Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Tabora: Dk Slaa ataja orodha mpya ya mafisadi!

Status
Not open for further replies.
- Mkuu hela za EPA legally zilikuwa ni za mkopo sio kwamba zilikuwa ni hela za wizi, however ni hela zilizochukuliwa na kundi la Mtandao, toka hii ishu ianze tumeona wahusika wote wakitajwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria, sasa leo the question ni kwamba Where was Malecela huko nyuma mpaka aje aingie leo? Halafu Mtandao walikuwa wanapigana na Malecela sasa ilikuwaje tena wakampa hela hizo hizo wanazompiga nazo? It does not make any sense at all!

William @ NYC, USA.

Hapo kwenye maneno, "legally zilikuwa ni za mkopo" una maana kuwa CCM walikopa fedha kihalali kutoka vyombo vya fedha kwa taratibu za mikopo?kama ni kweli hizo taratibu na masharti ya mkopo yalikuwaje? wakati wa urejeshaji ilikuwaje mpaka watu watajwe kama mafisadi ndiyo wakaanza kurejesha fedha? hata hivyo kwanini waliokuwa wakirejesha siyo (CCM) waliokopa bali watu wengine (mafisadi)?kundi la mtandao (ambalo siyo CCM) ulilotaja lilitoka wapi? una maana fedha ziliibwa mikononi mwa CCM na wanamtandao?

Ninachoona unakubaliana na ukweli kuwa CCM walichukua fedha lakini hapo hapo unataka kusema kuwa Malecela hakuhusika. Kwa vipi Malecela hakuhusika wakati yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM?

Kwa hiyo Malecela naona wamtetea Malecela bila kuwa na hoja zinazotosheleza kujibu maswali ya msingi juu ya wizi wa EPA.
 
sasa kama walikopesha kwa njia harali makubaliano ya riba ilikuwa shilling ngapi? na deni lilikuwa limepangwa kulipwa kwa kipindi gani? na hii ni kwa vyama vyote au ni ccm tu ndio wanaruhusiwa kukopa? maana hayo matukio ni ya hivi karibuni wakati wa vyama vingi
Mkuu naona unatuchanganya EPA legally zililiuwa ni hella za mikopo.en heee tumebie

  • Legally zikakopwa kwa kampuni gani?
  • Na legally wahusika wa hizo kampuni ni kina nani?
  • Je Legally BOT nayo imekuwa benki ?
Ukiongelea EPA Tanzania hakuna legality yeyote ni wizi. acha siasa.
------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Kwa wale wana CCM time is running out .Kikwete alitakiwa kufanya machache kumfunika MKapa sasa Yeye na aliyemtangulia hakuna tofauti.

JK naye alidangaya toto kuwa atarudisha nyumba kabla ya kuingia madarakani . Miaka saba bado amiri jeshi mkuu anashindwa kuchukua maamuzi mapesi ya kumjenga japo kidogo kwa kwa wanachi . Anamuogopa nani? kwa faida ya nani? Ya watanzania au ya wachache.?
 
Hoja gani umetoa? kuwa Malecela hakuhusika kwenye uchaguzi na hizo pesa kisa yeye ndio alikuwa mpinzani? Unataka kusema Malecela alikaa kando kwenye uchaguzi 2005? Hakuhusika baada ya kushindwa?
Pia hapa tunaongelea credibility yako kwanza! Tutegemee nini leo kwako wewe Malecela? Tungetegemea ukubali shutuma?hahaha
Wacha kutufanya maandazi sasa! This is the end of an era!
U dare to talk openly maana unajua huwezi enda chini. Tukienda mahakamani utasikia jadala limepotea, nk! Usijetudanganya kuwa wewe ni jasiri kupita wote hapa!

- Hoja yangu ni kwamba hela za EPA zilichukuliwa na kundi la Mtandao kwa ajili ya kampeni ya Urais against Malecela na wengine, unashitakiwa kwa wizi wa benki kama kuna sahihi yako katika kuchota zile pesa, unasema kwamba that is the case against Malecela na hela za EPA?

- Now hoja yako ni ipi mkuu?

William @ NYC, USA.
 
- Mkuu Chadema mbona hawajampeleka Sophia Simba mahakamani kwamba wanapewa hela kutoka nje kuleta vurugu, halafu jaribu kujibu hoja kwa hoja kama huna basi wapo hapa, huu ni uwanja wa hoja sio viroja, so lete hoja bros! I dare to talk openly ndio maana ninaingia kama nilivyo na picha pale juu!

William @ NYC, USA.
Hivi wewe Malecela unadhani unaweza kusema kitu kinyume na hicho kibabu chako?? Ni afadhali ukae kimya tu maana hujui kitu wewe.
 
