Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Junius mtani wangu (kama Mzenji nina imani hiyo) pamoja na wachangiaji wengine,

Nipeni muda kidogo na nitakuja na maoni yangu kwa ujumla juu ya Sikonge.

Malila, Wilaya ya Sikonge ina ardhi nyingi na kubwa saaana. Angalia kwenye Google Earth maeneo kama Pangale, Kasisi, Tutuo kwenda hadi Mole, vuka Sikonge na nenda chini kama waenda Mbeya na fika eneo jingine walilo-ZOOM yaani waweza kuona kwa karibu hadi nyumba na utaona vijiji kama vilivyo kama km.40 kutoka Sikonge. Huko utaona maeneo mengi na makubwa saaana. Yaani hata ukitaka km.10 kwa 10 bado utazipata bila wasiwasi na hakuna wa kukuuliza.

Tatizo la Sikonge na Tabora kwa ujumla ni USAFIRI na wakati wa Masika, maeneo hayo hadi kufika huko Itunda ambako Kikwete amekuwa Rais wa kwanza kufika, huwa hayafikiki. Hata Kikwete mwenyewe gari lilikwama na ikabidi watume Helcopiter imfikishe huko. Wakati wa Masika huwa ndiyo mabasi kama SHAKIRA linafika.

Wasomi kama Balozi Chokara, ndiyo wanatoka maeneo hayo. Pia jamaa wengine wengi tu humu wanatoka maeneo hayo kwani hivyo vijiji vilivyoanzishwa wakati huo miaka ya 70, kama Usunga nk chini ya Uhamishaji watu wa Mzee Luswetula (asante Keil kwa kunikumbusha huyu Mzee) ulifanya mkusanyiko mkubwa sana wa watu na ushindani shuleni ukawa mkubwa. Kijiji hiki kilikuwa na sifa ya kupasisha wanafunzi wengi karibu kila mwaka na mara nyingi wakiizidi hata Sikonge yenyewe pamoja na kuwa na shule mbili za Msingi.

Tatizo la Sikonge, ni tatizo common kwa Tabora nzima.

MALILA: Angalia pia sehemu inaitwa Tumbi, ni kama unaenda Urambo na karibu sana na Tabora Mjini, na baada ya hapo nenda Kaskazini hadi utaiona kambi ya JKT ya Msange. Hii kambi peke yake kuna misitu mikubwa sana ambayo zamani yalikuwa mashamba ya katani ya Msungu. Huyu Mzungu alishindwa kutamka Msange na akawa anasema Masange. Ndiyo maana zamani kambi pia ilikuwa ikiitwa Masange na baadaye ndiyo ikabadilishwa na kuitwa Msange (Mkute). Kutoka hapo unaenda hadi huko kijiji cha Mbola, ni msitu mkubwa sana. Hahaaaaa, kijiji cha Mbola kuna mama mmoja ambaye anaishi kwa kupewa Msaada na Mwanamziki Maarufu na Producer aitwaye John Legends. Ukiingia kwenye ukurasa wake, utaona picha zake akiwa Mbola na ukisikia katua Tz basi ujuwe kaenda kumtembelea mama yake wa Mbola. Vuka Msange nenda hadi maeneo lilipo bwawa la Igombe kama sikosei, na vuka Igombe, huko kote ni msitu mzito sana wa Miyombo na safi sana kwa kufuga asali..........

Ntaandika zaidi baadaye kama nilivyoahidi na nafikiri KEIL na Mkuu Kichuguu watasaidia na wao maoni yao. Nitajadili zaidi sababu ambazo naona zimesababisha hali iwe hivi na nini kinaweza kufanyika maana si kulaumu tu ila pia kujaribu kutoa maelezo nini kifanyike.

Mkuu Sikonge umenikumbusha Mbali sana, mimi ni mingoni mwa wanafunzi tuliofauru toka shule ya USUNGA - miaka hiyo. Mwaka wetu tulifauru sita - Mimi Moshi Tech, Mwingine Boys, mwingine Kigoma Sec, Kilosa na Bihawana.

Its true - Tabora is more than how people think about...
 
Nyie vijana bwana, msipe simanzi bure........

Mwavezya nakumbula kukaya maana nsiku nyingi sana. Namwizukila Mzivila na Marehemu Manywele wa ku-Chabutwa.

