Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Dr. Slaa nakukubali siku zote lakini kwenye hili umefanya makosa makubwa.

Sasa hivi mipango ya EL & Rostam ni kuwahusisha watu wengi kuwa ni mafisadi ili iwe vigumu wao kutoswa rasmi. Ingekuwa vizuri Chadema wasubiri kwanza vita kubwa inayokuja kati ya EL, RA & Chenge against CCM. Hapo Chadema wanachotakiwa kufanya ni kusubiri, ili NEC ikiwatosa hao watu rasmi, ndio sasa Chadema waseme wapelekwe mahakamani, wafukuzwe ubunge nk kama hoja ya msingi.

Unapoanza kugroup watu kama kina Magufuli, Malecela, JK na hawa Mafisadi papa, unacheza mchezo unaowafaidisha kina EL. Hata kama kina Mangula, Malecela wanamakosa madogo, lakini sio Mafisadi POINT BLANK.

This is a War, lazima kuwe na mipango inayoona mbali.

Sasa hivi ni kuwaisolate kwanza EL, RA, Chenge ili wao watumie pesa zao kuvunja CCM, na chadema wao itakuwa rahisi kuingia uko mbele na ndio uanze kuleta vioja mbalimbali.
Huwezi kuacha kumtaja au kumkamata mwizi kwa kuwa wengine hawajakamatwa, alichofanya Slaa ni kumwagilia petrol kwenye moto watajijua wenyewe wachague vita ipi nafuu ya sasa au ya zamani.
 
Kuwa na sera, mipango, mikakakti na malengo mbadala kuhusu uboreshaji wa maisha ya Mtanzania ndio njia pekee. Mwananchi akishasikia John Kato ni fisadi (tena hakuna mpango wa kuwawajibisha bali kusubiri mtu akapinge mahakamani) kutaboreshaje maisha?

Imefika wakati wa CHADEMA kuangalia upya viapaumbele vyao, kama wanataka mawazo waje hapa hapa JF tutawapa.

Tafuta Ilani ya Uchaguzi ya CDM ya 2010 usome, nakushauri usome ya CCM pia; maana unaomba vitu vilivyopo kwasababu hujui kuwa vipo!

Tatizo siyo Policy na strategy mbala, sikiliza pia vipindi vya Bunge maoni ya Mawaziri Vimvuli na Michango ya Wabunge wa Upinzani utaweza kupanua akili yako. Tatizo lililopo ni rai ya kutekeleza hayo yaliyopangwa na ridhaa ya ki-siasa kutoka kwa viongozi na watawala wa Africa kukubali dhana halisi ya vyama vingi na kuwapa wananchni fursa ya kufaidi matunda ya vyama vingi.
 
nyie magufuli msikieni tu fuatilieni stor zake kwenye jimbo lake alivyo mfanya mpinzani wake ni mbaya sana na nifisadi wa kutisha ccm wote awafai hilo linajulikana wako pale kwa ajili ya matumbo yao nakupeleka watoto wao ulaya tu
 