Hapo kwenye maneno, "legally zilikuwa ni za mkopo" una maana kuwa CCM walikopa fedha kihalali kutoka vyombo vya fedha kwa taratibu za mikopo?kama ni kweli hizo taratibu na masharti ya mkpo yalikuwaje? wakati wa urejeshaji ilikuwaje mpaka watu watajwe kama mafisadi ndiyo wakaanza kurejesha fedha? hata hivyo kwanini waliokuwa wakirejesha siyo (CCM) waliokopa bali watu wengine (mafisadi)?kama ni kweli kundi la mtandao (ambalo siyo CCM) lilitoka wapi? una maana ziliibwa mikononi mwa CCM na wanamtandao?

Ninachoona unakubaliana na ukweli kuwa CCM walichukua fedha lakini hapo hapo unataka kusema kuwa Malecela hakuhusika. Kwa vipi Malecela hakuhusika wakati yeye alikuwa makamu mwenyekiti wa CCM?

Kwa hiyo Malecela naona wamtetea Malecela bila kuwa na hoja zinazotosheleza kujibu maswali ya msingi juu ya wizi wa EPA.

- Majina ya watu wote waliohusika na EPa yalitajwa na kufikishwa mahakamani ni kwa sababu walisaini makaratasi, sijui unawezaje kumfunga mwananchi kwa sababu kundi moja la chama chake lilihusika na kuchukua pesa za EPA, I mean is this a great thinking?

William @ NYC, USA.
 
Hakuna jina jipya, hebu tupe feedback wa nani aliyefilisiwa baada ya kutajwa fisadi? Lowassa kapelekwa mahakamani, Chenge je, Karamagi, Meghji, Sumaye - tena huyu kageuka kuwa mlaani ufisadi, lolestiest.

Kama CHADEMA walishawataja hawa mvua kadhaa zilizopita kwa nini wanarudia kuwataja - tena hata wakifanya hivyo kwa matarumbeta na brass band - sirikali haiwezi wapeleka mahakamani na wanajua hilo.

Je ndio kusema CHADEMA wameishiwa hawana mawazi mapya pamoja kuwa na vijana wengi - if Lissu is also kijana.

@ Jasusi - nawaomba CHADEMA waandae sera, mipango, mikakati na malengo mbadala kuhusu uboreshaji wa maisha ya Mtanzania. Kama wamejaa hapa mbona wamekurupuka kwenda Tabora na kurudia mambo ambayo ni 'so over'.

Hakuna jipya kwa sababu uangalii mbali.
Lisiti ya majina ilitolewa - hakikutokea kitu
Kuanzia BM - sirikari inajua ila haitaki kutimiza wajibu wake.
Sasa kwa sababu katiba imekaa mshazari - basi Chadema ni lazima waende vijijini kufafanua kwa wananchi kwa nini matakwa ya wananchi hayatekelezwi, yanapuuzwa na dawa ni ipi? Katiba mpya siyo matakwa ya CCM - hilo hata wewe unalijua.
Chadema haitaki kuchukua njia ya Misri, Tunisia, Libya au yanayoendelea sasa Uganda.
Dada (kama wewe ni dada) - kuna uwezakano hapa nchini wa mtu binafsi au taasisi isiyo ya sirikari kumfikisha fisadi kortini? Kama unakifahamu kipengele hicho kwenye katiba yetu ya sasa - tafadhali mshutue Lisu.
 
Bwana Wiliam mbona uwezo wako wa kufikiri ni mdogo?
Nasema amefanya michoro mingi ila nilipo mfahamu ni kwenye uchaguzi wa biharamulo!!
Fikiria kabla ya kujibu. Soma uelewe ninachosema. Hata kama ni baba yako lakini alikosea. Alipokosea unatakiwa kusema samahani kuliko kutetea. Well, ukweli utajulikana soon or with time. Nitakupigia simu!!

- Malecela ni fisadi kwa sababu alienda kwenye uchaguzi wa Biharamulo na kubadili namba za magari ya serikali ili CCM ishinde, ndio maana Dr. Slaa amemuita fisadi wa EPA, well you are a genius!

William @ NYC, USA.
 
HTML:
Jk sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .

- Lakini mbona amewakimbiza CC na NEC kama hana ubavu? I mean this time Slaa amekosea sana!

William @ NYC, USA.
Will you shut up your big mouth. You are talking nonsense
 
HTML:
Jk sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .

- Lakini mbona amewakimbiza CC na NEC kama hana ubavu? I mean this time Slaa amekosea sana!

William @ NYC, USA.

It is just your wishful thinking.
 
