Tabora: Sakata la Kanisa lililojengwa kuziba barabara na kupiga muziki saa 24 kumbe ni genge la wahuni ( 5 )

King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
1,042
1,349
Kufuatia ripoti za kanisa lililojengwa katikati ya barabara na kupiga muziki mkubwa sana masaa 24 huko kata ya Kitete , mtaa wa Kariakoo Tabora imebainika kuwa kinachoitwa kanisa ni genge la wahuni vijana watupu wasiozidi miaka ishirini na tano ndio wanaoendesha uhuni huo

1. Kinachodaia kanisa hawana usajili wa kanisa kama sheria zinavyotaka
2. Hawana kibali cha ujenzi
3. Hawana kibali kuendesha kanisa
4. Hawana kibali cha afisa utamaduni kuruhusu wanachokifanya

Kwa kuwa kinaichoitwa kanisa hakina vibali husika , na Kuna vitendo vya kihuni vinavyofanywa na genge hilo lialojiita kanisa , sisi wakazi wa mtaa wa Kariakoo tunawataka afisa mipango miji, afisa mtendaji kata, afisa mtendaji mtaa na mwenyekiti wa mtaa kusimamisha shughuli zozote za kinachoitwa kanisa hilo na sheria zifutwe Kama tulivyokaa kikao na nyinyi siku ya inumaa tarehe 5/3 2021, ambapo mliahidi kuchukua hatua iwapo genge hilo la wahuni litaendelea na vurugu ikiwa I pamoja na kupiga muziki mkubwa sana huku kukiwa na shule mbili eneo hili, huku kukiwa na wagonjwa, wazee, watoto.

Afisa mipango miji kinachokufanya ushindwe kuchukua hatua ni nini? Maana Hawa watu hawana usajili wa kanisa, hawana kibali cha ujenzi, hawana kibali cha kuendesha kanisa/ ibada , sasa hebu chukua hatua Kama ulivyoahidi

Afisa mipango miji wewe mwenyewe umethibitisha madai ya wakazi wa mtaa kuwa genge hilo halina uhalali wa shughuli linazofanya kinyume na utaratibu. Hebu haki itendeke sisi hatutaki kujichukulia sheria mkononi. Mchungaji kusema amewaweka mfukoni kunaleta picha mbaya be.

IMG_20210226_124256_1.jpg
IMG_20210226_124259_0.jpg
 
Sasa huu muda unao utumia kulalamika humu jukwaani si ungeutumia kwenda kutoa haya madai yako kwa hao wahusika? Kwa nini unapatwa na kigugumizi?
Mkuu jwa wahusika tumefika sio mimi, sisi mtas mzima tumefika kwa tutakaa kikao kwa mtendaji wa kata tarehe 5 /3/2021 tutakubaliana hao wahuni wapewe muda wajirekebishe, tukawapa masharti manne, ikiwemo kutopiga muziki mkubwa sana, Sasa wamevunja makubaluano yetu na wao na tulisema wakikiuka wafungiwe shughuli zao na kuondolewa, hicho ndio ninachokikumbusua na kukisisitiza iki na viongozi wa ngazi za juu wajue, kwani mchungaji anadai afisa mipango miji, afisa mtendaji kata na mwenyekiti wa mtaa amewaweka mfukoni.
 
Tabora kwa majungu
Soma documents hapo juu hakuna majungu hiyo ni vivid evidence inajieleza wazi, kusema watu wamejenga katikati ya barabara ni majungu ? Kusema watu hawana kibali cha ujenzi ni majungu? Kusema watu hawana usajili wa kanisa ni majungu ? Kusema watu wanapiga muziki mkubwa sana wakati Kuna wagonjwa, wazee, watoto, wanafunzi , shule mbili kusumbua watu ni majungu ?
 
Nashindwa kuelewa hoja yako barua imeandikwa na Mkurugenzi alafu bado unauliza Afisa mipango miji sijui unataka afanye nini zaidi ya kuandika barua kama hivi na kufuata sheria na kanuni za matumizi bora ya ardhi?
 
Vip Bar na kumbi za disco, misikiti inayopiga kelele na kushtua watu kwenye usingizi alfajiri, nayo umeisemea?

Naona wewe hupendi tu makanisa ila siyo kwamba unapigiwa kelele!

Ukiona unahubiriwa neno la Mungu na unajickia kuumia au kuchanganyikiwa jua ndani yako kuna roho ya ibilisi!

Jitahidi kuikemea hiyo roho ya ibilisi ikutoke!
 
Soma documents hapo juu hakuna majungu hiyo ni vivid evidence inajieleza wazi , kusema watu wamejenga katikati ya barabara ni majungu ? Kusema watu hawana kibali cha ujenzi ni majungu ? Kusema watu hawana usajili wa kanisa ni majungu ? Kusema watu wanapiga muziki mkubwa sana wakati Kuna wagonjwa , wazee ,watoto ,wanafunzi , shule mbili kusumbua watu ni majungu ?
Sasa siamepewa notes kwa mujibu wa sheria?
 
Nashindwa kuelewa hoja yako barua imeandikwa na Mkurugenzi alafu bado unauliza Afisa mipango miji sijui unataka afanye nini zaidi ya kuandika barua kama hivi na kufuata sheria na kanuni za matumizi bora ya ardhi?
Utekelezaji ,yeye ndio mtekelezaji wa shughuli zote zinazohusu mipango miji na atekeleze ahadi yake? Yaani aandike tu barua halafu awaache waendelee na upuuzi ?, ahakishe na utekelezaji wake .
 
Utekelezaji ,yeye ndio mtekelezaji wa shughuli zote zinazohusu mipango miji na atekeleze ahadi yake? Yaani aandike tu barua halafu awaache waendelee na upuuzi ?, ahakishe na utekelezaji wake .
Afisa Mipango amewacopy Mwenyekiti wa mtaa na Mtendaji, kwanini usiwaulize hao kinachoendelea na wapo karibu hapo? Afisa Mipango aache kuhudumia wananchi ofisini awe ana shinda hapo kumzuia huyo mchungaji fake? chukua hatua nenda serikali ya mtaa toa taarifa atakamatwa na mgambo wa mtaa kwa kukaidi amri halali hata wewe kisheria unaruhusiwa kumkata mvunja sheria yoyote na siyo kuja kulialia hapa kama vile unachuki binafsi na Afisa mipango wa watu. Watz tujitambue kwanza sisi
 
Vip Bar na kumbi za disco, misikiti inayopiga kelele na kushtua watu kwenye usingizi alfajiri, nayo umeisemea?

Naona wewe hupendi tu makanisa ila siyo kwamba unapigiwa kelele!

Ukiona unahubiriwa neno la Mungu na unajickia kuumia au kuchanganyikiwa jua ndani yako kuna roho ya ibilisi!

Jitahidi kuikemea hiyo roho ya ibilisi ikutoke!
Kama unahitaji mada za bar na kumbi za disco anzisga uzi wako . Misikiti wanatoa adhana dakika hazizidi tano wanazima , hawa walokole uchwara wanapiga muziki mkubwa sana kuanzia asubuhi mpaka saa kumi na moja nonstop , Soma barua ya notisi uone . Kwani maudhui ya kanisa Ni kuhubiri watu wa ndani ya kanisa au kuhubiria mtaa ? Hebu tumia akili uelewe hoja , Ibilisi ni nyinyi walokole uchwara mnaopiga muziki mkubwa sana kusumbua wagonjwa wazee watoto na wanafunzi wanaojisomea .
 
Afisa Mipango amewacopy Mwenyekiti wa mtaa na Mtendaji, kwanini usiwaulize hao kinachoendelea na wapo karibu hapo? Afisa Mipango aache kuhudumia wananchi ofisini awe ana shinda hapo kumzuia huyo mchungaji fake? chukua hatua nenda serikali ya mtaa toa taarifa atakamatwa na mgambo wa mtaa kwa kukaidi amri halali hata wewe kisheria unaruhusiwa kumkata mvunja sheria yoyote na siyo kuja kulialia hapa kama vile unachuki binafsi na Afisa mipango wa watu. Watz tujitambue kwanza sisi
Sawa sisi ndio tupo huku kwenye tukio sawa , afisa mipango miji aliahidi kuchukua hatua hajachukua ndio tunamkumbusha , ndugu ukiona mada zinaandikwa hivi ujue Kuna mengi wewe uko mbali tu .
 
Back
Top Bottom