Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
Ahsante sana kwa kutaja mafisadi.

Tatizo letu kubwa ni kuishi kwenye lindi la umaskini, maradhi na idadi ya wajinga kuongezeka. Je huku kutaja mafisadi kutaboreshaje maisha ya Mtanzania?
Ndugu yangu, yani umenisikitisha kiasi ambacho sijawahi kusitikika hivyo kwa muda mrefu sana!
Yani kweli umeshindwa kuona uhusiano uliopo kati ya ufisadi na wizi wa kupindukia unaofanywa na hao watu kwa mali za nchi hii na jinsi hali hiyo inavoathiri maisha yetu ya kila siku??
Wanaiba mali ambayo ingetumika kutuletea maendeleo sote, badala yake wanaitumia kwa kujinufaisha wao na familia na maswahiba zao. Huoni miradi hewa inayofanywa amabayo inatugharimu mamilioni kulipa kwa pesa ambayo tungewekeza kwenye maendeleo ya taifa letu.
Hatuna dawa hospitalini na huduma ni mbovu kupindukia, pesa ambayo tungetumia kuboresha huduma za afya zinaibiwa na mafisadi kwa faida zao binafsi. Wewe huoni hayo ????
Ndugu yangu, try to think outside the box.
 
Suala la polic kataja nyumba zao maisha yao kwa ujumla,kasema wanaish kwenye tembe
 
Ndugu yangu, yani umenisikitisha kiasi ambacho sijawahi kusitikika hivyo kwa muda mrefu sana!
Yani kweli umeshindwa kuona uhusiano uliopo kati ya ufisadi na wizi wa kupindukia unaofanywa na hao watu kwa mali za nchi hii na jinsi hali hiyo inavoathiri maisha yetu ya kila siku??
Wanaiba mali ambayo ingetumika kutuletea maendeleo sote, badala yake wanaitumia kwa kujinufaisha wao na familia na maswahiba zao. Huoni miradi hewa inayofanywa amabayo inatugharimu mamilioni kulipa kwa pesa ambayo tungewekeza kwenye maendeleo ya taifa letu.
Hatuna dawa hospitalini na huduma ni mbovu kupindukia, pesa ambayo tungetumia kuboresha huduma za afya zinaibiwa na mafisadi kwa faida zao binafsi. Wewe huoni hayo ????
Ndugu yangu, try to think outside the box.
Umkontho,
Usichoke kuwaelimisha. Tuna njia ndefu.
 
Kwanza acha kupiga mayowe.

Pili, ukishamaliza kusikitika, anza panua wigo wa fikra zako, inaonekana hujafanya hivyo siku nyingi sana.

Frankly, CHADEMA walete mpya, policy mbadala, strategy, management objective and action plans mbadala za kuboresha maisha ya Watanzania.
 
Ahsante sana kwa kutaja mafisadi.

Tatizo letu kubwa ni kuishi kwenye lindi la umaskini, maradhi na idadi ya wajinga kuongezeka. Je huku kutaja mafisadi kutaboreshaje maisha ya Mtanzania?
bila ya kuwajua utaanzia wapi kuwadhibiti? ni lazima ujue ni kina nani , na wanatumia mbinu gani kuhujumu? amka
 
bila ya kuwajua utaanzia wapi kuwadhibiti? ni lazima ujue ni kina nani , na wanatumia mbinu gani kuhujumu? amka

Kuna fisadi gani mpya hapo?

Toka umeanza kusikia ufisadi wa Kagoda, wa wa nyumba za serikali ni miaka mingapi imepita.

Wake up people.
 
Hi coverage ya leo mh ... haijatulia list ngoja tusubiri
 
Kwa mwendo huu, nahisi na mimi Selemani pia nitatoka kwenye list ya mafisadi one day. @Dr. W. Slaa vipi muheshimiwa na mimi simo kweli?

Nakumbuka niliwapoza vijana wa Majembe na wekundu ili wasikitow ki-Starlet changu pale Barclays opposite na Movenpick. I did cost the city of Dar 120K that day.
 
Kwanza acha kupiga mayowe.

Pili, ukishamaliza kusikitika, anza panua wigo wa fikra zako, inaonekana hujafanya hivyo siku nyingi sana.

Frankly, CHADEMA walete mpya, policy mbadala, strategy, management objective and action plans mbadala za kuboresha maisha ya Watanzania.
Bora kipofu ambaye haoni kuliko anayeona halafu anajifanya kipofu
 
CDM hawana jipya bora tu chama changu CCM kijisafishe,tusubiri chama kingine cha kijamaa,from real tanzanians!....the rest is just blah! blah!
 
Kwa mwendo huu, nahisi na mimi Selemani pia nitatoka kwenye list ya mafisadi one day. @Dr. W. Slaa vipi muheshimiwa na mimi simo kweli?

Nakumbuka niliwapoza vijana wa Majembe na wekundu ili wasikitow ki-Starlet changu pale Barclays opposite na Movenpick. I did cost the city of Dar 120K that day.
Tatizo lenu mlifikiri atataja majina mengi naona mlipumbazwa na neno LISTI YA MAFISADI
 
Sasa Freema, matibabu bora utapataje bila kujenga hospitali bora na vifaa bora, hela ambayo inatumika kifisadi kupeleka mafisadi nje ya nchi kwa matibabu na watalipa wasindikizaji au ndugu? au ulitaka Slaa ndo atoe hela yake mfukoni?, Elimu bora utapataje kama walimu hawalipwi vyema na hamna shule za kutosha wakati huo huo hizo hela zinachukuliwa na mafisadi na kwenda kuwekeza nje ya nchi? Maji safi utapataje pasipo hela na miundo mbinu nk? Hao mafisadi ndo unatakiwa uwaulize hayo, maana unajua hela ya kodi inakoenda. A heri hata wangekuwa wanaiba wanawekeza nchini, wao wanazipeleka kuziwekeza nchi za nje (ambapo watawala wao wanazitumia kujenga huduma za jamii huko kwao). Nashangaa mtu anapotetea wezi :sleepy:.
Nashindwa kuelewa kama vyama vya siasa vinaelewa jukumu lao au wanafanya maigizo.

Tunataka matibabu bora, elimu bora, maji safi na salama, mazingira safi etc.

Kama umeishi miongo minne kama mimi una hakika kabisa hii taja taja ya mafisadi haijaanza leo, wengine na mahakamani wamefikishwa. Je imeleta impact gani kwenye maisha ya Mtanzania zaidi ya kuongeza kura za mgombea Urais wa CHADEMA?

Hebu wananchi tufungue macho, tujiulize maswali magumu, tufanye tathmini ya viongozi wetu na wale tuliowapa dhamana ya kutuwalisha, tupeane feedback kama malengo yametimizwa, kama hayajatimizwa wapi tumekwera mrama, tufanye nini ili tusiende mrama etc...

I see ulivyoshirikisha ubongo na mikono yako kuandika haya.
 
TBC watarusha live? Si Wanajiendesha kwa kodi zetu bana. La sivyo nao wajumuishwe kwenye orodha ya mafisadi, wanatuibia kodi zetu

Imeipata wapi?jibu ni humo humo ccm!sasa ni staili ya mwaga mboga nitupe ugali.
Kazi ipo tusubiri majina.

Saturday, 16 April 2011
Fidelis Butahe

WAKATI Chama Cha Mapinduzi (CCM) kikijivua gamba kwa kuwataka wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe kwenye uongozi wa chama hicho, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa leo anataja orodha mpya ya mafisadi ndani ya chama hicho tawala ili nao waunganishwe katika orodha hiyo.

Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa Chadema, Singo Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa Dk Slaa atataja majina hayo leo mkoani Tabora katika mkutano wa hadhara kama alivyofanya mwaka 2007, katika Viwanja vya Mwembeyanga, Dar es Salaam.

Alisema katika mkutano huo, Dk Slaa akiwa na viongozi wengine wa Chadema, atataja majina hayo ya mafisadi ili kuipa CCM wakati mzuri wa kuwatambua na kuwachukulia hatua kama kweli ina nia njema ya kujivua gamba.

Hii ni changamoto mpya kwa CCM ambayo tayari imenyooshea kidole genge la mafisadi lililoko ndani ya chama hicho na kuwapa siku 90 watuhumiwa hao kujiuzulu ili kukinusuru.

Bensoni aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa orodha hiyo mpya ya mafisadi inayotarajiwa kutajwa leo, ni kubwa kuliko ile ya mwaka 2007.

