Tabora: Rais Samia atoa bilioni 4 ujenzi wa soko la kisasa Nzega Parking

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko hilo.

Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.
WhatsApp Image 2023-10-18 at 14.33.40-2.jpeg

WhatsApp Image 2023-10-18 at 14.33.40.jpeg
 
Kila apitako Rais samia watu wanakuwa na Tabasamu, furaha na matumaini makubwa sana mioyoni mwao. Hata wagonjwa wakisikia ziara ya Rais samia mahali wanajikuta wamepata ahueni ya afya zao.
 
Tunashukuru sana
Tuachane na ujinga huu wa kumshukuru na kumsifia rais pale anapotekeleza majukumu yake ya kawaida. Kwani rais anatoa hizi fedha mfukoni mwake? Hizi ni fedha za Kodi zetu.

Kwann tunamsifia? Kwani tulitarania rais akae bila kupanga, kutekeleza na kukagua mradi wowote?

Ujinga huu umenikinai wallah!
 
Tuna rais tajiri sana, sijui huu ukwasi aliupata wapi, maana anamwaga manoti kama njugu. Marais waliotangulia kabla yake walikuwa wanatumia fedha ya serikali kwenye miradi lakini yeye anatumia fedha ya mfukoni mwake. Kwa kweli watanzania tuna bahati ya kuwa na rais tajiri.
 
- Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko Hilo.

Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.
IMG-20231018-WA0016.jpg
IMG-20231018-WA0014.jpg
IMG-20231018-WA0015.jpg
 
- Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko Hilo.

Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.View attachment 2785636View attachment 2785637View attachment 2785639
Hizo hela zimetoka mfuko upi? Zilikuwa budgeted au ni utashi wa raisi?
 
Hii ni kwa sababu upeo wetu waananchi wa kupembua mambo ni finyu. Inatakiwa tujiulize, kuna maeneo mangapi Tanzania yanahitaji fedha kwa mahitaji mbalimbali? Rais ataweza kupitia kila sehemu na atoe fedha kwenye kila hitaji? Hizo fedha ni zake au amezitoa wapi? Yeye na wenzake wanatumia kiasi gani? Hizi ni siasa za made in Africa only na ndiyo maana hatuendelei.
 
- Atoa mitaji kwa wajasiriamali na Wafanyabiashara wa soko hilo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt, Samia Suluhu Hassan ametoa Bilioni 4 kwa ajili ya Ujenzi wa Soko la kisasa la Nzega Parking mkoani Tabora Ili kuwezesha wafanyabiashara kufanya shughuli zao kwenye mazingira bora.

Rais Dkt, Samia ametoa fedha hizo alipotembelea soko hilo kufuatia ombi la Mbunge wa Nzega na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kumuomba kutembelea soko Hilo.

Aidha Rais Samia amewataka Wafanyabiashara hao kupisha ujenzi na kuwaelekeza Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi kuhakikisha soko likikamilika wafanyabiashara waliopisha ujenzi ndio wapewe kipaumbele.View attachment 2785636View attachment 2785637View attachment 2785639
Hivi hizi hela zake !.
 
Back
Top Bottom