Bwana Wiliam mbona uwezo wako wa kufikiri ni mdogo?
Nasema amefanya michoro mingi ila nilipo mfahamu ni kwenye uchaguzi wa biharamulo!!
Fikiria kabla ya kujibu. Soma uelewe ninachosema. Hata kama ni baba yako lakini alikosea. Alipokosea unatakiwa kusema samahani kuliko kutetea. Well, ukweli utajulikana soon or with time. Nitakupigia simu!!

- Mkuu sawa sawa nimekuelewa alichora michoro mingi ndio maana Slaa anasema ameiba hela za EPA hilo nimekuelewa sana mkuu!

william @ NYC, USA.
 
- Hoja yangu ni kwamba hela za EPA zilichukuliwa na kundi la Mtandao kwa ajili ya kampeni ya Urais against Malecela na wengine, unashitakiwa kwa wizi wa benki kama kuna sahihi yako katika kuchota zile pesa, unasema kwamba that is the case against Malecela na hela za EPA?

- Now hoja yako ni ipi mkuu?

William @ NYC, USA.

Mkuu kama wewe una uhusiano na mzee malechela ni the same CCM unaweza kuwaomba msahama watanzania kwa niaba ya mzee akikubali yake kwa makosa aliyofanya na yiliyofanywa na chama chake.

Tatizo la wanasiasa likimbumbuluka kila mmoja anajitenga lakini Mzee malechelea alikuwa katika top hierechy ya chama . Huwezi kumuweka kando na Ovu lolote la CCM for past ten years.

Tuwaambie wazee wetu kukubali makosa ni mwanzo mpya tena mzuri. Ni njia ya kjivua magamba pia. Tusitetee tuuuuuuuu.
Mbona politician wa nje wanaomba radhi . Sijawai kusikia hawa viongozi wetu wakikiri makosa. ya kitendaji au kimaamuzi.

Hata kama EPA zilikuwa za mtandao na Mzee kwanza alijua alifanya nini kudhibiti au kupiga kelele. na yeye alikuwa na ana EPA zake sema watanzania tulikuwa hatujaamka usingizini miaka hiyo. Si unakumbuka ile ya kuusaka urais na ufadhili wa IRAN?

- Hayo ni maswali BOT na Serikali, sio Malecela.

William @ NYC, USA.

kama ni maswali ya BOT na serikali wewe umethibitisha vipi legality yake .
 
Mkuu kama wewe una uhusiano na mzee malechela ni the same CCM unaweza kuwaomba msahama watanzania kwa niaba ya mzee akikubali yake kwa makosa aliyofanya na yiliyofanywa na chama chake.

Tatizo la wanasiasa likimbumbuluka kila mmoja anajitenga lakini Mzee malechelea alikuwa katika top hierechy ya chama . Huwezi kumuweka kando na Ovu lolote la CCM for past ten years.

Tuwaambie wazee wetu kukubali makosa ni mwanzo mpya tena mzuri. Ni njia ya kjivua magamba pia. Tusitetee tuuuuuuuu. Ni njia
Mbona politician wa nej wanaomba radhi . Sijawai kusikia hawa aviongozi wetu wakikiri makosa. ya kitendaji au kimaamuzi.

- Mkuu tunaongela hela zilizochuliwa Benki kwa jina la EPA, unasema una ushahidi kwamba Malecela alisaini moja ya hayo makaratasi ya kuchukua hizo hela? Na ndio maana Slaa akamtaja kwamba anahusika na EPA au?

- Well, naomba kuondoka kidogo, later people!

William @ NYC, USA.
 
- Majina ya watu wote waliohusika na EPa yalitajwa na kufikishwa mahakamani ni kwa sababu walisaini makaratasi, sijui unawezaje kumfunga mwananchi kwa sababu kundi moja la chama chake lilihusika na kuchukua pesa za EPA, I mean is this a great thinking?

William @ NYC, USA.

Kwa hiyo walifikishwa mahakamani na benki ilyowakopesha CCM?Wamefikishwa makamani kwa kosa lipi? Hoja yetu ni wizi wa fedha za EPA, je unakubali kwamba waliofikishwa mahakamani ni wezi? Kama ni wezi, je, suala kuwa CCM ilikopa fedha limeishia wapi?
 
HTML:
Jk sio jasiri na hana ubavu wa kuweza kupambana na mafisadi wa ndani ya chama chake kwani hawezi kuchukua hatua .

- Lakini mbona amewakimbiza CC na NEC kama hana ubavu? I mean this time Slaa amekosea sana!

William @ NYC, USA.