Maghufuli ni fisadi aliyekubuhu na hatari sana kwani ndiye aliyesuka mpango wa "kuuzwa" nyumba za serikali ambapo kilichofanyika kwa hakika ilikuwa ni wizi mtupu. nyumba zenye thamani ya mamia ya mamilioni "ziliuzwa" kwa bei ya kutupwa kwa "watumishi wa serikali" ambao kwa kweli walikuwa ni wajanja wachache waliogawana hizo nyumba. Zoezi lile limeisababishia serikali hasara kubwa inayodumu hadi leo hii kwani wapo watumishi wa serikali ambao hadi leo huishi hotelini kwa vile nyumba walizopaswa kuishi waliuziwa watangulizi wao. Katika mkumbo huu wapo mahakimu, majaji, watumishi wa idara mbalimbali za serikali n.k.
Maghufuli aliahidi kujenga nyumba mpya eti kwa ajili ilikuwa gharama kubwa mno kuzihudumia "chakavu" ziliozouzwa, ukweli ni kwamba baadhi a nyumba "ziluzwa baada ya kukarabatiwa kwa gharama kubwa mno. Miongoni mwa waliouziwa nyumba hizo alikuwa JK mwenyewe, Maghufuli ambaye upo ushahidi wa yeye kuuziwa nyumba kadhaa nyingine akiwanunulia vimada wake, waliokuwa wakuu wa majeshi kama Jenerali Mboma anayefahamika vyema kwa ufisadi, aliyekuwa IGP Mahita ambaye licha ya kuwa na utitiri wa nyumba aliuziwa nyumba ya Oysterbay, Makamba aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM na orodha ndefu ya waliokuwa viongozi wa CCM na serikali . Kwa kweli ule ulikuwa uporaji wa rasilimali za serikali uliofanywa na kundi la watu ndani ya serikali waliokubuhu kwa ufisadi.
Wengi wa waliouziwa nyumba hizo hawakuwa wahitaji kwani walikuwa tayari wakimiliki nyumba kadhaa na huo ulikuwa ukiukwaji mkubwa wa sheria na Katiba ya nchi ambayo inashangaza hadi sasa ni kwa nini CHADEMA kama chama makini hakikuufanya mtaji wa kisiasa. nilifarijika sana kumsikia Profesa Safari alipowakumbusha CHADEMA juu ya uhalifu ule uliofanywa na watu waliokuwa na dhamana ya kulinda mali za serikali. Ni matumaini yetu kwamba ipo siku tutapata serikali makini itakayowapokonya wezi hawa nyumba zetu na kuwafikisha mbele ya haki wote waliofisadi taifa hili. Kama kweli CCM wanasema wamejivua gamba na eti sasa ni wapambanaji wa ufisadi waanze na kurejesha nyumba zote za serikali zilizoporwa kwa ulaghai wa Maghufuli na Mkapa na wahakikishe wote wanawajibishwa. Kwa serikali makini hilo linawezekana kabisa kwani hata Hayati Baba wa Taifa aliwahi kutaifisha nyumba zilizojengwa kifisadi enzi za Azimio la Arusha. Wengi wameshazipangisha nyumba hizo zilizoporwa serikalini na wamezipangisha - jambo lililo kinyume kabisa cha sheria.
 
Tuliondoka Dodoma majira ya saa kumi kwenda Tabora kushuhudia tulicho tarajia, kwa kweli ilikuwa kama tulivyotarajia, watu walikuwa wachache sana tofauti na mikutano ya sept/october mwaka jana, na baada ya dr kuanza kutaja list ya wahindi mafisadi umati wa watu walianza kuondoka mkutanoni na kuacha watu wachache sana,huku wakipiga kelele za "tunataka hoja za maendeleo na siyo hadithi za ufisadi unaofanywa na wahindi wachache" nimerudi Dodoma na sasa niko kwenye tafrija ya chama lakini nitawawekea picha kidogo muone kwa macho yenu kile kilichojiri.

Hizi ndizo hoja za CCM! Tafuteni watu waliopevuka akili kuwakilisha CCM hii style ya Makamba na Tabwe bado mnayo hata baada ya Makamba kuondoka?
 
Hakuna ufisadi eeh? unakumbuka sababu ya kuvunjika uchaguzi wa viti maalum wanawake CDM?? au unakurupuka tu
Kama unaona huo ndio ufisadi wa CDM unaohatarisha uchumi wa taifa kweli CCM mmeishiwa niwa kuhurumia.
 
Dr. Slaa nakukubali siku zote lakini kwenye hili umefanya makosa makubwa.

Sasa hivi mipango ya EL & Rostam ni kuwahusisha watu wengi kuwa ni mafisadi ili iwe vigumu wao kutoswa rasmi. Ingekuwa vizuri Chadema wasubiri kwanza vita kubwa inayokuja kati ya EL, RA & Chenge against CCM. Hapo Chadema wanachotakiwa kufanya ni kusubiri, ili NEC ikiwatosa hao watu rasmi, ndio sasa Chadema waseme wapelekwe mahakamani, wafukuzwe ubunge nk kama hoja ya msingi.

Unapoanza kugroup watu kama kina Magufuli, Malecela, JK na hawa Mafisadi papa, unacheza mchezo unaowafaidisha kina EL. Hata kama kina Mangula, Malecela wanamakosa madogo, lakini sio Mafisadi POINT BLANK.

This is a War, lazima kuwe na mipango inayoona mbali.

Sasa hivi ni kuwaisolate kwanza EL, RA, Chenge ili wao watumie pesa zao kuvunja CCM, na chadema wao itakuwa rahisi kuingia uko mbele na ndio uanze kuleta vioja mbalimbali.

Mkuu huyu jamaa ajafanya kosa lolote lile tatizo hamjui kuwa hapa kuna mambo mawili uwizi kufanyika na wezi wakiwemo wakina malecela na la pili ni hawa wezi wakina malecela kuwalinda hawa wachora ramani za wizi. CCM inataka kuwahadaa wananchi kwa kuwatosa watu watatu au wanne tu na kurudi kwenye chat. anachosema dokta hapa ni kuwa CCM yote ni mafisadi na babu jinga hawezi tena kufurukuta. tatizo la nchi hii ni kwamba kuna wale wezi wanaotuibia kila mtu anawajua lakini wabaya sana ni hawa wakina malecela. Kumbuka ile issue ya Zitto aliyekuwa anaishabikia afukuzwe bungeni ni nani Rostam au Malecela. Walioiteka hoja ya mafisadi bunge lililopita ni nani RA? au mama kilango na mume wake na waliifikisha wapi? Kutuletea msanii tena kwa miaka mitano.

Subirini tu mtashangaa sana kwani hata wakina mwakyembe, sita , nape, na wengine ufisadi wao utatajwa tu muda sio mrefu. walikuwa na nafasi ya kuikomboa nchii hii wakagwaya kwa matendo yao maovu. Akilini mwangu najua kuwa hii dokta anabeep tu bado kubwa yake
 
HTML:
Jk sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .

- Lakini mbona amewakimbiza CC na NEC kama hana ubavu? I mean this time Slaa amekosea sana!

William @ NYC, USA.
Kwa vile kamtaja mzee
 
- Mkuu hela za EPA legally zilikuwa ni za mkopo sio kwamba zilikuwa ni hela za wizi, however ni hela zilizochukuliwa na kundi la Mtandao, toka hii ishu ianze tumeona wahusika wote wakitajwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria, sasa leo the question ni kwamba Where was Malecela huko nyuma mpaka aje aingie leo? Halafu Mtandao walikuwa wanapigana na Malecela sasa ilikuwaje tena wakampa hela hizo hizo wanazompiga nazo? It does not make any sense at all!

William @ NYC, USA.

Scrutinise walio-sign fedha kwaniaba ya Kagoda! alafu utwambie wao walifikishwa mahakamani lini?
 
List ya ya mafisadi waliotajwa ni wale waliochonga EPA na kuisimamia ila wale waliotekeleza walitajwa Mwembechai 2007. Sasa CCM ijivue gamba kwa kuwatosa viongozi wake wote walioiongoza hadi 2005!
wasipofanya hivyo basi CCM litakuwa ni gamba ambalo ni lazima Wananchi walivue ili kuwepo na chama kingine kipya ambacho kwa maoni yangu naona kitakuwa ni CHADEMA
 
- Another genius now what this has anything to do na maneno ya leo ya Slaa kwamba Malecela ni mmoja wa mafisadi wa EPA meaning kwamba alisani makaratasi ya kuchukua hizo hela benki kuu au?

William @ NYC, USA.

Najua huamni yalilikuta jina la Mzee john au lile la wakati Jumanne. Ila makamanda wamesema kama anaona ameonewa aende mahakamani wao watadhibitisha kwamba aliiba vipi. Kamanda mmetuibia sana sasa tumesema basi
 
- Unaenda kumfunga mtu kwasababu ya kutumia the word of mouth kuiba hela bank, you are a genius bro!

William @ NYC, USA.
Kutiwa hatiani kwa mtu si lazima hakimu aone sahihi yake kama sahihi ni issue majambazi ya benki huwa yanaweka wapi sahihi.
 
CDM tujipange zaidi ni vipi tutaimarisha chama chetu, hii ya mafisadi sasa imeanza kuchuja. tuangalie ni point gani nyingine ili tuingie nayo kuibomoa CCM.

Mkuu ni imani yangu kuwa wewe ni Chadema japo post hii inaonesha kuwa unavaa uhusika usiokuwa nao. You can note separate ufisadi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania. Hawa wapuuzi waliibia Taifa na kuwa na exposed income ambayo hawajui wafanye nini, matokeo ya ni ku-drive price of everything up, hasa katika miji mikubwa kama Dar kwenye upande wa viwanja, majumba just everything kwani hili genge lenye hela chafu halioni shida kununua nyumba ya Tshs 20m kwa Tshs 200M. Hebu niembie hard woker gani anayepata mshahara wa let say Tshs 800,000 kwa mwezi ataweza kujipatia sehemu yake ya kujihifadhi japo ajinyime kwa miaka miwili apate Tshs 15M?. Huwezi hata siku moja kutenganisha ufisadi na maendeleo ya nchi.
 
- Mkuu hela za EPA legally zilikuwa ni za mkopo sio kwamba zilikuwa ni hela za wizi, however ni hela zilizochukuliwa na kundi la Mtandao, toka hii ishu ianze tumeona wahusika wote wakitajwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria, sasa leo the question ni kwamba Where was Malecela huko nyuma mpaka aje aingie leo? Halafu Mtandao walikuwa wanapigana na Malecela sasa ilikuwaje tena wakampa hela hizo hizo wanazompiga nazo? It does not make any sense at all!

Ni kweli fedha hizi zilichukuliwa au kukopwa na wasio walengwa, pamoja na kelele zote hakuna mahali ccm wamekiri kukopa fedha hizo kwa ajili ya uchaguzi wewe ni mwana ccm na unasema wazi kuwa zilichukuliwa na wanamtandao huoni kama unaanzisha so nyingine kwa chama chako ya wizi wa njia za panya? niko tayari kusahihishwa katika hili
 
- Hoja yangu ni kwamba hela za EPA zilichukuliwa na kundi la Mtandao kwa ajili ya kampeni ya Urais against Malecela na wengine, unashitakiwa kwa wizi wa benki kama kuna sahihi yako katika kuchota zile pesa, unasema kwamba that is the case against Malecela na hela za EPA?

- Now hoja yako ni ipi mkuu?

William @ NYC, USA.

Malecela ni Fisadi Mkubwa sana ndani ya CCM kuliko wana-CCM wote! Ni mkongwe wa Ufisadi kifupi ndio walioleta mfumo mbovu ndani ya Chama na Serikali, ni kweli kisayansi unaweza kusafisha maji ya choo yakawa masafi lakini bado yataitwa maji ya chooni ingawa yatakuwa yametenganishwa na kinyesi, sidhani kama source ya maji itabadilika na kuwa mto au ziwa!

Wanaojua uchaguzi wa 1995 na Malecela wanaweza kumpima kuanzia huko. Katika suala la EPA si kweli kuwa fedha za EPA zilitumika dhidi ya Malecela huo ni Uongo unaojaribu kuupaka rangi ya ukweli, Malecele ni miongoni mwa majina yaliyoenguliwa awali kabisa kwa nguvu za M/kiti wa CCM Mr. Clean (kama alivyojulikana kabla ya kuingia madarakani) wala siyo fedha! Ni mwenyekiti ndie aliye simama na kumtaka atoe jina lake ili kumpa nafasi, hicho kitendo kilimuuma sana Malecela lakini kwa kuwa si msafi ni Fisadi hakuwa na jinsi bali kujinyamazia kimia na tuli.

Kama unataka Direct connection ya EPA na Malecela M-PM Dr. Slaa badala ya kulalama kutetea Uozo, {Ashakum si Matusi, Uozo ni Ufisadi siyo Malecela kama mfano wa maji ya chooni; uozo ni kinyesi siyo maji! ila kwakuwa maji yalichamba kinyesi basi yamechanganyika sijui yanaitwaje ila Civil Engineers wanaita "Blakish Water" Endelea kuyasafisha hakika inawezekana hasa ukiona wataalam wa maji taka na maji safi}
 
Dr. Slaa nakukubali siku zote lakini kwenye hili umefanya makosa makubwa.

Sasa hivi mipango ya EL & Rostam ni kuwahusisha watu wengi kuwa ni mafisadi ili iwe vigumu wao kutoswa rasmi. Ingekuwa vizuri Chadema wasubiri kwanza vita kubwa inayokuja kati ya EL, RA & Chenge against CCM. Hapo Chadema wanachotakiwa kufanya ni kusubiri, ili NEC ikiwatosa hao watu rasmi, ndio sasa Chadema waseme wapelekwe mahakamani, wafukuzwe ubunge nk kama hoja ya msingi.

Unapoanza kugroup watu kama kina Magufuli, Malecela, JK na hawa Mafisadi papa, unacheza mchezo unaowafaidisha kina EL. Hata kama kina Mangula, Malecela wanamakosa madogo, lakini sio Mafisadi POINT BLANK.

This is a War, lazima kuwe na mipango inayoona mbali.

Sasa hivi ni kuwaisolate kwanza EL, RA, Chenge ili wao watumie pesa zao kuvunja CCM, na chadema wao itakuwa rahisi kuingia uko mbele na ndio uanze kuleta vioja [/]

UShauri wako ungekuwa mtamu kama Chadema ingekuwa CCM-B maana ingekuwa inafanya for good of CCM -A; now this is different Chadema inafanya for good of nation, awe makamba mangula lowasa wote kama ni wezi ni wezi na hakuna wizi mdogo; to hell; sasa mpango sijui tumsuirie lowasa aanze aaaa na RA aanze bbbb this is sickness and bullshit. watakaangana kwa sababu chadema imewapa mahala pa kuanzia tofauti na hapo haisaidii yaani ushauri wako kama kazi angekuwa anaifanya Prof Lipumba ingekuwa njema maana lengo lake ni kuwasaiidia macomrade wake. anyway you dared to talk openly
 
Moelex said:
Dr. Slaa nakukubali siku zote lakini kwenye hili umefanya makosa makubwa.

Sasa hivi mipango ya EL & Rostam ni kuwahusisha watu wengi kuwa ni mafisadi ili iwe vigumu wao kutoswa rasmi. Ingekuwa vizuri Chadema wasubiri kwanza vita kubwa inayokuja kati ya EL, RA & Chenge against CCM. Hapo Chadema wanachotakiwa kufanya ni kusubiri, ili NEC ikiwatosa hao watu rasmi, ndio sasa Chadema waseme wapelekwe mahakamani, wafukuzwe ubunge nk kama hoja ya msingi.

Unapoanza kugroup watu kama kina Magufuli, Malecela, JK na hawa Mafisadi papa, unacheza mchezo unaowafaidisha kina EL. Hata kama kina Mangula, Malecela wanamakosa madogo, lakini sio Mafisadi POINT BLANK.

This is a War, lazima kuwe na mipango inayoona mbali.

Sasa hivi ni kuwaisolate kwanza EL, RA, Chenge ili wao watumie pesa zao kuvunja CCM, na chadema wao itakuwa rahisi kuingia uko mbele na ndio uanze kuleta vioja mbalimbali.

Moelex,

..kuwatosa Rostam,Chenge,na Lowassa, hakutoshi kuisafisha CCM.

..CCM walitaka kutupumbaza wananchi kwa kujidai kwamba hao watatu tu ndiyo wachafu na mafisadi ndani ya chama chao.

..binafsi naunga mkono Chadema kuongeza wana-CCM wengine kama Kikwete,Magufuli, na hata retired politicians kama Mkapa na Mangula.

..actually napendekeza Chadema waendelee kuongeza[expand, fine tune..] orodha ya mafisadi kadiri CCM wanavyoendelea kujivua magamba.

..Chadema waongozwe na UKWELI, na siyo kupiga mahesabu ya kisiasa ktk suala linalohusisha maadili ya kitaifa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom