Katikati hali ya kushangaza na rushwa ilivyokithiri mamlaka za mkoa wa Tabora zadaiwa kuruhusu Kanisa kujengwa katikati ya barabara

King Kisali

JF-Expert Member
Nov 20, 2019
1,042
1,349
Katika hali ya Kushangaza sana mamlaka za mkoa wa Tabora zimeruhusu kanisa la wahuni kujengwa katikati ya barabara na kuziba barabara katika mtaa wa Kariakoo , kata ya Kitete , wilaya ya Tabora mjini , mkoa wa Tabora .

Licha ya kikundi hicho kinachojiita kanisa kutokuwa na kibali cha ujenzi kutoka manispaa, kutokuwa na ramani iliyoidhinishwa na mamlaka za kisheria , kutokuwa na kibali chochote cha muda au cha kudumu cha kuendesha kanisa , licha ya kikundi hicho kutofuata sheria na taratibu za nchi za kuendesha ibada, sauti kubwa sana inayotumika wakati wote , muda mrefu unaotumika kuendesha ibada kuanzia saa moja asubuhi hadi saa kumi na moja siku za jumapili , siku za kawaida kuanzia saa Saba hadi saa mbili usiku , na kuanza tena kuanzia saa sita usiku hadi asubuhi huku wakipiga kelele kubwa , fimbo , mbao , viti ardhini wakimuua shetani .

Pamoja na malalamiko ya muda mrefu ya wakazi wa mtaa wa Kariakoo, serikali ya mkoa, wilaya, manispaa imepuuza huku wenyewe wakitamba kwenye spika waziwazi kuwa wana hell , wamewaweka viongozi wote mfukoni. Viongozi wa mkoa, wilaya , manispaa pamoja na kujua chini ya mita hamsini kutoka hapo lilipo hilo kanisa kuna shule mbili , shule ya msingi Itetemia na Westland bado wameruhusu wahuni hao kuathiri masomo ya wanafunzi usiku na mchana , mamlaka za juu hebu ingilieni kati muokoe wanafunzi , wazee watoto , wagonjwa wanataabika sana kikundi hichoykisichokuwa hata na usajili wa kanisa.

IMG_20211209_120908_1.jpg
 
Umeandika kwa hasira sana. Kwanini uite wenzio wahuni? Acha kujitoa faham kama pamekushinda hamis Paris
 
Umeandika kwa hasira sana. Kwanini uite wenzio wahuni? Acha kujitoa faham kama pamekushinda hamis Paris
Wahuni ndio , watu wasio wahuni wanafuata sheria na taratibu na wahuni ni watu wasiofuata sheria na taratibu na ndivyo walivyo , ulitaka niwaite vipi watakatifuu ? Mbona vitendo vyao vinakataa ? Au wewe unasoma Biblia ya aina gani ? Kifupi soma 6:5 Mathayo umsikie Yesu Kristu mwenyewe anasemaje
.
 
Back
Top Bottom