Tabora: Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Mikaa ashtakiwa kwa kujipatia hongo ya Tzs. 300,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,281
Mnamo Februari 9, 2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Uyui, mbele ya Mh. Tausi Mongi, imefunguliwa kesi ya jinai (Criminal case No. 20240209000003354) Jamhuri dhidi ya GEORGE FICHA MANYAMA (Mwenyekiti wa Chama cha Wauza Mikaa - UWAMUKU - Tabora). Kesi imefunguliwa na waendesha Mashitaka wa TAKUKURU - Annifa Kapinga & Mwanaidi Mbuguni, ambapo mshtakiwa anakabiliwa na makosa chini ya kf cha 15 (1) (a) & (b) na (2) cha Sheria ya Kuzuia na kupambana na Rushwa Sura ya 329 marejeo ya 2022.

Mshitakiwa, Desemba 2022 kupitia simu yake ya mkononi, alishawishi na kujipatia hongo ya fedha za kitanzania shilingi laki tatu (Tzs. 300,000/= kutoka kwa mwananchi, ili kutomchukulia hatua za kisheria kwa kutokufuata matakwa ya usafirishaji wa mkaa katika ujazo unaopaswa kisheria.

Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake amekana mashitaka yote. Mshtakiwa yuko mahabusu kwani hakutimiza vigezo na masharti ya dhamana.

Shauri limepangwa kurudi kwa usikilizwaji Februari 23, 2024.
 
Nchi hii inashangaza sana kesi za mabillion hazichukuliwi hatua ila daily mahakama zinapekelewa kesi za laki tatu ujinga wa hari ya juu...
 
Dadeq, TAKUKURU wapo kazini. Siku hzi ukitaka kula hizi hongo za laki laki kiwa makin, daily watu wanapelekwa mahakamani. Ukitaka kuiba iba nyingi hadi za kumuhonga DPP.
 
Mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake amekana mashitaka yote. Mshtakiwa yuko mahabusu kwani hakutimiza vigezo na masharti ya dhamana.

Shauri limepangwa kurudi kwa usikilizwaji Februari 23, 2024.
Huyu kama sijakosea ni yule 'aliyechonga' sana siku ya kikao Cha Mwenezi Makonda kuhusu dhuluma wanazofanyiwa wauzaji wa mkaa Tabora.

Naona Sasa ni ulipizanaji wa visasi umeanza.

Maana hao Takukuru walitajwa sana kwenye 'skendo' hiyo siku hiyo.

Ngoja nifuatilie kuona kama ni yeye.
 
Drama tu kesi za msingi na zile kubwa huwezi kusikia PCCB imekamata mtu

Sikija hizi za kuku ndo wako serious yaani wanatumia bajeti ya milioni 50 kumfunga mtu aliyepokea laki tatu
 
Huyu ana bahati mbaya ila ukisikia mahali kuna rushwa ni huku bana. Ukitaka kusafirisha mkaa unaanza kurata hela kwa mwenyekiti wa kijiji, wilayani kwenye vibali, halafu funga kazi ni maliasili. Kusafirisha mzigo wa 3M uwe na 1m ya kuhonga na kuacha njiani. Barrier kama zote.

Na agisa maliasili akiwa na mood yake mbaya anaweza tu kuamua kushikilia mzigo wako au kuutaifisha. Ni biashara yenye utumwa sana japo ina faida kubwa. Maafisa maliasili unawanyenyekea kama miungu,hawa ndio wa kufunguliwa mikesi.
 
Back
Top Bottom