Kabla ya bei ya mafuta kupanda mafuta yaliadimika sasa hakuna tena tatizo la mafuta

MKWEAMINAZI

JF-Expert Member
May 28, 2023
930
1,299
Taifa gumu sana hili. Inaonekana kuna mawasiliano ya ukaribu sana kati ya wamiliki wa vituo vya mafuta na viongozi wa EWURA.

Kabla ya bei ya mafuta haijapanda kulikuwa na uhaba mkubwa wa mafuta nchi nzima, lakini baada ya bei kupanda hakuna uhaba kabisa wa mafuta. Hali hiyo inaonyesha kuwa wamiliki wa vituo vya mafuta walikuwa na taarifa zote za upandishwaji wa bei ya mafuta toka EWURA ndio maana wakayaficha mafuta.

Kama ingekuwa hawajui lolote wasingeficha mafuta kusuburi bei ipande.
 
... that means that was sabotage! Ule ujinga wa kuficha bidhaa au huduma kusubiria bei mpya au mishahara ipande umerudi tena kwa kasi na hakuna hata anayeonekana kukemea japo kwa kauli tu!
 
TAIFA gumu sana hili.Inaonekana Kuna Mawasiliano ya ukaribu sana kati ya WAMILIKI wa VITUO vya MAFUTA na VIONGOZI wa EWURA.
Kabla ya Bei ya MAFUTA haijapanda kulikuwa na UHABA MKUBWA wa MAFUTA NCHI NZIMA,lakini baada ya BEI KUPANDA hakuna UHABA KABISA wa MAFUTA.hali hiyo inaonyesha kuwa WAMILIKI wa VITUO vya MAFUTA walikuwa na TAARIFA zote za UPANDISHAJI wa BEI ya MAFUTA toka EWURA ndio maana WAKAYAFICHA MAFUTA.
Kama ingekuwa hawajui lolote WASINGEFICHA Mafuta kusuburi BEI IPANDE.
Tanzania yetu 🇹🇿 🎶🎶
 
Wanaomiliki vituo vya mafuta ndo hao hao. Kwa akili yangu mbovu, Sheri yangu pendwa, ya muda mrefu nakunywa pale mafuta, niliwahama tangu j tano. Sababu kuu ni, na wao kuyabana mafuta wakisubiri niwapandishie hela kwa mtaji wao ule ule wa mwanzo.
 
JPM alikua anawajulia hao watu,japo walimkomesha naye kipindi cha sukari.Acha wapete tu.
 
Hata reli,itachukua muda sana kukamilika,wamiliki wa mabasi,na vyombo vingine vya usàfiri lazima watakua na mkono wa uhujumu wa reli tarajali.
 
Ujafanya survey vizuri kuna baadhi ya wilaya za morogoro Hadi mda huu wanaangaika mafuta ya petrol akuna
 
Back
Top Bottom