza kuamua kujitibu matatizo yako kwa kutumia mimea asilia inayotuzunguka, majani, mizizi au magome ya baadhi ya mimea inayotuzunguka ni tiba ya magonjwa mengi tuliyonayo.
Mimea hii hutibu kwa uhakika magonjwa mengi maana hushughulika na chanzo cha tatizo lakini pia haina chemikali kali ambao zinaweza kuwa na sumu kali zinazoweza kufanya ini na figo kuwa hatarini zaidi.Mimea kama Lozera,aloevera, mchaichai, mlonge, limao, mkaratusi na aina nyingi za miti pori inaweza kutibu matatizo mengi waliyonayo watu leo kama shida ya shinikizo la damu,matatizo ya mifupa,matatizo ya uzazi, matatizo ya uchafu sehemu za siri, PID pamoja na matatizo mengine mengi yasababishwayo na mtindo wetu wa maisha ya kila siku.
Zaidi tujitahidi kurejea na kuamini katika asili huku tukila chakula bora na kuzingatia mazoezi.Tuachane na mtindo wa maisha wa kimagharibi.
TUREJEE EDENI.
Ezekiel 47:12