Tafakuri: Vyuo vya hovyo hovyo ni vyuo gani?

Victor wa happy

JF-Expert Member
Apr 24, 2013
11,660
11,647
Wakuu heri ya jumatatu ya pasaka

Naomba tushirikiane kuhusu mtazamo wa Rais

Mh.Rais anaamini UDSM ndio chuo pekee kinachostahili kuitwa chuo kikuu
Labda kwasababu naye kabahatika kusoma ud

Lakini kauli zake km kiongoz wa nchi kuvidhalilisha vyuo vingine kuwa ni vibovu na havina sifa je ni sawa?

Juzi wakat ana zindua hostel alisema haina haja ya kuwa na vyuo vingine ambavyo vinadahili wanafunz ilimrad wapate mkopo serkalini tu

Kiukweli Rais hakutakiwa kuvidhalilisha vyuo,
Yeye km kiongozi wa nchi alitakiwa azihamashe na kuzitia moyo taasis za dini na mashirika yaliyoamua kuwekeza katika elimu

Rais anaonekana Bado ana mitazamo ya 80's kwamba chuo kikuu ni UDSM pekeyake

Mh Rais ajue kuwa wanafunz wanaohitimu high school kwa sasa ni wengi sana tofaut na miaka ya nyuma

Hivyo alitakiwa awashukuru watu walioamua kuwekeza katika elimu ya juu badala ya kuwakatisha tamaa

Mh. Rais anatakiwa aelewe na atambue umuhimu wa sekta binafs ndio wenye mchango mkubwa katika Maendeleo ya Taifa

Mh Rais nchi ya Gambia yenye chuo kikuu kimoja tu ndio nchi inayoshikilia mkia kwa ujinga duniani

Mh. Rais jenga mazoea ya kuwatia watu moyo wanaojitolea kwa nguvu zao kusaidia kuijenga nchi yao

Mimi ni mluther, nakumbuka miaka ya 2000's kila jumapili kulikuwa na kikapu cha sadaka kwa ajili ya ujenz wa vyuo vikuu vya Tumaini Tanzania, sasa Tanzania Kuna vyuo vikuu vya Tumaini km viwili Hivi na branch mbili

Naamini hata saut kupitia kanisa Lao la Catholic walichanga ivyo ivyo

Mh. Rais jenga utamaduni wa kuwapongeza na kuwatia moyo wananchi, Usiwe mtu wakuwakatisha tamaa

Tunajua unamamlaka makubwa, lakini jamii inayoheshimiana huishi kwa upendo na Amani zaid

Nyerere mpaka tunamuimba na kumskiliza ni kwa sabab hakuwa mtu wa kujikwezwa

Nyerere angeweza kutumia elimu yake kubwa alyoipata makerere na uingereza kutuadhibu wananchi

Sijawahi kusikia kwenye hotuba zake akizungumzia elimu yake

Napenda nchi yangu Tanzania
 
Udsm wameweza kumpa PHD mtu asieweza kuongea kiingereza, chakushangaza alitumia lugha hiyo kujifunzia.

Udsm wameweza kumpa Phd ambayo alitakiwa asome kwa miaka 5 yeye kasoma miaka 3. Ni sawa na mtu apewe Degree ambayo alitakiwa asome miaka 3 yeye asome kwa mwaka mmoja.
 
Mtu kasoma UDSM anaringa kama nini angesoma Harvard University au Oxford si tungekoma sisi tuliosoma sauti, halafu mtu mwenyewe alianzia diploma ndio akaenda bachelor na sisi tulioenda bachelor moja kwa moja mbona hatumringii, vitu vingine vinatia hasira sana
 
Nampenda Magu,ila sipendi hulka yake ya ubaguzi. Sijui kwanini aliamua kudhalilisha sekta binafsi zilizowekeza kwenye elimu. Nadhani wahitimu wengi mtaani,ndo wanamnyima raha kwa kuhoji utendaji wa serikali. Asijisahau akaanza kudharau mchango wa mashirika ya dini kwenye afya na maji.
 
Mtu kasoma UDSM anaringa kama nini angesoma Harvard University au Oxford si tungekoma sisi tuliosoma sauti, halafu mtu mwenyewe alianzia diploma ndio akaenda bachelor na sisi tulioenda bachelor moja kwa moja mbona hatumringii, vitu vingine vinatia hasira sana
Nyeyere alipiga Makerere alafu Edinburgh na hakuwahi kusikika akijivunia chuo alichosoma!
 
Mkuu mi naomba tu jibapa moja basi.
Anza na hiii kaka
92dabb12077f0f834aacb3c0a6c2e426.jpg
 
Back
Top Bottom