Alitakiwa kufanya hayo 2006.
Ya sasa ni kuwa amesoma ishara.
Hata ingekuwa wewe - choices pressed on you - unasuka au unanyoa.
 
Kwa hiyo walifikishwa mahakamani na benki ilyowakopesha CCM?Wamefikishwa makamani kwa kosa lipi? Hoja yetu ni wizi wa fedha za EPA, je unakubali kwamba waliofikishwa mahakamani ni wezi? Kama ni wezi, je, suala kuwa CCM ilikopa fedha limeishia wapi?

- Walifikishwa mahakamani kwa sababu hawkutakiwa kuhusika na kukopa zile hela, na waliofikishwa mahakamani ni kwa sababu kulikuwepo saini zao kwenye makaratasi ya mikopo, je la Malecela lilikuwepo kati ya waliosaini?

William @ NYC, USA.
 
- Hoja yangu ni kwamba hela za EPA zilichukuliwa na kundi la Mtandao kwa ajili ya kampeni ya Urais against Malecela na wengine, unashitakiwa kwa wizi wa benki kama kuna sahihi yako katika kuchota zile pesa, unasema kwamba that is the case against Malecela na hela za EPA?

- Now hoja yako ni ipi mkuu?

William @ NYC, USA.

Kuweka sahihi kwenye kutoa pesa sio issue. Kwani hao walioweka sahihi sio wazi kuwa walitumika kwa mbele tu. Tunajua kweli kuwa hizo pesa walizichukua na kwenda kuwapa ccm! Na ndio maana wanalindwa. Kwanza hujaweka timeline ya uchukuzi wa pesa na matumizi yake. Hapa tunaenda na word of mouth. You have not given us evidence on the contrary! Kwani hizi pesa zilitumika kwenye primaries za ccm tu? Kama mliona kuchezewa rafu wakati ule, kwa nini hamkutoka live na kukemea? Mbona hii ishu mmeimeza na sasa ndio mnajifanya kuipangua?
 
Ikiwa tunangoja ccm watimize ahadi yao ili sisi wananchi tuone nani fisadi, wavukazane ndani ya chama tutoke kwenye kucha ya mafisadi. dk slaa huyo kutochanganya.
Hana uvumilivu, subira hili linatufanya tuanze kuamini uwezo wake wa kuongozataifa kubwa tz likawa salama. kauli ya Msajili wa vyama vya siasa kuhusu dk slaa inaanza kuonekana
hekima ni kitu muhimu, subira ni muhimu pia.

Nawaamini sana wazee ila wewe una waaibisha sana wazee, una nipa mashaka kuamini huo Uzee wako, huwa siamini kuwa wazee wakizeeka akili zao pia zina zeeka na kuota kutu siamini hivyo ingawa wewe unaonyesha hivyo! Ebu jaribu kujadili haya mambo yafuatayo: -

  1. Hunashindwa nini kujua kuwa CCM hawana la kufanya zaidi ya waliyofanya Dodoma? Yaani wewe hujui kuwa kama vikao halali havikuwachukulia hatua hao mafisadi hamna mtu mwingine tena ndani ya CCM ataweza kuwafanya lolote!
  2. Hujui kuwa Mzee Msekwa anazunguka kupiga ngoma kuwaomba Mafisadi wajitoe CCM? Kama hawataki kutoka itakuwa? Maana kuomba kuna kukubaliwa na kukataliwa! CCM ilishindwa nini kuwachukulia hatua ndani ya vikao halali na vyenye mamlaka ya kuwatimua wanachama! Msekwa wala Mkama hana mamlaka yoyote kumfukuza Mtu kutoka CCM, au hujui hilo!
  3. Unadhani Msajiri wa vyama vya Siasa (Ndg. Tendwa ni kisima cha busara!) hivyo unaweza kumtumia kama reference ya ku-sopport hoja yoyote katika Dunia hii! au Una-refer Msajiri wa Vyama vya Siasa vya nchni gani? Je? unadhani kutumia maneno ya shutuma kutoka kwa wakala wa CCM kuwa ndio reference yako ku-support hoja dhidi ya huyo unaye mtuhumu siyo kunaregeza hoja zako?
  4. Kwani CDM ni Jumuiya ya CCM hivyo inapaswa kushirikiana na CCM! au Uoni kuwa Watanzania wamesubiri CCM ishughulikie Mafisadi tokea ile list of Shame 2007 hadi leo 2011 lakini CCM imeshindwa! unataka kusubiri hadi lini tena?
  5. Mwisho huoni kuwa Slaa anafanya vyema kuwapa up date list ili waweze kuwa up date na list mpya!
Mzee wa Hoja, Ebu elezea vyema hapa una hoja gani unataka kujenga?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom