Tabora: Mwanamke afikishwa Mahakamani kwa kuwaingiza vidole sehemu za siri watoto wa majirani zake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Irene James mwenye miaka 36 amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu mkazi Tabora kwa tuhuma za kuwafanyia unyanyasaji wa kingono watoto saba (7) wa kike wenye umri kati ya miaka Minne (4) hadi Saba (7) ambao ni watoto wa majirani zake.

Akisoma maelezo ya awali ya makosa yanayomkabili mshtakiwa huyo, Wakili upande wa Jamhuri, Gladness Senya ameieleza mahakama kwamba mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa saba ya uzalilishaji wa kingono wa hali ya juu kwa kuwaingiza vidole watoto hao sehemu zao nyeti, kinyume cha Kifungu cha 138 C (1) (a) na Kifungu kidogo cha 2(b) cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Majina ya watoto hao saba yamehifadhiwa.

Mbele ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, John Mdoe, Wakili huyo wa Jamhuri alidai kuwa mtuhumiwa aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti hususan nyakati za mchana tarehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye, Manispaa ya Tabora.

Mara baada ya kusikiliza maelezo hayo, Mahakama hiyo ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemnyima dhamana mshtakiwa kwa madai ya usalama wake na kwamba amepelekwa mahabusu mpaka pale kesi hiyo itakapotajwa tena Agosti 13.

AZAM TV
 
Duh!!!!,Dunia simama nishuke mie.Sasa jamani ukisikia mtu ameawa ana wananchi wenye hasira kali ndo km hivi.Sasa kweli Malaika hao kwanini awanyanyase hivyo?.Anakuwa anatafuta nini?.
 
Mwanamke mmoja Irene James (36) amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Tabora akituhumiwa kuwafanyia unyanyasaji wa kingono kwa kuwaingizia vidole sehemu zao za siri watoto saba wa kike wenye umri kati ya miaka 4 hadi 7 ambao ni watoto wa majirani zake.

Imeelezwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa huyo aliwatendea makosa hayo watoto hao saba wa majirani zake kwa nyakati tofauti majira ya mchana terehe zisizojulikana kati ya mwezi Januari hadi Julai mwaka huu huko katika Kata ya Kanyenye manispaa ya Tabora.

AZAM TV
Huyo mwanamke lazima ana matatizo ya kisaikolojia kutokana na kutendewa hivyo hivyo akiwa mdogo.
 
Sura ya kazi
image.jpeg
 

Attachments

  • image.jpeg
    image.jpeg
    309.5 KB · Views: 1
Duniani Kuna mambo. Nilishaona mtu kwenye bar Kigoma anaingiza vidole sehemu za Siri za mwanamke Kisha ananusa vidole vyake na kutabasamu sana
 
Back
Top Bottom