Tabora: Mwanamke afikishwa Mahakamani kwa kuwaingiza vidole sehemu za siri watoto wa majirani zake

Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Irene James mwenye miaka 36 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora kwa tuhuma za kuwafanyia unyanyasaji wa kingono watoto saba (7) wa kike wenye umri kati ya miaka Minne (4) hadi Saba (7) ambao ni watoto wa majirani zake.

Akisoma maelezo ya awali ya makosa yanayomkabili mshtakiwa huyo, Wakili upande wa Jamhuri, Gladness Senya ameieleza mahakama kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa saba ya uzalilishaji wa kingono wa hali ya juu kwa kuwaingiza vidole watoto hao sehemu zao nyeti, kinyume cha Kifungu cha 138 C (1) (a) na Kifungu kidogo cha 2(b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Majina ya watoto hao saba yamehifadhiwa.

Mbele ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, John Mdoe, Wakili huyo wa Jamhuri alidai kuwa mtuhumiwa aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti hususan nyakati za mchana tarehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye, Manispaa ya Tabora.

Mara baada ya kusikiliza maelezo hayo, Mahakama hiyo ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemnyima dhamana mshtakiwa kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotajwa tena Agosti 13.

AZAM TV
Yaani huyu mama!hivi ana watoto wa kike kweli!
Mungu atunusuru kwakweli.
 
Typical child molestation! Nchi nyingi zilizo endelea carrying kifungo cha maisha
 
Dahhh hawa wanawake wa siku hizii ni hatari wameanza michezo ya ajabu mana kam mtoto wa miaka 4 anamtia vidole basi wakubwa na yy mwenyewe sijui anafanywa nn tumuombe mungu atuepushe na haya mabo
 
Back
Top Bottom