Hii naona ni familia ya Mwana Lwelwe wa Migavo / Maswezi ila yeye wa Igalula.

Elnino, unamfahamu mshikaji mmoja akiitwa Charles Sepetu? Kama sikosei familia yao wanafahamika kwa jina la Ng'ombe na baba yao alikuwa na mroli miaka ya 70.
 
Attachments

doh,
naona tatizo ni viwanda vya uzalishaji hakuna,na vilivyokuwepo vimefungwa kama kiwanda cha nyuzi na hata kile cha tumbaku.
enzi hizo hivi vilisaidia kuinua uchumi wa tabora sio kama sasa.kwa sasa hivi wanategemea tu kilimo hicho cha tumbaku na inauzwa mikoa jirani wakati hapo kiwanda kilikuwepo,na zinanunuliwa kwa bei ya chini.
wengi wa wazawa wa tabora hawajapata elimu ya kutosha,japo mashule yapo mengi ya kutosha.wengi ni wageni wanasoma na kuondoka.anyway wafufue viwanda kwanza wataamka na kusimama taratibu.
kitu kingine,ushauri kwa wawekezaji,tabora ina eneo la ardhi kuubwa sana ambayo ipo tupu na inahitaji kuendelezwa.mfano kule wangepeleka viwanda kama vitatu tu vingetosha sana,kama kiwanda cha vinywaji kama juis na maji,pia viwanda vya vyakula as long mpunga na mahindi ni zao linalolimwa mkoani hapo.
si mbaya pia baadhi ya ofisi za serikali zikahamishia huko makao makuu.ni matumaini yangu wafanyakazi wake wengi watakaokua huko kufanya kazi watapaboresha zaidi.
Samwel Sitta alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo Cha Uwekezaji (TIC) kwa muda mrefu. Aliufanyia nini mkoa wake kiuwekezaji? Au Ndizo speed na standards alizotamba nazo? Kuna msemo: Mzigo mzito mtwishe Mnyamwezi. Tangu enzi za kina Tip Tip kazi yao ni kubeba mizigo ya wengine si ya kwao wenyewe. Tangu 1940s kuna shule kama Tabora Boys, Mirambo, Tabora Girls, Kazima, nk. Hizo wamesoma watu wa kuja tu? Kama ni hivyo alaumiwe nani?
 
mkuu Sikonge i salute you!!

Yaani unaijua vizuri tabora mimi nimewahi kufika urambo miaka ya 98 lakini hivi juzi tu miezi kama miwli iliyopita nilifika bukene kwa mara ya kwanza kama baaada ya miaka kumi nilivyopaacha ni vilevile nilivyopakuata haki yanani hata maji bomba hakuna kimji kizima umeme kwao ndoto wafanyabiashara wale wa kiburushi wamehamia nzega yaani kuna sehemu nymba zimedondoka au kushikwa na miti any time chali hapo ndo city center daa!! Sijui nibadili kabila kama walivyosema wengine?

Kahawa kashata vitumbua siku nzima mtu toka unapata akili; unamkuta mzee mpaka anazeeka anauza tumbaku ya kuvuta karidhika nyumba anayokaa mbavu za mbwa na ndiyo hali halisi ya watu wetu wa huko. Ni lazima wabadilishwe mtazamo na lazima wanaTabora wakutane wao wenyewe wajadili kwa kina.

Tuna mheshimiwa Sitta, Kapuya huyo Kaboyonga sasa Aden mwenywe anajulikana kama mtoto wa mjini Mzee said el maamry na wengineo wengi waliyokaa katika system. Lazima wanatabora bila kujali wilaya wanayotoka wajiulize nini faida ya kuwa na viongozi wote waliopata kushika madaraka na wameifanyia nini Tabora au ndo kuishia Dar?! Na hii ndo stahili yao kubwa. Sasa nini faida ya kutamba mbele za watu mimi mnyamwezi au msukuma? Mimi huwa wakati mwingine naona kichefuchefu twaabiwa wanyamwezi kazi yao kustarehe tu.

Suala la kuuwa na viwanda ni muhimu angalia hivi majuzi tu (98 elfu mbili kama sikosei) eti tumbaku inavunwa Tabora kimekuja kujengwa kiwanda kipya kilichokuwa kinaitwa Dimon pale Morogoro kingulowila! Tena hili ni kosa, kwa mara nyingine wenye Tabora waliona na wakanyamza kimya.

