JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,308
- 5,462
Inadaiwa kuwa yalikuwa kwenye mkakati wa kucheleweshwa wa lengo la kutengeneza mazingira ya kupandisha bei ya mafuta hayo ambayo yalikuwa yanasafirishwa kutoka Jijini Dar-es-Salaam kuelekea mikoa ya Katavi, Tabora na Shinyanga ambayo kwa sasa inatajwa kuwa na upungufu mkubwa wa mafuta.
Akifafanua kilichotokea, Kaimu Meneja wa EWURA Kanda ya Mashariki, Walter Christopher amesema:
“Tumegundua kuwa mafuta haya yalifika zaidi ya saa 24, hali hiyo inaonesha kuna mchezo mchafu unaofanywa na Wafanyabiashara, magari haya yalikuwa na Dizeli na Petroli ambapo kila moja lina uwezo wa kubeba Lita 35,000 hadi 39,000, yalikuwa yanapelekwa Katavi, Nzega na Kahama.
“Kulingana na Sheria kuna adhabu ya faini au kifungo au vyote kwa pamoja, tutaangalia ukubwa wa kosa ambalo limetendeka.
Chanzo: Azam TV