A
Anonymous
Guest
Kanisa la kilokole la Bethel linalopatikana katika eneo la Nyasaka-Msumbiji, kata ya Kawekamo,wilaya ya Ilemela,mkoa wa Mwanza limekithiri kwa kupiga kelele kuzidi viwango vibakubalika kisheria.
Imekua ni kawaida sasa kufungulia mziki kwa sauti kubwa tangu saa mbili asubui mpk saa nne kasorobi usiku.siku zote za wiki na hasa kipindi hiki cha desemba hali imekua tete zaidi.Cha ajabu sasa muda mwingi wanaofungulia mziki kwa sauti kubwa ni muda ambao hawafanyi ibadi bali vijana wanadai wanafanya mazoezi.
Hali hii imekua kero kubwa kwetu wakazi wa eneo ili ukichukulia kanisa limejengwa katikati ya eneo la makazi. Eneo ili lina makanisa zaidi ya manne ila ili kanisa la Bethel ndio limekithiri kwa kelele bila kujali afya za majirani.
Sheria ya mazingira sura ya 191 kifungu cha 106 (5 na 6) kinakataza kupiga kelele kuzidi viwango vinavyoruhusiwa na ni kosa kupiga kelele kinyume na viwango vilivyoruhusiwa.Kanuni ya udhibiti wa kelele na miteremo ya mwaka 2015 zimeainisha viwango vya sauti vinavyoruhusiwa kwenye makazi ili kulinda afya ya jamii.
Pia sheria ya afya ya jamii ya mwaka 2009 na sheria ya mipango miji ya mwaka 2007 sote kwa pamoja zinatoa muongozo wa kiasi cha kelele na viwango vilivyoruhusiwa.
Kelele hizi (Nuisance)imekua kero kwa wakazi wengi wa eneo ili kitu ambacho kimeathiri mahusiano kwenye jamii,ukosefu wa utulivu,usumbufu kwa wazee na wagonjwa na hata inakua ngumu kwa watoto kujisomea kuanzia saa 2 mpk saa 3 usiku.
Wito wetu sie majirani wa kanisa la Bethel ni kuomba Baba mchungaji na viongozi wengine wa kanisa,moja ni kuendesha shughuli za ibada kwa kuzingatia matumizi ya ardhi yaliopangwa katika eneo husika,pili kudhibiti kupiga kelele kinyume na kiwango kinachokubalika kisheria ambacho ni 50dBA mchana na 35dBA usiku, tatu muda wa mazoez basi wajitahidi kupunguza sauti ya spika ili sauti iwafaa walio ndani ya kanisa,maana kuna muda unaweza kukuta kanisalina watu chini ya 15 ila sauti ni kubwa mpk mtaa wa tatu.
Pia tunaviomba vyombo vinavyohusika na usimamizi wa mazingira ikiwemo TAMISEMI (kuanzia mwenyekiti wa mtaa mpk mkurugenzi),NEMC,wizara ya afya na polisi kusimamia sheria na kufanya patrol za mara kwa mara katika maeneo haya na kuchukua hatua kama inavoainishwa katila sheria za kudhitibiti kelele na mitetemo
Licha ya Ratiba zao kuonesha ibada zinaanza jioni siku za kazi, ila kuna vijana uwa wanakuja kuwasha muziki muda wowote ule hata iwe asubuhi au mchana wa siku za kazi.
Nimeambatanisha na ratiba zao za ibada hapo chini, maana muda ambao sio wa ibada kama inavoonekana kwemye bango lao ndio muda wa kelele nyingi.