Mambo tuliyokuwa tunayapenda sisi Vipanga tukiwa Masomoni

Jokajeusi

JF-Expert Member
Jun 1, 2018
6,305
10,564
Wakuu kwema!

Kwa sasa tumeshakuwa watu wazima, maisha yanaendelea vizuri. Leo nimekumbuka mambo niliyokuwa nayapenda enzi hizo miaka kumi iliyopita nilipokuwa masomoni.

Mimi nilikuwa miongoni mwa vijana vipanga enzi hizo, kuanzia shule ya msingi mpaka namaliza chuo kikuu sijawahi kushuka daraja la kwanza au kupata chini ya wastani wa A. Matokeo yangu ya darasa la saba niliwafurumusha wenzangu kwa kupata maksi 239 kwenye masomo matano yenye jumla ya maksi 250, hii ni kusema nilikosa maksi kumi na moja tuu kupata 100%.

Kidato cha pili nilipata maksi 979 kwenye masomo kumi na moja kwa wastani wa 89.

Kidato cha nne nilipata divisheni one ya 9 kwenye masomo tisa, nikiwa nimepata masomo matano A na manne B
Kidato cha sita ndio ilikuwa bwerere, hapa nilinyuka one ya 4, masomo mawili nikichapa A huku somo moja nikipiga B, na GS nikinyuka A.
Chuo kikuu mambo yalikuwa matamu nilipata First Class GPA YA 4.6

Kwa sisi Vipanga kufaulu ni tabia sio kusoma au juhudi, wakati wengine wanawekeza kusoma ili wafaulu sisi vipanga tunawekeza kwenye tabia ya kufaulu na hivyo kwenye mitihani tunakula bata tuu.

Mambo ambayo sisi Vipanga tulikuwa tunayapenda tukiwa masomoni enzi hizo twasoma!

1. Tunapenda Mitihani
Vipanga wote tulikuwa tunapenda mitihani. Sifa ya kipanga ni kupenda mitihani. Ukiona ulikuwa huipendi mitihani basi jua ulikuwa kilaza. Vipanga tunapenda sana mitihani, nilikuwa naombea kila siku kuwe na mitihani ili nisifundishwe darasani. Kwa kweli nilikuwa sipendi mwalimu aingie darasani aanze kufundisha hasa akiwa na fimbo au atoe notes nyingi tuandike. Vipanga hatupendi kuandika notes. Ukiona ulikuwa na notes nyingi na ulikuwa unaandika notes basi jua wewe bado haupo kundi la vipanga.

Kipindi cha mitihani tunakifurahia sana, nilikuwa nataka kujua akili ya mwalimu wangu ikoje, na akili ya mwalimu ipo kwenye utungaji wa mitihani.

Kwetu mitihani ilikuwa kama fimbo ya kuchapia vilaza na kuwadhalilisha wajione ni wajinga wasio na tofauti na wanyama. Unakuta upo ndani ya mtihani kilaza anakukodolea macho:D:D:D akitaka kupiga chabo.Vipanga tuna miondoko mingi sana,kipindi cha mitihani tunakuwa tunatembea kama wanasayansi wa NASA:p:p:p:p. Mimi nilikuwa siumwi na macho lakini utaniona nimevaa miwani yenye kioo cheupe nyakati za mitihani hapo ukiongeza na mwendo wangu wa kisayansi basi vilaza walikuwa wanatukodolea macho kweli kwa hofu;);)

2. Tunapenda matokeo
Vipanga wote tukishafanya mitihani tulikuwa tunajua matokeo kabla hayajatoka, tulikuwa tunapenda matokeo yatoke mapema ili tupewe sifa na tuzidi kuogopwa. Ucheleweshaji wa matokeo ni kutufanya vipanga tukose Kiki tuwapo mtaani au shuleni/vyuoni. Kikawaida vipanga hatuangaliaga matokeo pindi yatokapo huwa tunaletewa na vilaza wanaoenda kuangalia kwenye Ubao wa matangazo wa shule. Hiki ni kipindi chetu cha kutamba.

Kwa level ya shule za msingi na sekondari ugawaji wa karatasi za matokeo pia tulikuwa tunaupenda. Vipanga tulikuwa tunapenda mwalimu ataje jina na maksi jambo ambalo vilaza walikuwa wanaona ni adhabu kubwa ni bora wachimbe visiki:D:D:D:D. Hivi unatajaje maksi za shalobaro wa darasa kapata mbili, alafu unataja mbele ya mademu;););) Waalimu wengine mlikuwa mnawakera vilaza mashalobaro. Au mbabe wa darasa kala zake tatu chini ya mia alafu utaje maksi:p:p:p:p Kwa nini usipigwe mayai viza.

Mimi karatasi yangu ikiitwa kwanza darasa zima wanajua hapo sio chini ya 80%, mwalimu ataita mimi nitachelewa kuinuka kwenye kiti makusudi ili arudie jina langu mara kadhaa:D:D kisha darasa zima litageuka nyuma (nilikuwa backbencher) kunitazama kwa hofu huku wengine wakinitolea macho ya hasira utadhani mimi ndio nimewapa ukilaza. Nitachukua miwani yangu na kuiweka usoni kisha nitaupinda mgongo kidogo na kuunza mwendo wa kitesla, mwendo huu nikitembea hapana shaka mpaka mwalimu anaamini mimi ni kichwa:D:D:D:D

3. Hatupendi Masahihisho
Hakuna jambo baya ambalo vipanga hatulipendi kama masahihisho ya mitihani. Vilaza hupenda masahihisho kwa vile wamekosa nusu ya mtihani, mtu kapata 20% kwa nini asipende masahihisho. Mimi nimepata 93% hizo maksi nane ndio zinifanye nihangaike na masahihisho? Thubutuu!

4. Tunapenda Mahafali
Vipanga tunapenda mahafali, na kwa bahati nzuri ukiwa kipanga OG lazima ualikwe kwenye matukio muhimu kama mahafali ya wanafunzi wengine hata kama sio darasa lako. Kipanga yoyote yule lazima awepo kwenye mahafali hata kama sio yake, hii ni kutokana na ratiba ya zawadi kwa vipanga wa shule. Ufikapo muda wa zawadi lazima jina lako litajwe kwa vyovyote vile. Kama sio zawadi ya kushika nafasi ya kwanza basi zawadi ya kuongoza somo la mathematics, Fizikia, kemia na Biolojia. kuna mwendo wa kuchukulia zawadi pia, hapa kwenye mchomekeo lazima uvae kidogo mayeno kwa mbali kama ishara ya kushindikana kwenye masomo:D:D:D:D. Wale wavaa milegezo tulikuwa tunawaona akili yao ipo chini kabisa ya matako yao.

Pia siku ya mahafali tunakuwaga na suruali zetu spesheli kwa tukio la mahafali. Ni lazima suruali iwe na marinda ili tuweze kuvaa mayeno, unajua modo haipendezi mayeno ndio maana siku ya mahafali vipanga wote duniani tunavaa duruali zenye marinda kusudi tupandishe yeno kwa mbali kama ishara akili zetu zinaenda juu sio chini kama wavaa milegezo.

5. Tunapenda Usaili/ Interview
Vipanga tunapenda kufanyiwa usaili ndipo tupate kazi au jambo lolote. Hatupendi kazi za bure bure, Mimi nilikuwa napenda usaili ili niweze kuwapima wale wanataka kuniajiri, kwenye usaili licha ya kuwa mimi ndio muombaji wa kazi lakini wanaonifanyia usaili wanajikuta kwenye wakati mgumu sana kwani wakimaliza kunipima nami nitakuwa nimemaliza kuwapima. Vipanga tunapenda usaili hasa mimi, kwa sababu pale HR anapochukua CV na vyeti vyangu na kuvipitia nikiwa namtazama lazima awe na hofu kubwa kwani HR wengi zaidi ya 99% hawajawahi kunikaribia ufaulu nilioupata. Pia hakuna swali ambalo HR angeniuliza ambalo nitashindwa kulijibu.

Nilishangaa humu wakimshambulia YEHODAYA alipokuwa akiwaponda wasomi wa masuala ya fedha alafu hawajui Noti ya elfu kumi inamnyama gani, ndio shida ya vilaza,, hilo ni swali dogo sana, huwezi shindwa swali la kitoto kama hilo.

Niliposoma post ya YEHODAYA, Pembeni yangu alikuwepo mke wangu, yeye ni Daktari Muhimbili, nikamuuliza kwenye sindano ya kumchomea mgonjwa, zipo mililita ngapi? Akabaki anashangaa wakati kila siku anashika sindano. Huo ni ukilaza, basi tulisemana tukitaniana huku naye akinitafutia maswali ili nami aniite kilaza lakini alikosa kwani yote aliyouliza nilijibu.

Hayo ndio mambo Vipanga tuliyokuwa tunayapenda enzi tukiwa masomoni.

Jokajeusi
 
Ila sisi Vilaza ndo tulikua ma famous sana kuliko nyiee wakusoma 🤣🤣

:D :D :D

Halafu nyie mlikuwa mnatutesa sana hasa wale mashalobaro na miondoko yao na miongeo yao.
Ufemasi wenu ulitokana na kuwa mitihani ilikuwa kwa msimu jambo ambalo lilikuwa mwiba kwetu. Ninyi kwenye michezo, muda wa mapumziko, muda wa lunch kote mlikuwa mnatamba, sasa sisi mpaka tusubiri Debate na mitihani ilikuwa inatugharimu.

Miondoko ya tambo za vilaza wakiwa wamepiga kiwi viatu ilitutesa sana walahi
 
Kipanga ni yule mtoto wa Morogoro vijijini ambaye kwa kutumia vidole vyake 20( miguu na mikono) ameweza kubuni formula kichwani mwake ya kujumlisha na kutoa namba yoyote akiwa na umri wa miaka 6 tu!.

Wewe Jokajeusi ni bingwa wa kukariri na si kipanga kwani mpaka sasa huna ulichogundua.
 
Vipanga mlikosa moment mbalimbali za kukumbuka shuleni hamku enjoy maisha ya shule nyinyi ni darasani chooni na bwenini wenzenu


Kwa wale tuliosoma porini Tulikuwa tunawinda na kukimbizana na wafugaji japo ni utoto ila hilo tukio lina exciment fulani yani u adventure ndani yake

Kwenda mtaani kucheki ball na kuzurura na si ajabu usiku umekaa siti moja na ticha kibandani mnabishana mpira na hii ilitusaidia kujua mitaa na kufahamiana na wana sio wewe uko class unapiga msuli tu unasoma mbeya hujui mbeya unajua stendi na njia ya kwenda shule tu

Wale madoja ili kua inasaidia kukwepa vitu vingi japo sio sahihi kuwa mtoro darasani sio wewe kipanga kila sehemu upo kazi za kufyeka sjui kunyanyua mawe kazi za darasa we upo kuna zile adhabu za "wote" we upo tena nyinyi jkt ndo mlikuwa mnajila sana mnajiumiza kwelikweli mnakuja na ule umimi wenu lakini at the end of the day wote cheti kimoja

Vipanga wengi hamkuwa na marafiki mlikuwa na wafuasi wakutaka muwafundishe na kama mnao ni wawili au mmoja tofauti na wahuni walikuwa na marafiki hardcore tokanitoke ,wengi tu na walikuwa very social na hii ilisaidia vyuoni ila nyie mnaenda kuwa na ma introvert vyuoni hamjuani na watu mnakosa mengi penye watu kunamengi wengine ndo vijana wa sahivi.mnamaliza.na.gpa kali we ulikuwa wa kusoma tu hata watu huwajui huna chaneli upoupo tu

Ila wahuni na vilaza tuna mengi ya kukumbuka na kujifunza na si ajabu utakuta licha ya vipanga kusoma sana wote mko level sawa kielimu au mko cheo sawa

SIO SAWA KUA KUWA KILAZA ...akili kumkichwa

Ni hayo tu .



Muhuni wa kwanza Manzese kuwa entomologist

Kunguru
 
Vipanga mlikosa moment mbalimbali za kukumbuka shuleni hamku enjoy maisha ya shule nyinyi ni darasani chooni na bwenini wenzenu


Kwa wale tuliosoma porini Tulikuwa tunawinda na kukimbizana na wafugaji japo ni utoto ila hilo tukio lina exciment fulani yani u adventure ndani yake

Kwenda mtaani kucheki ball na kuzurura na si ajabu usiku umekaa siti moja na ticha kibandani mnabishana mpira na hii ilitusaidia kujua mitaa na kufahamiana na wana sio wewe uko class unapiga msuli tu unasoma mbeya hujui mbeya unajua stendi na njia ya kwenda shule tu

Wale madoja ili kua inasaidia kukwepa vitu vingi japo sio sahihi kuwa mtoro darasani sio wewe kipanga kila sehemu upo kazi za kufyeka sjui kunyanyua mawe kazi za darasa we upo kuna zile adhabu za "wote" we upo tena nyinyi jkt ndo mlikuwa mnajila sana mnajiumiza kwelikweli mnakuja na ule umimi wenu lakini at the end of the day wote cheti kimoja

Vipanga wengi hamkuwa na marafiki mlikuwa na wafuasi wakutaka muwafundishe na kama mnao ni wawili au mmoja tofauti na wahuni walikuwa na marafiki hardcore tokanitoke ,wengi tu na walikuwa very social na hii ilisaidia vyuoni ila nyie mnaenda kuwa na ma introvert vyuoni hamjuani na watu mnakosa mengi penye watu kunamengi wengine ndo vijana wa sahivi.mnamaliza.na.gpa kali we ulikuwa wa kusoma tu hata watu huwajui huna chaneli upoupo tu

Ila wahuni na vilaza tuna mengi ya kukumbuka na kujifunza na si ajabu utakuta licha ya vipanga kusoma sana wote mko level sawa kielimu au mko cheo sawa

SIO SAWA KUA KUWA KILAZA ...akili kumkichwa

Ni hayo tu .



Muhuni wa kwanza Manzese kuwa entomologist

Kunguru

Mkuu unawajua vipanga au unawasikia?
Toautisha Vipanga na wasongokaji.

Mimi ni kipanga, Gifted, hakuna ambacho sikufanya shuleni isipokuwa ugomvi tuu ndio nilikuwa siupendi,
Nilishawahi kuiba chakula cha waalimu nikachapwa mbele ya shule tukiwa na kundi langu.
Nilishawahi kuitisha mgomo wa kupinga makande nikapewa suspension ya siki tatu.
Nishawahi kukutwa na simu shuleni, nikapigwa per ya wiki mbili.
Nishawahi kutoka na madam nikaingia mgogoro na sir J, hii nitaianzishia uzi humu.
Nishawahi kuunda genge la wahuni na kumtengenezea zengwe mkuu wa shule nikataka kufukuzwa shule, nikahamishwa kutokana na maombi ya wazazi wangu.

Unajua maana ya mtu Gifted mkuu, mimi sio Talented bali Gifted, nina zaidi ya vipaji saba, na vyote nimevitumia shuleni na vyuoni
 
Mkuu, sijaachana nazo, nilisema nitawapumzisha kwa miezi kadhaa kisha watano nitarudi tena.
Unajua nilipigwa Ban ya mwezi mzima, na mimi lugha ninayoitumia ni kali na siwezi kubalisha hivyo nawapumzisha tuuu
Okay sawa
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom