Bacary Superior
JF-Expert Member
- Jul 3, 2014
- 3,721
- 1,515
Lakini kiukweli vyuo vingi miundombinu yake mibovu
Mkuu mahondaw ndio signature yako?
Naogopa ban tuKwanini wadau hampendi kuambiwa ukweli na Raisi wetu juu ya kinachojiri nchini!?
Ukitekwa shauri yakoChuo cha hovyo hovyo ni chuo ambacho kinaweza kutoa mtu mwenye PhD na hajui kingereza.
Tatizo watanzania mlizoea kudanganywa .mkiambiwa ukweli povuuu.Haa ha...Huyu jamaa anaongeaga kinachokuja kichwani mwake bila kujali..!!
Bule=bure? Halafu unajiita msomi !! Kwa taarifa yako huwajui wasukuma kinachokusumbua ni wivu. Na Kwa sababu hiyo kwa miaka hii kumi mtatoa povu saana na mwisho wa siku mtanyooka tu ili unyumbu uwatoke.Mkuu huu ni usukuma.. Ndio hulka yao.. Wasamehe bule
Hama nchiSerikali ya hovyo hovyo imevisajili vyuo vya hovyo hovyo ili tuwe na elimu ya hovyo hovyo halafu inatuletea kauli za hovyo hovyo. Najisikia kiungulia!!
Ukweli upi mkuu, kiongoz mkuu anatakiwa awe na njia mbadala ya kusovu matatizo na sio kukemea na kudhalilisha watu, hata kwa mambo muhimu
yani imagine ile elimu ya zamani mzee aliyesoma mpaka darasa la 4 tu la zamani akafeli anaongea kingereza kumzidi mtu wa degree saivi, nashangaa mzee wangu (mzee ndoz) anao PhD na kingereza hakipandi, sielewi mzee wangu elimu yake ikoje ikoje manake mjukuu wake(mwanangu) nilimpeleka English medium huko mikoani(mother Kevin English Medium) iko wilaya ya same, mtoto kurudi likizo anaangalia tu CNN, BBC, al jazeera anafatilia mzozo wa North Korea na US, nashangaa mzee wangu anao PhD lakini kutwa kuangalia shilawadu, anazidiwa na mjukuu wake aliyeko class four, apongezwe sana mwalimu wa English class four huko mother Kevin.Ukitekwa shauri yako
Ndio ajabu sasa, sababu awa watoto wa English Medium saivi tu wanaongea kingereza kama niniHivi kweli unaweza kuwa PhD holder usijue kingereza????
Mkuu, na thesis yenyewe aliyoiandika imegundulika kuwa 90 percent ni copy & paste ya thesis ya jamaa fulani aliyehitimu Chuo Kikuu kimoja Ujerumani!Udsm wameweza kumpa PHD mtu asieweza kuongea kiingereza, chakushangaza alitumia lugha hiyo kujifunzia.
Udsm wameweza kumpa Phd ambayo alitakiwa asome kwa miaka 5 yeye kasoma miaka 3. Ni sawa na mtu apewe Degree ambayo alitakiwa asome miaka 3 yeye asome kwa mwaka mmoja.
Njooni tabata kimanga, we ulizia tu kwa Jafari ndoze utanikuta na nitakupeleka kwa mzee ndoze moja kwa mojatutakuja kufanya upekuzi olewako tusiikute phd kabatini tutunzie hata kifungio chake
Kamdhalilisha nani!?
Wanaoenda TCU kuhonga ili wanafunzi wanaopata mikopo wapangiwe kwenye vyuo vyao au? Tena Raisi slimezea kumwaga yote, hiyo nikuambie inamanisha anafatilia zaidi yaani uchunguzi unaendelea wa yanayotendeka.
Naamini kama chuo binafsi hakitumii njia za mikato na wanafunzi watapenda kusoma hapo basi watazichagua.
Hii ni awamu ya tano
Hapa kazi tu
Well said. TCU ni jipu.Baada ya maelezo yako inaonyesha serikali nayo ni hovyo kwani inaruhusu vijana wetu na wengine kusoma vyuo vya hovyo. Vyuo hivi vilipitishwa na serikali na baadae TCU ilipoanza ikapewa jukumu hilo. Tunakubaliana kuna tatizo kwenye mfumo huo na serikali inachangia kwenye tatizo/matatizo hayo kwa kuruhusu vyuo ulivyo viita vya hovyo kutoa elimu kwa vijana wetu. Ulianza kwa kusema "Kama hukusoma Udsm, Sua , Mzumbe, Mhimbili, IFM bas jua upo chuo cha hovyo". Haukuwa sawa mkuu. Afadhali sasa umesema vyuo vingi vya private na sio vyote na kama ni kweli ni vyuo vingi basi tatizo liko pale pale serikali inashindwa kusimamaia elimu ya juu. Economics za kuendesha chuo cha serikali na za kuendesha chuo binafsi ni tofauti kabisa na ndiyo maana serikali inatakiwa ihakikishe watanzania wanapata elimu bora na si bora elimu. Vyuo vya umma hupata mafungu ya maendeleo, OC pamoja na mishahara kutoka serikalini na wanafunzi hulipa ada pia (private na mikopo). Vyuo vya binafsi hutegemea zaidi ada na kwa hali halisi kupitia wanafunzi wanaopata mikopo ya serikali zaidi. Hivyo ni wazi kwa uchumi wetu wasipopata ada ya kutosha watshindwa kujiendesha. Je vinarubuni TCU iwape wanafunzi? Kama ni kweli huo ni ubovu wa TCU hakitakiwi kuwa chombo cha kurubuniwa hadi kuruhusu elimu ya hovyo kutolewa. Na serikali kama imeliona hilo imechukua hatua gani zidi ya TCU/Vyuo (tumeona kwa sekeseke la St Joseph lakini sio la UDOM). Ni kweli wasipopata wanafunzi wakutosha watafunga vyuo sio kwa sababu wako kibiashara zaidi lazima chuo at least kiweze kujiendesha. Sasa kwenye safari ya mamba hukosi kenge na hapo ndio serikali na TCU wanapoingia. Tamko la Raisi la juzi kuhusu udahili halisaidii nilitegemea angeweka mkazo kwenye TCU kusimamia viwango kwa vyuo vyote na visivyo faa vijirekebishe au vifungwe kabisa na sio aseme vitajifia wakati hivyo vyuo anavyopenda yeye havina capacity ya kuchukua hao waombaji wote.
Raisi ana promote vyuo vya serikali nawe hapo juu umemuunga mkono lakini sidhani kama approach yake ni sawa ya kubagua vyuo binafsi. Unasema library na madarasa vipo standard-ndugu yangu hebu tembelea baadhi ya vyuo ulivyo taja ndio vyuo utaona mengi yakustajaabisha na vyuo vimelemewa na wanafunzi. Kuna vyenye hao maprofesa unaosema kuwa ni wengi lakini bado hawaonekani darasani afadhali hata huko kusiko na doctorate nyingi lakini walimu hawakosi darasani.
Kuwa na shift mbili sio tatizo kama chuo kina mudu na hili lipo vyuo vingi kwa sababu ya demand utakuta kuna masomo ya mchana na masomo ya usiku yaani degree hiyo hiyo husomwa hivyo (angalia Nairobi na Makerere). La msingi ni uwepo wa walimu na miundo mbinu ya kutosha. Tanzania inahitaji mchango wa vyuo binafsi lakini visimamiwe ipasavyo pamoja na vya serikali na kama nchi ina uwezo wa kifedha hakuna ubaya kuwa na sera ya kusaidia vile ambavyo vinahitaji msaada au vikipatiwa msaada vitatoa huduma pana kwa watanzania.
Baada ya maelezo yako inaonyesha serikali nayo ni hovyo kwani inaruhusu vijana wetu na wengine kusoma vyuo vya hovyo. Vyuo hivi vilipitishwa na serikali na baadae TCU ilipoanza ikapewa jukumu hilo. Tunakubaliana kuna tatizo kwenye mfumo huo na serikali inachangia kwenye tatizo/matatizo hayo kwa kuruhusu vyuo ulivyo viita vya hovyo kutoa elimu kwa vijana wetu. Ulianza kwa kusema "Kama hukusoma Udsm, Sua , Mzumbe, Mhimbili, IFM bas jua upo chuo cha hovyo". Haukuwa sawa mkuu. Afadhali sasa umesema vyuo vingi vya private na sio vyote na kama ni kweli ni vyuo vingi basi tatizo liko pale pale serikali inashindwa kusimamaia elimu ya juu. Economics za kuendesha chuo cha serikali na za kuendesha chuo binafsi ni tofauti kabisa na ndiyo maana serikali inatakiwa ihakikishe watanzania wanapata elimu bora na si bora elimu. Vyuo vya umma hupata mafungu ya maendeleo, OC pamoja na mishahara kutoka serikalini na wanafunzi hulipa ada pia (private na mikopo). Vyuo vya binafsi hutegemea zaidi ada na kwa hali halisi kupitia wanafunzi wanaopata mikopo ya serikali zaidi. Hivyo ni wazi kwa uchumi wetu wasipopata ada ya kutosha watshindwa kujiendesha. Je vinarubuni TCU iwape wanafunzi? Kama ni kweli huo ni ubovu wa TCU hakitakiwi kuwa chombo cha kurubuniwa hadi kuruhusu elimu ya hovyo kutolewa. Na serikali kama imeliona hilo imechukua hatua gani zidi ya TCU/Vyuo (tumeona kwa sekeseke la St Joseph lakini sio la UDOM). Ni kweli wasipopata wanafunzi wakutosha watafunga vyuo sio kwa sababu wako kibiashara zaidi lazima chuo at least kiweze kujiendesha. Sasa kwenye safari ya mamba hukosi kenge na hapo ndio serikali na TCU wanapoingia. Tamko la Raisi la juzi kuhusu udahili halisaidii nilitegemea angeweka mkazo kwenye TCU kusimamia viwango kwa vyuo vyote na visivyo faa vijirekebishe au vifungwe kabisa na sio aseme vitajifia wakati hivyo vyuo anavyopenda yeye havina capacity ya kuchukua hao waombaji wote.
Raisi ana promote vyuo vya serikali nawe hapo juu umemuunga mkono lakini sidhani kama approach yake ni sawa ya kubagua vyuo binafsi. Unasema library na madarasa vipo standard-ndugu yangu hebu tembelea baadhi ya vyuo ulivyo taja ndio vyuo utaona mengi yakustajaabisha na vyuo vimelemewa na wanafunzi. Kuna vyenye hao maprofesa unaosema kuwa ni wengi lakini bado hawaonekani darasani afadhali hata huko kusiko na doctorate nyingi lakini walimu hawakosi darasani.
Kuwa na shift mbili sio tatizo kama chuo kina mudu na hili lipo vyuo vingi kwa sababu ya demand utakuta kuna masomo ya mchana na masomo ya usiku yaani degree hiyo hiyo husomwa hivyo (angalia Nairobi na Makerere). La msingi ni uwepo wa walimu na miundo mbinu ya kutosha. Tanzania inahitaji mchango wa vyuo binafsi lakini visimamiwe ipasavyo pamoja na vya serikali na kama nchi ina uwezo wa kifedha hakuna ubaya kuwa na sera ya kusaidia vile ambavyo vinahitaji msaada au vikipatiwa msaada vitatoa huduma pana kwa watanzania.
Serikali ya hovyo hovyo imevisajili vyuo vya hovyo hovyo ili tuwe na elimu ya hovyo hovyo halafu inatuletea kauli za hovyo hovyo. Najisikia kiungulia!!