Pasco_jr_ngumi
JF-Expert Member
- Nov 20, 2010
- 1,802
- 283
:A S 465::alien::sleepy::sleepy:CCM KWISHA.....................:rant:
Naona umeamka toka usingizini.
Huu ni msamiati ulioanzishwa na wabunge wapambanaji wa CCM waliokuwa wakiwapinga wale waliotajwa na kamati ya Bunge kushiriki ufisadi wa Richmond na Dowans.
Nilikuwa nina hamu sana ya kuipata orodha mpya ya mafisadi aliyoahidi kuitoa Dr. Slaa, siamini kama hili ndio bomu alilolipanga kulilipua leo na kuitikisa nchi kwa mshindo mkuu, naona sasa Mzee wetu anaelekea kuishiwa hoja.
Kwa mwendo huu siku nyingine Dr. Slaa akitangaza kutaja orodha mpya ya mafisadi sidhani kama watu watapata mshawasha wa kuisubiria.
William @ NYC, USA.[/U]
TUJIKUMBUSHE ORODHA YA 2007
1. Dr. Daudi T.S. Balali
2. Andrew J. Chenge
3. Basil Pesambili Mramba
4. Gray S. Mgonja
5. Patrick P.R Rutabanzibwa
6. Nazir Karamagi
7. Nimrod Mkono
8. Rostam Aziz
9. Edward Lowassa
10. Benjamin W. Mkapa
11. Jakaya Mrisho Kikwete
(1) wana JF naona kama kuna messages zinakuwa deleted na mtu anaitwa PAW...naomba tujuzwe kinachoendelea.
(2) Kwa sisi tulio mkunazini hatuna access na TV wala Radio, naomba aliyesikia hiyo listi aiweke humu, sio kuendelekza malumbano tu!
Akhsanteni.
Mkuu huyu jamaa ajafanya kosa lolote lile tatizo hamjui kuwa hapa kuna mambo mawili uwizi kufanyika na wezi wakiwemo wakina malecela na la pili ni hawa wezi wakina malecela kuwalinda hawa wachora ramani za wizi. CCM inataka kuwahadaa wananchi kwa kuwatosa watu watatu au wanne tu na kurudi kwenye chat. anachosema dokta hapa ni kuwa CCM yote ni mafisadi na babu jinga hawezi tena kufurukuta. tatizo la nchi hii ni kwamba kuna wale wezi wanaotuibia kila mtu anawajua lakini wabaya sana ni hawa wakina malecela. Kumbuka ile issue ya Zitto aliyekuwa anaishabikia afukuzwe bungeni ni nani Rostam au Malecela. Walioiteka hoja ya mafisadi bunge lililopita ni nani RA? au mama kilango na mume wake na waliifikisha wapi? Kutuletea msanii tena kwa miaka mitano.
Subirini tu mtashangaa sana kwani hata wakina mwakyembe, sita , nape, na wengine ufisadi wao utatajwa tu muda sio mrefu. walikuwa na nafasi ya kuikomboa nchii hii wakagwaya kwa matendo yao maovu. Akilini mwangu najua kuwa hii dokta anabeep tu bado kubwa yake
Huyu dkt Slaa hana lake jipya, na hatimaye baada ya kuisaidia CCM kutoka nje atarudi kulekule alikotoka kama wenzake wengi wanavyofanya.Tambwe Hiza,Akwilombwe......
Chama cha upinzani halisi ni CUF tu.
Asante kwa kutujulisha.......ingawa ni uwongo....CUF si mpinzani halisi....labda kwa kuipinga CHADEMA.....ina ndoa na CCM
kuna mwingine alikuwa anaripoti kwenye thread nyingine.....nae kwa sasa yuko kimya.............huku nako kuko kimya.............huenda kuna vurugu huko maana haiwezekani...au moderm zimeisha mafuta!!
ndoa ipo matatanihivi kwenye CC na NEC mpya mbona sijaona uteuzi wa majina ya CUF