Tabia za Vipanga wa darasa na vimbwanga vyao

Tabia za Vipanga wa darasa na vimbwanga vyao

Ganda la ushuru

Senior Member
Joined
Mar 18, 2020
Posts
132
Reaction score
112
Salaam! matumaini yangu ni kwamba jumapili ya leo ni nzuri na tuna chukua hatua kuepukana na Corona.

Leo nimekumbuka mbali enzi za primary ,O-level, na A-level back in the days. Kuna hawa wenzetu ambao walikuwa vizuri kwenye masomo walikuwa wanakimbiza sana kwenye masomo.

Kuna ambao walikiwa na roho nzuri na njema lakini baadhi yao aisee basi tu ili akusovie swali umekutana na kuwekwa pending sana, umempamba pamba we na mambo mengine mengi yani in short walikuwa wanajivuna.

Lakini cha kushukuru Mungu ni kwamba kutokana na tabia zao watu waliamua kupiga msuli adimu na kupasua. Karibu na wewe ushee tabia za vipanga ulosoma nao, hata kama ni wewe ulokuwa kipanga tiririka tabia zako.

GLU™
 
Kuna mpuuzi mmoja tukiwa F6 alikuwa na Qn Paper 1 & 2 Bios na marking scheme zake... mpuuzi yule alikuwa anazizomea room tu, msuli bed! Haji nazo prepo hata! Kuna siku nikamchezea mchezo!

Muda wa Prepo nikajifanya kama naenda kumbe nikanyuti korido. Baada ya km ½saa nikarudi room vuuuh! Jamaa aliruka kutoka deka la juu mpk chini na pepa zake tumboni!
Ntarudi.

Msamvu kuna Mvua kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unge 'share' ka story kidogo mkuu ili tusogeze siku.
GLU[emoji769]
Nahofia usalama wangu ila ni product ya shule za kata kauli yangu ilikuwa moja tu wanafunzi we zangu mkisikia shule hii kafaulu mtu mmoja msihangaike kuangalia matokeo jueni ni mimi tu na wakati walikuwepo kama 20 wanaonipita uwezo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
They used to call me "C.E.O wa msuli yatima"[emoji23][emoji23]nikisoma kwenye magroup sielewi naona kabisa napoteza muda basi najikunja mwenyewe tuu.

Kufika chuo naambiwa nasoma kama siji kuolewa, but it was a life lived. Siendi darasani discussion sizielewi but end of semester gpa inasoma.

All in all, jambo lililonitesa ni kunyimwa notice, mtu anaona anakupa notice afu uje kumpita haiwezekani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dah!

Lakini na nyie Vilaza wa Primary mlikuwa na visa sana manake mlikuwa na wivu ingawaje mlikuwa vitoto vidogo!!

Ngoja nianze na huyu "Shetwani" enzi hizo tukiwa Darasa la II !! Sikuwa na mpinzani kwenye zile alama za good (tick) zikiwa zinahitimishwa na maneno VIZURI SANA/VEMA SANA zilizokuwa zinakolezwa kwa Bic Nyekundu!!

Sema na mimi nilikuwa na nyodo, wacha bhana hadi siku moja "litoto lihuni limoja" likaja school na chain stick!!! Yaani mitoto ya Uswahilini ina laana! Yaani kitoto cha miaka 10 (+/-) kinatembea na chain stick na kujifanya eti Bruce Lee... cjui alizipata wapi mtukutu yule!

Wacha atutwange nazo ingawaje tulimchangia ugomvi na sister angu, salama yetu ikawa wapita njia!!!

Basi bhana... kinyume na mazoea yangu ya kupata alama PATA mwanzo hadi mwisho, siku hiyo narudishiwa daftari nakuta limejaa mikasi kuanzia swali la kwanza hadi la mwisho!!

Dogo mmoja, kwa jina la Ismail, KILAZA namba moja darasani si akaanza kulitembeza daftari langu darasa zima kuonesha mikasi yangu!!

Ingawaje jamaa lilikuwa kubwa kwangu lakini sikuvumilia udhalilishaji ule! Yaani Mkali wa Darasa anapata Mikasi mwanzo mwisho halafu unaanza kumchoresha darasani?! Usin'tanie!

Tukazichapa, sana tu... sikumbuki matokeo ya mpambano ule lakini nadhani alinitandika tu!! Kwanza mitoto isiyo na akili darasani ilikuwa inajua kupigana kishenzi; no wonder yalikuwa vilaza!!

Kesi ilipofika kwa Mwalimu, teacher akawa upande wangu!! Unamwadhibu vp "Mtalaamu" hata kama ndie kaanza kurusha ngumi?!

Hayo yakapita, akatokea Mhujumu Mkubwa zaidi enzi nikiwa Darasa la VI au VII... sikumbuki vizuri!!

Kama kawaida chige na Very Good/Excellent... Keep It Up zangu siku moja nikawa nasubiria kwa hamu daftari langu baada ya kupewa zoezi la Hisabati!

Siku madaftari yamerudishwa nika-mind kishenzi kukuta hayajasahishwa wakati nilikuwa nasubiria EXCELLENT CHIGE, KEEP IT UP yangu!! Usicheze na mimi wewe... Jitu ambalo nilijaribishiwa mtihani wa LY wakati nipo Darasa VI na bado nikapasua?

Sijui niliharibikia wapi chige mimi, manake kufika Form IV nikawa naona shule kama Mgonjwa wa Coronavirus!!!

Basi bhana, nikiwa nime-mind madaftari kutosahishwa na hivyo kukosa EXCELLENT CHIGE, baadae kuja kuchunguza lile daftari, AHMADI!!

Kumbe kuna Mhujumu mmoja ali-edit majibu yangu karibu yote! Yaani nilipoandika 6, akaitengeneza kuwa 8, au nilipoandika 1 angeibadilisha kuwa 7 !! Yaani endapo yale madaftari yangesahishwa, ningekuwa nimekosa maswali YOTE na hatimae kuandikiwa PLEASE SEE ME!!!

Just imagine, kitoto cha primary kinafanya hujuma namna hiyo kwa kitoto chenzake... huko aliko huyo jamaa sijui kakubuhu kiasi gani kwa Uhujumu!!

Ni vile tu sina uhakika Mhujumu wangu alikuwa nani ingawaje nahisi alikuwa Mtoto wa Headteacher... headteacher ambae pia alikuwa ndie Mwalimu wa Hisabati!!

Hili toto lilikuwa linajifanya rafiki yangu lakini inaelekea lilikuwa na wivu kwa sababu ingawaje lenyewe lilikuwa toto la Mwalimu Mkuu lakini nilikuwa naliburuza kuanzia Std I hadi VII... pumbavu zake!!

So, kwavile mimi nilikuwa Kipanga, sikuwa na budi ku-share tabia za Vilaza Wenzenu... mlikuwa na wivu kishenzi!!! Tena ilikuwa tukitumwa kuandika ubaoni ndo mlikuwa mnateseka ile mbaya utadhani sie ndio tuliwafanya muwe mnaandika majongoo... shenzi taipu!!!
 
Nahofia usalama wangu ila ni product ya shule za kata kauli yangu ilikuwa moja tu wanafunzi we zangu mkisikia shule hii kafaulu mtu mmoja msihangaike kuangalia matokeo jueni ni mimi tu na wakati walikuwepo kama 20 wanaonipita uwezo

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonekana ulikuwa mtata sana 💪💪.
GLU™
 
Nilikuaaga nachelewa shule , nachelewa parade, nachelewa bwalo la chakula, nachelewa prepo, etc.

Kwenye mtihani tuu sichelewi na nawahi kumaliza, na naongoza.

Nakukumbuka mtihani wa chemistry niliwahi fanya dk 30 , nikatoka nukaenda kulala dom..namka ndio nakuta wenzangu wanarudi.. na huo mtihani nibangua 99%


Najiuliza yale maakili nilipeleka wapi? Haaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom