BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Shauri la Uhujumu Uchumi namba 2015/2024- Jamhuri dhidi ya Bw. BONIFACE YOHANA NKAKATISI- Katibu Mkuu Taifa wa CHAMA CHA WAFANYAKAZI WA VIWANDA, BIASHARA-TAASISI ZA FEDHA, HUDUMA NA USHAURI (TUICO) imefunguliwa leo Januari 31, 2024 mbele ya Mh. Bittony Mwakisu (SRM) katika Mahakama ya wilaya Ilala.
Mshtakiwa ameshtakiwa kwa kosa la Kutumia madaraka yake vibaya kinyume na kifungu cha 31 na kosa la Ubadhirifu na Ufujaji wa fedha kiasi cha Tshs.238,545, 044/= kinyume na kifungu cha 28(2) vyote vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 329 ikisomwa pamoja na Sheria ya Uhujumu Uchumi,Sura ya 200,R.E 2022.
Mshtakiwa amekana makosa yote na kupelekwa mahabusu baada ya kutokukidhi masharti ya dhamana.
Kesi imeahirishwa hadi tarehe 05.02.2024 kwa ajili ya kutajwa.