Jamani inaumaa yaani mzee Sikonge nasubiri hiyo mada yako kwa hamu kuna umuhimu wa kuweka msukumo kuona nini kinafanyika ni hatari mzee daa tuna vyanzo vingi vya uchumi na uwekezaji
 
Last edited by a moderator:
Unahitaji mkakati wa dhai wa kubadilisha muonekano wa Tabora. Kwa mara ya kwanza nilipofika sikuamini kuona yale niliyoyaona. Nilitegemea mambo makubwa zaidi. Wakati ule tunasoma nilikuwa nasikia sifa za shule kama Uyui, Tabora Boys, Kazima etc. Waliosoma waanze kufikiria sasa kutoa misaada ya hali na mali kuioresha Tabora na historia yake. Wakina Sita na Rage wao ni wawakilishi tu
 
jamani sijui wenzangu kama mmepata kung'amua kitu hiki mkoa wa Tabora ni kama vile umekufa kwa jinsi nionavyo mimi licha ya wakazi wake kuwa na chakula pengine cha kutosha lakini miaka nenda rudi nikipita hapo sioni mabadiliko utafikiri vile hakuna wazawa waliokwenda shule mpaka leo mbavu za mbwa ziko katika mji tatizo liko wapi?
-kwa wazawa wenyewe?
-serikali?
kwa kuwa kama ni viongozi waliosoma na kuwepo katika sytem hii ya serikali wapo tangu kitambo mbona kunadorola yaani huwa napata maswali mengi kichwani?
hebu nisaidiane hasa ninyi wazawa wa tabora na wenye kuufahamu vizuri unastahili kuwa kama ilivyo? ukizingatia kuwa ni mkoa wa kihistoria katika harakati za uhuru wa nchi hii.

Inategemea unapita Tabora ya wapi, kama unapitia ile Tabora ya mji mkuu basi huwezi kuona mabadiliko sana kwa vile pale kuna majumba mengi ya msajiri na ya tasisi mbalimbali, inabidi upitie pembezoni mwa mji ndipo uone tulivyofanya vitu vyetu huko.
 
Junius mtani wangu (kama Mzenji nina imani hiyo) pamoja na wachangiaji wengine,

Nipeni muda kidogo na nitakuja na maoni yangu kwa ujumla juu ya Sikonge.

Malila, Wilaya ya Sikonge ina ardhi nyingi na kubwa saaana. Angalia kwenye Google Earth maeneo kama Pangale, Kasisi, Tutuo kwenda hadi Mole, vuka Sikonge na nenda chini kama waenda Mbeya na fika eneo jingine walilo-ZOOM yaani waweza kuona kwa karibu hadi nyumba na utaona vijiji kama vilivyo kama km.40 kutoka Sikonge. Huko utaona maeneo mengi na makubwa saaana. Yaani hata ukitaka km.10 kwa 10 bado utazipata bila wasiwasi na hakuna wa kukuuliza.

Tatizo la Sikonge na Tabora kwa ujumla ni USAFIRI na wakati wa Masika, maeneo hayo hadi kufika huko Itunda ambako Kikwete amekuwa Rais wa kwanza kufika, huwa hayafikiki. Hata Kikwete mwenyewe gari lilikwama na ikabidi watume Helcopiter imfikishe huko. Wakati wa Masika huwa ndiyo mabasi kama SHAKIRA linafika.

Wasomi kama Balozi Chokara, ndiyo wanatoka maeneo hayo. Pia jamaa wengine wengi tu humu wanatoka maeneo hayo kwani hivyo vijiji vilivyoanzishwa wakati huo miaka ya 70, kama Usunga nk chini ya Uhamishaji watu wa Mzee Luswetula (asante Keil kwa kunikumbusha huyu Mzee) ulifanya mkusanyiko mkubwa sana wa watu na ushindani shuleni ukawa mkubwa. Kijiji hiki kilikuwa na sifa ya kupasisha wanafunzi wengi karibu kila mwaka na mara nyingi wakiizidi hata Sikonge yenyewe pamoja na kuwa na shule mbili za Msingi.

Tatizo la Sikonge, ni tatizo common kwa Tabora nzima.

MALILA: Angalia pia sehemu inaitwa Tumbi, ni kama unaenda Urambo na karibu sana na Tabora Mjini, na baada ya hapo nenda Kaskazini hadi utaiona kambi ya JKT ya Msange. Hii kambi peke yake kuna misitu mikubwa sana ambayo zamani yalikuwa mashamba ya katani ya Mzungu. Huyu Mzungu alishindwa kutamka Msange na akawa anasema Masange. Ndiyo maana zamani kambi pia ilikuwa ikiitwa Masange na baadaye ndiyo ikabadilishwa na kuitwa Msange (Mkute). Kutoka hapo unaenda hadi huko kijiji cha Mbola, ni msitu mkubwa sana. Hahaaaaa, kijiji cha Mbola kuna mama mmoja ambaye anaishi kwa kupewa Msaada na Mwanamziki Maarufu na Producer aitwaye John Legends. Ukiingia kwenye ukurasa wake, utaona picha zake akiwa Mbola na ukisikia katua Tz basi ujuwe kaenda kumtembelea mama yake wa Mbola. Vuka Msange nenda hadi maeneo lilipo bwawa la Igombe kama sikosei, na vuka Igombe, huko kote ni msitu mzito sana wa Miyombo na safi sana kwa kufuga asali..........

Ntaandika zaidi baadaye kama nilivyoahidi na nafikiri KEIL na Mkuu Kichuguu watasaidia na wao maoni yao. Nitajadili zaidi sababu ambazo naona zimesababisha hali iwe hivi na nini kinaweza kufanyika maana si kulaumu tu ila pia kujaribu kutoa maelezo nini kifanyike.

Sikonge inaonekana uko juu sana kuhusu mkoa wa Tabora, unayajua Magandu?, ni katika vitu vilivyonishinda kula. Vipi pia uliwahi sikia story ya mkulima tumbaku bora wa kijiji kinachoitwa ufumila akiitwa Juma Magono?. JKT masange nimeshawahi fika kama sikosei ukifika kijiji cha kalunde unaingia kushoto, tuwaliwahi mpeleka dada yetu mmoja enzi zile za mujibu wa sheria. Kuna sehemu kama izimbili kuna mlima ambao ni solid rock tu. Igombe ilikuwa tukienda Picnic kuna samaki fulani nawakumbuka walikuwa wakiitwa ndomondomo wa bwawa la igombe. Kuna maeneo kama itetemia kule kwenye jiwe linalolia kama ngoma na alama za nyayo kwenye solid rock.

Ukija kwa vitongoji vya mjini ninayoikumbuka ni Gongoni, isevya, Cheyo, National housing, Ipuli, Ng'ambo, Kanyenye, Makokolo kule kwa watani wetu wa Milambo sec, Chemchem, Bachu, Tambukaleli, Milambo barracks, Itetemia, Mwanza road. Duh long time last time kutembelea Tabora ni 2000.

Duh! ninakumbuka mbali sana kuhusu Tabora, hasa enzi zile kulikuwa na Kombe la Mgulunde lilikuwa linashinaniwa na shule za sekondari na vyuo vya Tabora.
 
Wanyanyembe , na wakonongo kama ndugu yangu SIKONGE, nafurahi kwa michango yenu mingi kuhusu TB au Tabora, naona wengie hawaijui Tabora hata wanadiriki kusema watu wa Tabora hawajasoma. Hii inatokana na kutokuwajua kwa undani wazawa wa Tabora ni akina nani? anyway nitarudi baadae ngoja niishie hapa.

Mluga
 
sijawahi kufika Tabora,ila vipi enzi zile za marehemu Lawrence Gama,je maendeleo ya kicuhumi yalkikuwaje na miundo mbinu?au yeye anasifika kuipandisha milambo toka mchangani daraja la 3 enzi hizo mpaka ligi daraja la kwanza(ligi kuu siku hizi)na ule uwanja wa ally hassan mwinyi,achilia mbali uwanjawa vita,na kuna timu mpaka leo sijui ipo inaitwa polisi hao hawajahi kucheza ligi kuu labda kama walibadilisha jina,samahanini lakini mimi naingia sana kwenye michezo,na ndio najua moja ya mafanikio ya marehemu Gama mikoa ya Ruvuma na Tabora yalikuwa ktk soka kazisaidia majiwater na milambo kuwa tishio ligi kuu vs simba na yanga,wapi mikidadi j4 bubu,jobe ayubu kwasakwasa,quresh ufunguo,dadi phares wanyanyembe!
 
jamani sijui wenzangu kama mmepata kung'amua kitu hiki mkoa wa Tabora ni kama vile umekufa kwa jinsi nionavyo mimi licha ya wakazi wake kuwa na chakula pengine cha kutosha lakini miaka nenda rudi nikipita hapo sioni mabadiliko utafikiri vile hakuna wazawa waliokwenda shule mpaka leo mbavu za mbwa ziko katika mji tatizo liko wapi?
-kwa wazawa wenyewe?
-serikali?
kwa kuwa kama ni viongozi waliosoma na kuwepo katika sytem hii ya serikali wapo tangu kitambo mbona kunadorola yaani huwa napata maswali mengi kichwani?
hebu nisaidiane hasa ninyi wazawa wa tabora na wenye kuufahamu vizuri unastahili kuwa kama ilivyo? ukizingatia kuwa ni mkoa wa kihistoria katika harakati za uhuru wa nchi hii.

I miss Tabora
 
Wajenge kwanza barabara ya lami kuunganisha nzega na tabora mjini hapo ndio wataanza kufungua milango ya mji kuleta maendeleo..........mengineyo yatafuata. Ila kiukweli mji unasikitisha, Tabora mjini pale maji ya bomba yanapopatikana rangi yake tu huwezi hata kufua shati lako jeupe ulipendalo.
 
Tabora tuna matatizo mengi lakini si ya kujitakia ni kwamba tumesahaulika mno, miundo mbinu ya maji safi inaanzia mto Igombe kama unaenda sehemu inaitwa Itaga. hiki chanzo ni cha zamaini sana miaka ya 70 so mitambo imechakaa.

Ningependa Miundombinu ya maji na barabara ipewe priority na viongozi wetu. kwa mfano
Barabara toka Nzega hadi Tabora ingefungua milango ya biashara - Mwanza - Nzega - Tabara.

Barabara ya Dodoma - Manyoni - Tabora - Ipole - Mpanda - Kigoma. Barabara hii ilishafanyiwa upembuzi yakinifu mwaka 1994 na Kampuni ya PHOTOMAP international ya Kenya. Makaratasi yapo kapuni wizara ya ardhi. Barabara hii ingefungua milango kati yetu na watu wa Mpanda hadi Kigoma hence Dar -Tabora - Kigoma

Barabara ya kutoka Tabora - Sikonge - Ipole - Mbeya (Alikokwamia mgombea Urais wa CCM) . hii ingefungua milango na wenzetu wa mbeya kama mnavyojua mbeya ni kati ya mikoa inayopiga hatua ki maendeleo.

Kilimo.
Wananchi wa Tabora wanategemea kilimo cha Tumbaku kama zao lao la biashara, lakini kilimo hiki hakijatiliwa mkazo wakulima wanajaribu kwa uwezo wao lakini wanakosa support toka serikalini. Matokeo yake kilimo kimedorora vibaya sana kwa miaka ya hivi karibuni.

Ni kweli mkoa huu umesahaulika ingawa umetoa wasomi wengi sana hasa kutoka katika shule za wavulana na wasichana TABORA pia Milambo Sec.
 
sijawahi kufika Tabora,ila vipi enzi zile za marehemu Lawrence Gama,je maendeleo ya kicuhumi yalkikuwaje na miundo mbinu?au yeye anasifika kuipandisha milambo toka mchangani daraja la 3 enzi hizo mpaka ligi daraja la kwanza(ligi kuu siku hizi)na ule uwanja wa ally hassan mwinyi,achilia mbali uwanjawa vita,na kuna timu mpaka leo sijui ipo inaitwa polisi hao hawajahi kucheza ligi kuu labda kama walibadilisha jina,samahanini lakini mimi naingia sana kwenye michezo,na ndio najua moja ya mafanikio ya marehemu Gama mikoa ya Ruvuma na Tabora yalikuwa ktk soka kazisaidia majiwater na milambo kuwa tishio ligi kuu vs simba na yanga,wapi mikidadi j4 bubu,jobe ayubu kwasakwasa,quresh ufunguo,dadi phares wanyanyembe!

Mkubwa, ule uwanja wa Ali hassan mwinyi kweli hakuna mwananchi wa Tabora ambaye hakushiriki - nakumbuka hadi Vijijini michango ilipita mwenye kuku, bata, mbuzi ili mradi uwanja uishe. Wenzetu waliokuwa Tabora mjini wasioweza kutoa pesa basi wajijitolea kufanya kazi ya ujenzi - kufyatua matofali, kubeba mchanga, kuchanganya simenti n.k

Kinachosikitisha uwanja sasa hvi ni pango la wezi, umekatika vipande vipande -usimamizi mbovu nguvu ya wananchi imepotea bure.

Ile timu yetu iliyokuwa inawika ya Mashujaa wa Unyanyembe yaani Milambo, inasuasua - nakumbuka enzi hizo kuna kijana alikuwa anaitwa Quresh Ufunguo na yule number Tano ( Wanyawezi wanapenda kuita Dala ) Yule alikuwa Bubu Jina la uchezaji alipachikwa "Kwasakwasa" Ilikuwa moto wa kuotea mbali.

Wakuu sasa nakumbuka home sana...
 
Yeah Wachangiaji.

Wee Hosftede, mie siyo Mkonongo bana. Wala Magando ni Wakonongo wanaotoka Kitunda.

Watu wa kitunda ni kati ya Mnyamwezi na Mfipa / Mnyakyusa. Wanavyoongea kwa mfano neno Hivyo hivyo, Wanyamwezi wa Sikonge tunasema "Vyenivyo", Wasukuma wanasema "Shenisho" na Wakonongo kwa kukaa karibu na Wanyakyusa wanasema "Fyenifyo.....".

Magando, hahahaa kwa wasiofahamu ni kuwa kuna mti unaitwa Mgando na huwa kuna hawa Catapiller wanapenda sana kula majani yake na Wakonongo (baadhi ya Wanyamwezi pia) huwa wanaenda na kuukata mti (Hapa wanafanya makosa) au huwa wanapanda na kutikisa matawi na wale Caterpiller huwa wanaanguka na wanawachukua na kuwakaanga. Kama sikosei watakuwa na radha kama Senene au Kumbikumbi...

Niliporudi kutoka mjini (niliishi nikiwa mtoto) niliambiwa kuwa watu wanakula. Bahati nzuri kwetu tulikuwa hatuli maana ingelikuwa kasheshe kunilazimisha kula. Ila nilisoma na kusikia makala moja kwenye CCN juu ya kisa kwamba Wazungu wanaagiza kwa wingi sana haya Magando. Wengine wameyapenda na wengine wameyachukia. Ila yana soko sana.

Caterpillar12.jpg

Nina mpango wa kuja kuwa napita vijijini Sikonge nzima na kuwaambia kuwa siku kama wameshuka senene, basi wawakamate wengi na wanipigie simu na mie siku hiyohiyo ninaingia na kuwabeba. Ntawakaanga na kuwatunza vizuri na baadaye kuja JF, Tanzanet, Michuzi Blog nk nk na kuwauza. Wahaya na Waganda wanaoishi nje, watanunua hata kwa dola 200 kilo, hihihiiiii ..... Elnino, Kichuguu na Keil msinicopy.
Kwa Wanyamwezi ntawatumia (Matini) mchwa wa kwenye Kichuguu. Pia ntakuuzieni ule uyoga wa Bunsolele, teteteteeeeee 🙂
Na kwa makabila yoote, ntauza pia kumbikumbi. Mnaonaje hii biashara? Kila kitu kitakuwa kwenye EBAY, hahahahaaaaa na malipo kwa PAYPAL na Mkuu wangu Mwakalinga atakusanya pesa yangu na kunitumia........

Jamani, makala yangu bado naandika.
 
Naskia eti ukianzisha kitu chochote cha maendeleo kabla hakijafika kati unapigwa kipapai......... Naskia tu....
 
Junius mtani wangu (kama Mzenji nina imani hiyo) pamoja na wachangiaji wengine,

Nipeni muda kidogo na nitakuja na maoni yangu kwa ujumla juu ya Sikonge.

Malila, Wilaya ya Sikonge ina ardhi nyingi na kubwa saaana. Angalia kwenye Google Earth maeneo kama Pangale, Kasisi, Tutuo kwenda hadi Mole, vuka Sikonge na nenda chini kama waenda Mbeya na fika eneo jingine walilo-ZOOM yaani waweza kuona kwa karibu hadi nyumba na utaona vijiji kama vilivyo kama km.40 kutoka Sikonge. Huko utaona maeneo mengi na makubwa saaana. Yaani hata ukitaka km.10 kwa 10 bado utazipata bila wasiwasi na hakuna wa kukuuliza.

Tatizo la Sikonge na Tabora kwa ujumla ni USAFIRI na wakati wa Masika, maeneo hayo hadi kufika huko Itunda ambako Kikwete amekuwa Rais wa kwanza kufika, huwa hayafikiki. Hata Kikwete mwenyewe gari lilikwama na ikabidi watume Helcopiter imfikishe huko. Wakati wa Masika huwa ndiyo mabasi kama SHAKIRA linafika.

Wasomi kama Balozi Chokara, ndiyo wanatoka maeneo hayo. Pia jamaa wengine wengi tu humu wanatoka maeneo hayo kwani hivyo vijiji vilivyoanzishwa wakati huo miaka ya 70, kama Usunga nk chini ya Uhamishaji watu wa Mzee Luswetula (asante Keil kwa kunikumbusha huyu Mzee) ulifanya mkusanyiko mkubwa sana wa watu na ushindani shuleni ukawa mkubwa. Kijiji hiki kilikuwa na sifa ya kupasisha wanafunzi wengi karibu kila mwaka na mara nyingi wakiizidi hata Sikonge yenyewe pamoja na kuwa na shule mbili za Msingi.

Tatizo la Sikonge, ni tatizo common kwa Tabora nzima.

MALILA: Angalia pia sehemu inaitwa Tumbi, ni kama unaenda Urambo na karibu sana na Tabora Mjini, na baada ya hapo nenda Kaskazini hadi utaiona kambi ya JKT ya Msange. Hii kambi peke yake kuna misitu mikubwa sana ambayo zamani yalikuwa mashamba ya katani ya Mzungu. Huyu Mzungu alishindwa kutamka Msange na akawa anasema Masange. Ndiyo maana zamani kambi pia ilikuwa ikiitwa Masange na baadaye ndiyo ikabadilishwa na kuitwa Msange (Mkute). Kutoka hapo unaenda hadi huko kijiji cha Mbola, ni msitu mkubwa sana. Hahaaaaa, kijiji cha Mbola kuna mama mmoja ambaye anaishi kwa kupewa Msaada na Mwanamziki Maarufu na Producer aitwaye John Legends. Ukiingia kwenye ukurasa wake, utaona picha zake akiwa Mbola na ukisikia katua Tz basi ujuwe kaenda kumtembelea mama yake wa Mbola. Vuka Msange nenda hadi maeneo lilipo bwawa la Igombe kama sikosei, na vuka Igombe, huko kote ni msitu mzito sana wa Miyombo na safi sana kwa kufuga asali..........

Ntaandika zaidi baadaye kama nilivyoahidi na nafikiri KEIL na Mkuu Kichuguu watasaidia na wao maoni yao. Nitajadili zaidi sababu ambazo naona zimesababisha hali iwe hivi na nini kinaweza kufanyika maana si kulaumu tu ila pia kujaribu kutoa maelezo nini kifanyike.

Ktk ardhi hiyo ni miti aina gani inamea?,hasa ya kigeni (exortic trees), niliwahi kuomba msaada wa kujua kiwanda walau kidogo cha kusindika asali huko kwenu Tabora,mkaahidi kuni-PM mpaka leo kimyaaa.
 
Mlila nifuate Dec twende wote nikakupe Eneo. panalimika inategemea unatumia nyezo gani na kilimo kipi.

Safari yangu ya kutembelea Tabora ipo pale pale hata kama hujanipa PM uliyoahidi kunipa. Niliomba msaada wa location ya kiwanda/mtambo wa kusindika asali unaofanya kazi kwa sasa ili nikajifunze. Mimi nimebobea ktk misitu ya miti ya mbao na boriti,hivi punde nitaanza kilimo cha miti ya matunda,pia mimi ninapenda ufugaji. Kama ardhi yenu inakubali haya mambo matatu kwa pamoja basi siku moja utanikuta Tabora.

Mazao jamii ya nafaka sina mpango nayo kwa sasa,nikishapata trecta la nguvu ndio nitaanza mazao ya nafaka.
 
Back
Top Bottom