Yeah ni kweli, wanawake tuna ile mentality ya kupenda kubebwa na kuhurumiwa, na kubembelezwa, tunaona tunastahili special treatment sasa tukikutana wenyewe kwa wenyewe kila mmoja anahisi ana haki ya kupata hivyo vitu kutoka kwa mwenzake matokeo yake tunajikuta tunavimbiana. Mfano mdogo ni mimi siku za nyuma ilikuwa ninapoenda kazini lazima nipite pale stendi ya mkoa kwa hiyo nilikuwa nakutana sana na adha ya wapiga debe. Nilichokuwa nafanya siongei na mtu mimi ni kuangalia mbele tu hata nikivutwa mkono najitoa kimya kimya. Nilizoea hivyo yaani ila siku moja nikakutana na mpiga debe wa kike kama kawaida yangu nikapota kama upepo...wacha abwatuke, sikumsikia maneno yake ila nilisikia tu maneno 'wanawake sisi tunafanyiana roho mbaya'....yaani mimi wapiga depe wote nawapita kimya ila yeye kwa vile mwanamke mwenzangu nilitakiwa nisimame, nimsalimie kwa tabasamu pana nimwambie 'samahani mpenzi leo sisafiri ila wiki ijayo naenda Moro nitakutafuta'. Upuuzi huu