“Ushahidi tunao ndiyo maana hata tuliowataja mwaka 2007 hadi leo hawajafungua kesi yoyote mahakamani. Wanasema kuwa wamejivua gamba. Gamba la CCM siyo uzee ni ufisadi,” alisema Bensoni na kuongeza: “Tutawakumbusha gamba wanalotakiwa kujivua ni lipi ili Watanzania watambue. Dk Slaa ataweka mambo hadharani katika mkutano huo akiwa pamoja Profesa Abdalah Safari na Mabere Malando.”

Alisema licha ya CCM kutoa siku 90 kwa watuhumiwa wa ufisadi wanaotajwatajwa, wapo ambao hawajatajwa kati ya waliotakiwa kujiuzulu kwa tuhuma za hizo. “Hapa sasa ndiyo watajua mafisadi ni kina nani. Tunataka kuwakumbusha gamba ni lipi.”

Alisema kuwa orodha hiyo ni mpya na ina tofauti na ile ya Mwembeyanga kwa kuwa tangu kipindi hicho mpaka leo kuna matukio mengi ya ufisadi yaliyoendelea nchini. “Ufisadi wa sasa ni mkubwa sana hivyo orodha itakuwa kubwa, ‘Ni ngoma nzito’ na tukimaliza kutaja orodha hiyo tutaendelea na mikutano yetu nchi nzima,” alisema Bensoni.

Akizungumzia hatua hiyo ya Chadema, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema: "Chadema wamefilisika kisiasa, walidhani wataitisha CCM kwa hoja ya ufisadi lakini sasa CCM ni chama safi. Kwa mabadiliko tuliyoyafanya, Chadema inatakiwa kucheza ngoma yetu (CCM) na siyo sisi (CCM) kucheza ngoma yao."

Nape alitumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa uamuzi wake wa kukubali kurudisha muswada wa Katiba kwa wananchi na kuwapa fursa zaidi kujadili suala hilo.

MAFISADI WAPYA HADI SASA NI ;
  1. John Kato mwajiriwa Caspian (KAGODA).
  2. Bharati Goda ni mwajiriwa caspian (KAGODA).
  3. John Samweli Malecela –EPA
  4. Philip Mangula – EPA
  5. John Magufuli – nyumba za Serikali.
SAMAHANI SIJAWEZA KUIHARIRI ILA HAYO NDIO YANAENDELEA .NTAWAJUZA ZAIDI.
PROF.SAFARI.
Anasema kuwa ni wakati wa kudai nyumba za serikali kwa nguvu ya umma , kwani kwenda mahakamani sio muafaka kwani hata majaji wenyewe walijiuzia hivyo hawawezi kutoa haki.
Zidaiwe kwa nguvu ya umma ndio njia pekee ya kupata nyumba hizo kwani viongozi wengi wanakaa hotelini.

Udini.
Wakoloni waliwagawa watu kwa njia za makabila ili wawatawale ,wakagawa watu kwa njia za udini mf.waingereza waliingiza dini na kjuweka watu wao serikalini , na waislamu wengi walikosa nafasi ya kusoma ndio maana hawakuingia serikalini mapema .
Waislamu walipigania uhuru ila , kutokana na waingereza kuwabagua , ndio maana waliamua kupinga ukoloni ili waweza kuweka serikali ambayo haiwabagui, anasema ugomvi wa Nyerere na shehe takadir kuhusu waislamu kubaguliwa , na anasema kuwa ndani ya CDM hakuna udini ila ndani ya nchi kuna tatizo la kihistoria la kidini.
Anasema kuwa ni mbinu ya serikali kuwagawa watanzania ili waweze kuwatawala .
Alipojitoa CUF na kujiunga na CDM alifuatwa na mashehe wakimwambia kuwa yeye ameamua kujiunga na wakristo , yeye akajibu kuwa walitaka yeye aende kwenye chama gani? Mbona CCM sio ya waislamu kwani ukiondoka JK wengi waliopo serikalini ni
Anasema yeye hajabatizwa na pia Slaa sio yohana mbatizaji na amewataka waislamu kuungana pamoja ili kupigania haki za waislamu kwani CCM ndio ambao wanawakandamiza waislamu hivyo ni bora wakajiunga na CDM kwa wingi ili waweze kudai haki zao tangu awali na wasisubiri , waingie cdm tangu mwanzo ili wawe sehemu ya kupigania haki zao na njia nzuri ni kuhakikisha nkuwa wanajiunga ili kuingiza hoja zao kabla ya cdm kuingia serikalini na ni lazima waislamu wakitaka madai yao yasikilizwe wanapaswa kuingia sasa na sio wawasusie cdm kwa hoja za udini halafu baadae waje walalamike .
Kuna haja ya kujiunga na cdm sasa.

MARANDO.
Ameanza kwa kusema Slaa alishinda ila kura zilichakachuliwa na hivyo ndio maana Slaa ameamua kuingia kazini rasmi kujenga chama ili kiwe imara na kuweza kujiandaa na uchaguzi ujao .
Anasedma yeye ataongelea mambo matatu.(KATIBA , EPA , NA MAGAMBA YA CCM).
KATIBA .
Hii ilikuwa hoja ya CDM kwani iliyopo inawafanya mafisadi watamalaki, katiba ni maji, ni unga ni kila kitu ambacho kipo , ukishaweka katiba mengine yote yanawezekana .
Anasema JK alishauriwa na watu kuhusu katiba , ila aliweza kjuipata muswada wa sheria kutokana na taaluma yake ya kishushu aliupata mapema na kuisambaza a kwani jk hakuwa tayari kupata katiba .
Amewataka watanzania kuwa macho kwani nia ya ccm ni kuendelea na katiba iliyopo na sio kweli kjuwa wanataka katiba mpya.
Tofauti ya CCM na CDM kwenye katiba ni kuwa CCM wanataka iliyopo iwekwe viraka , na CDM wanataka mpya .
Cdm wanataka mambo yafuatayo kwenhye katiba mpya.
1. Kupunguza madaraka ya rais haswa ktk kuteua watu mbalimbali.
2. Viongozi wa wilaya wapigiwe kura na sio kuteuliwa na rais…..
3. Madini yalindwe na katiba
4. Power of recall kwa wabunge na madiwani
Kuhusu EPA na magamba ya CCM.
Ccm ndio gamba la watanzania na tunapaswa kuliondoa hilo gamba ccm na sio wao waondoane wenyewe
Ccm ndio gamba lenyewe na linapaswa kuondolewa moja kwa moja
Lissu amewafundishwa wabunge sheria .
Epa ni ya jk kwani ndio ilimuingiza madarakani.
Kikwete amesamehe wezi wa EPA wakati wezi wanapaswa kupelekwa jela .
Slaa alipotaja mafisadi ccm walisema ni uongo kuwa hakuna mafisadi , jk juzi kakiri kuwa kuna mafisadi wengi ndani ya chama na walitaja listi yao ya mafisadi , lowass,change na rostam.
Jk sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .
Jk alishindwa hata kujua mafisadi dowans.
Kagoda .
Kuna visamaki vidogo vimeshitakiwa ila kagoda hawajapelekwa mahakamani ,rais alisema hawajui wahusika wa Kagoda ,
Kemhondo willium ni jina la bandia – John Kato mwajiriwa Caspian
Francis wilium jina bandia –Bharati goda na ni mwajiriwa caspian
Aliweka majeshi yake kwa siku tatu na majina halisi ni haya;
Na jk kama hawajui aende ofisini kwake atampa mpaka picha
Kama jk anataka atume watu ofisini kwake ili waende kuchukua picha .
Anasema yuko tayari kama jk akimtaka kujitolea apewe jalada la kagoda na atawafikisha mahakamani na wataishia keko.
Wengine kagoda ni malecela na Mangula .
Cdm tulimuita safari ili aje aweze kutueleza ni jinsi gani tunaweza kiutatua matatizo ya waislamu na pindi tukiingia madarakani tutakuwa tayari kuzitekelezaz kwani ccm kwa miaka 60 wameshindwa kutatua matataizo hayo.

DR.SLAA.
Ameanza kwa kuwataka maasikari kuacha siasa na haswa jana walipoamua kuzuia maandamano kwa madai kuwa hali ya nchi ni tete , amewataka polisi kuacha kufanya siasa.hiyo hali wameipima hospitali gani mpaka kujua hali ni tete , na pia pesa zimeibiwa ndani ya jeshi la polisi na hata mdhibiti mkuu amesema uozo wa polisi.
Sababu ya pili waliyotoa polisi kuwa hoja yetu ya maandamano imefutwa na serikali ,hiyo sio kazi ya polisi kusema kuwa maandamano yamevunjwa .
Polisi kuweni na uchungu na nchi hii kwani mama, baba , watoto wenu wanaumia sana kutokana na ufisadi wan chi hii, pia usalama wa taifa wanapaswa sasa kuamka na kulinda masilahi ya taifa na sio kulinda masilahi ya viongozi kama wanavyofanya sasa.
Nchi haiwezi kutawalika ni mpaka mafisadi wote wakamatwe kwani haiwezekani kluwa na mafisadi na nchi ikaweza kutawalika.
Wananchi wa tabora kwa ujumla wenu mmefanywa kuwa wateja wa CCM kwani hii ni ngome yao ya kuvuna kura wakati hakuna hata barabara kwenye mkutano wenu.
Hawezi kujibu vyama wanaozunguka kuisema CDM ila hoja yake ni maisha ya watanzania tuu na sio vinginevyo kwani maisha ni magumu kwa kila mwananchi bila kiujali vyama vyao.
Maeneo waliyoikataa ccm kuna lami ila huku ambako kuna ccm hakuna barabara , za kwenda Urambo,Bukene, Nzega … huku mmetelekezwa .
Rais anaahidi kujenga viwanja vya ndege wakati cha Tabora hakitumiki sasa hivyo vipya anaweza?
Kwa taarifa yenu mimi ni mwana Tabora kwani nilikulia na kusoma Itaga , wakati huo kulikuwa na viwanda vya nyuzi, maziwa n.k. na kwelina sababu nzito ya kuikataa CCM.
Makisio ya kodi ya tabora mwaka huu ni kulipa serikali kuu 9.9 bilioni.ila hakuna barabara je?kodi zenu zinapelekwa wapi?
Anazungumzia juu ya nyumba za serikali na sasa muda umeisha wa kuendelea kuvumilia kuhusu nyumba za serikali lazima sasa zirejeshwe mara moja .
Mkapa anahusika na uuzwaji wa nyumba za Serikali.
Wale wanaosema kuwa slaa anamchukia jk kwa sababu ya dini . kwani alimshughulikia sumaye .
Mkapa na Magufuli kwenye kuuza nyumba za serikali na wao ni mafisadi .
Ndege za jk za kampeni zilitoka kwa watu walioiba EPA na ndio maana ameshindwa kuchukua hatua kwani anashirikiana nao .
Kama JK kawapa mafisadi siku 90 ndani ya chama chake nay eye Tunampa JK na eye siku 90 ataje fedha za mabango yake dola 1.5 milioni aseme zilitoka wapi zilizotumwa CANADA kutengeneza 2010 election .na yeye anapaswa kujitoa kama atashindwa kuchukua hatua hizo.

hii timu iliyotoa tamko imetulia,wamemaliza mwanzo-mwisho kuweza kuweka bayana matatizo yetu watanzania.

Udini,ufisadi& katiba mpya; ndio vitu vibovu vinavyotuvuruga watanzania leo hii. Ahh chadema wamemaliza

Asante dr.slaa,marando, prof.safari na chadema kwa ujumla kwa mchango wao mkubwa kujitoa kuwaeleza umma wa watanzania chanzo cha matatizo yao.
 
Sasa Freema, matibabu bora utapataje bila kujenga hospitali bora na vifaa bora, hela ambayo inatumika kifisadi kupeleka mafisadi nje ya nchi kwa matibabu na watalipa wasindikizaji au ndugu? au ulitaka Slaa ndo atoe hela yake mfukoni?, Elimu bora utapataje kama walimu hawalipwi vyema na hamna shule za kutosha wakati huo huo hizo hela zinachukuliwa na mafisadi na kwenda kuwekeza nje ya nchi? Maji safi utapataje pasipo hela na miundo mbinu nk? Hao mafisadi ndo unatakiwa uwaulize hayo, maana unajua hela ya kodi inakoenda. A heri hata wangekuwa wanaiba wanawekeza nchini, wao wanazipeleka kuziwekeza nchi za nje (ambapo watawala wao wanazitumia kujenga huduma za jamii huko kwao). Nashangaa mtu anapotetea wezi :sleepy:.

Kuwa na sera, mipango, mikakakti na malengo mbadala kuhusu uboreshaji wa maisha ya Mtanzania ndio njia pekee. Mwananchi akishasikia John Kato ni fisadi (tena hakuna mpango wa kuwawajibisha bali kusubiri mtu akapinge mahakamani) kutaboreshaje maisha?

Imefika wakati wa CHADEMA kuangalia upya viapaumbele vyao, kama wanataka mawazo waje hapa hapa JF tutawapa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom