Tabia za wanawake kuchukiana bila sababu.

Tabia za wanawake kuchukiana bila sababu.

The iron batterfly

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
1,952
Reaction score
2,527
Habari za jioni wana jukwaa.

Ni hivi kwenye ofisi ninayofanya kazi tuko watumishi kama 15 hivi,kati ya hao wanawake tuko saa watano pamoja na ps,walobaki ni wanaume.

Basi kuna kipindi tulipewa zawadi ofisini,nami nilikuwepo miongoni mwa waliopata,tukiwa wanawake wawil tu tuliobahatika ,nikajipost kwenye group ya ofisini wanaume almost wote walikuwa happy na kunipongeza,ikaja kwa wanawake Sasa,mtu unakutana naye koridoni anakuuliza nimeona bana umepewa cheti,unamjibu ndio,anakwambia hongera huku ikiambatana na kicheko Cha kebehi na kejeli.

Ukija kwenye groups za wasap, comments wanazotoa wanaume kwetu wanawake si za kubeza,hata kama kukukosoa atakukosoa kistaarabu.Ila wanawake mtu atoa comments kama mna ugomvi,ama aweza comment neno la kukudhalilisha ilmradi usijisikie vizuri.Hadi wajiuliza ,tatizo nini?

Kuna wakati mwenzetu mmoja alikuwa mjamzito, jamaa mmoja wa ofisin akapiga naye picha akaipost kwa group,most of men walikuwa happy na walikuwa wanacomment positively,na matani ya hapa na pale,ila upande wa wanawake sasa wakatoa maneno ya kejeli na kuonyesha kutofurahia hilo jambo,as if wamechangia mume .Mwingine akaandika ,,ahhh mama kijaaa hongera bwana,then hehehehe halooo
,Like what the f@ck?

Hata kwenye ishu za deals ni mara chache,mwanamke akushirikishe hata kama una uwezo wa kulifanikisha,but kwa upande wa wanaume wako so smooth na washirikishaji wazuri.Tena wanawake hao wakigundua kuna kaishu unafatilia yuko radhi hata akuharibie kwa client,ili tu mkose wote.

Ishu ni nyingi,ila wanawake mostly hatupendani maofisini,Hatuko professional mostly,Tunasemana vibaya,tunaoneana wivu wa kijinga (siyo wa kimaendeleo),tunachafuana Wala hatusapotiani kwenye ishu positive.Nashindwa elewa tatizo ni nini.

So swali ni kwanini wanawake hatupendani?ni nature?Ni laana?Na suala la kutaka unnecessary competition na wanawake wengine sababu ni nini?
 
Niwe mkweli sina chuki na wanawake wenzangu hata kidogo

Ila naprefer kudeal na wanaume zaidi manake najua wanawake wengi wapo kama ulivyoelezea hapo juu (unafiki)

Heri kubishana na mwanaume kuliko na mwanamke
 
Yes tuna tabia za unafik sana,utaona mtu akuchekea ukidhan rafiki kweli akikupa kisogo aenda kukuharibia.Kuna kaishu jamaa mmoja aliniletea ofisini nikamwambia we pambana kikipatikana chochote tutagawana,heeh si shost mmoja akaisikia hiyo ishu akaenda haribu kwa client,hadi client akasema ameghairi kununua hiyo bidhaa.kuja kupata ukweli aloharibu ni shost nayekula na kunywa naye most of the time,nilichoka mwili na roho.
 
Hahaha minuno mingi unashangaa mtu anakupiga kikumbo cha kimuandiko je ukikutana nae si anakumwagia mafuta kabisa!!!! Nipenge kamasi kwanza
Nimecheka hadi nimepaliwa
Hicho ndicho kilitokea jamaa alipompost yule dada mjamzito,yani miandiko ilikuwa inascream hate,mtu anaumia mwenzie kuwa mama kija,wakati hawashei mume wala hawana ushost wa karibu kihivooo.
 
Sio kwamba men tuko happy ila tunatengeneza mazingira ya kupata favour fulani fulani toka kwenye maungo yenu. Bora hao wanawake wenzenu wako real na maisha yao maana hamhitajiani kihisia.
Inaweza kuwa sababu kweli,ila sioni logic mtu kumchukia mwanamke mwenzie eti kisa ana ujauzito,ndomana wanasema kibongobongo mimba ikiwa changa yapaswa kufichwa.
 
Yes tuna tabia za unafik sana,utaona mtu akuchekea ukidhan rafiki kweli akikupa kisogo aenda kukuharibia.Kuna kaishu jamaa mmoja aliniletea ofisini nikamwambia we pambana kikipatikana chochote tutagawana,heeh si shost mmoja akaisikia hiyo ishu akaenda haribu kwa client,hadi client akasema ameghairi kununua hiyo bidhaa.kuja kupata ukweli aloharibu ni shost nayekula na kunywa naye most of the time,nilichoka mwili na roho.

Ndio tatizo
Huwa hakuna ile loyalty kati ya mwanamke na mwanamke...mwanamke ni rahisi sana kukuzunguka,ana uwezo wa kukufanyia baya lolote na siku ikitokea ukagundua alichofanya ni either atakupa excuses zisizo za msingi ama atakuonesha dharau za wazi kwa alichokufanyia
 
Back
Top Bottom