Tabora: Afikishwa mahakamani kwa kosa la kumlawiti Mtoto wa Miaka 11

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
207
453
Juma Binya mwenye umri wa miaka 47 mkazi wa Kata ya Malolo, Manispaa ya Tabora amepandishwa kizimbani leo Aprili 19, katika Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora akituhumiwa kumlawiti mtoto wa kiume mwenye miaka 11 akimrubuni kwa kumpatia vijizawadi vidogo vidogo kama Juisi na shilingi 200.

Binya anadaiwa kutenda kosa hilo la kulawiti kinyume na Kifungu cha 154 (1) (a) (2) kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2022 ambapo alimlawiti mtoto huyo anayesoma darasa la pili kwenye moja ya Shule ya Msingi Tabora mjini.

Wakili Dickson Swai mbele ya Hakimu mkazi, SIGWA MZIGE katika maelezo yake yaliyoandikwa kwenye hati ya mashtaka alisema mtuhumiwa amekuwa akimlawiti mtoto huyo kwa zaidi ya mara tano kati ya mwezi Februari na Machi mwaka huu.

Katika kesi hiyo mtuhumiwa atatetewa na Wakili Kanani Chombala na Mahakama imeahirisha shauri hilo hadi Mei tatu, mwaka huu itaporejeshwa kwaajili ya kusomwa hoja za awali na mtuhumiwa amepelekwa mahabusu.

Katika hatua nyingine Mahakamaya Hakimu mkazi Mfawidhi Wilaya ya Lindi imemuhukumu Said Mohammed mwenye umri wa miaka 49 mkazi wa Chikonji kutumikia kifungo cha miaka 30 Jela,

viboko sita pamoja na kulipa fidia ya shilingi 500,000 baada ya kupatikana na kosa la kumbaka Bibi mwenye umri wa miaka 62 tukio ambalo alilifanya majira ya saa 11 alfajiri wakati Bibi huyo akielekea shambani.

Hukumu hiyo imetolewa na hakimu mkazi mfawidhi Maria Batulaine huku akiweka wazi nafasi ya kukata rufaa.

#kulawiti #mtoto #mshtakiwa #mahakama #tabora #sheria
 
Yaani nmekuja haraka nikajua ni mwalimu ndie kalawiti...
Walimu wamevurugwa sana kwenye swala la kulawiti
 
Back
Top Bottom