Tabia ya Watanzania wengi kupenda kusalimiwa!

Tabia ya Watanzania wengi kupenda kusalimiwa!

Cha kushangaza ni kuwa, salamu ni kudanganyana tu Ila tunapenda!

Mtu anaulizwa, "Mambo vipi?
Anaitikia "Fresh

Wakati Mambo yake yako vibaya, na yuko na stress nyingi tu!
[emoji1787][emoji1787]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Kuna wengine ukiwasalimia hawaitikii salamu yako,siku zinazofata ukila buyu wanakuona haufai au wao ndo wakusalimie sasa.
 
Kumsaidia mtu akidondoka ni jukumu la mtu aliye karibu naye kwa wakati huo, iwe aliyeanguka alisalimia au hakusalimia. Mbali na hapo, huo utakuwa si msaada bali ni unafiki.

Yaani kumsaidia mtu aliyeanguka ni mpaka usalimiwe?
😂😄😁😆😅😅😆😆😁
 
Salamu haigombi.
Ila likikukuta la kukukuta utajua .
Habari za asubuhi Jambo Forums!

Wengi nimeshuhudia wakisemwa vibaya kwenye mikusanyiko mbali mbali kwa sababu ya kutosalimia aidha kwa bahati mbayaau makusudi.

Hivi kwa nini imefika kipindi ni bora Mtanzania umnyime chakula ila si salamu?
Yaani hata ukiwa ndani ya gari ukampita mtu bila kumsalimia atasambaza maneno mtaa wote na wote watakuona unajivuna.

Hata ukikuta tu 'wasela' wamekaa basi ukiwapa salamu wanaweza hata kutokukukaba kabisa.

Ingawa salamu ni nzuri ila ni kwa nini Watanzania wengi wanailazimisha na kuifanya kama chakula?

Mpaka kufikia watu kuchukiana na kujengeana husuda kwa ajili ya salamu si dalili nzuri. Tujithamini!.
 
Acheni Dharau na Majivuno Kwa watu salimieni watu .
Hata hakuna Gharama yoyote Ile kusalimia.
Gari lako zuri
Cheo chako kazini
Nyumba yako nzuri
Pesa zako nyingi
Na kila hadhi uliyo nayo
Kuna wakati sio kitu ukipata tatizo Kwa jamii inayokuzunguka.
Zingatieni kipengele Cha Good interactions with other social groups.
Millennials wakianza kupata vipesa vinaanzaga kuwa vizungu mkuu....heshima kwao inapimwa kwa mafanikio...kujuliana hali ni kupoteza muda wa kutengeneza pesa zaidi...
 
Habari za asubuhi Jambo Forums!

Wengi nimeshuhudia wakisemwa vibaya kwenye mikusanyiko mbali mbali kwa sababu ya kutosalimia aidha kwa bahati mbayaau makusudi.

Hivi kwa nini imefika kipindi ni bora Mtanzania umnyime chakula ila si salamu?
Yaani hata ukiwa ndani ya gari ukampita mtu bila kumsalimia atasambaza maneno mtaa wote na wote watakuona unajivuna.

Hata ukikuta tu 'wasela' wamekaa basi ukiwapa salamu wanaweza hata kutokukukaba kabisa.

Ingawa salamu ni nzuri ila ni kwa nini Watanzania wengi wanailazimisha na kuifanya kama chakula?

Mpaka kufikia watu kuchukiana na kujengeana husuda kwa ajili ya salamu si dalili nzuri. Tujithamini!.
Nyie watoto wa siku Hz shida sana,salamu ni destuli za kiafrika,sie kaka,wajomba zenu ndivyo tulivyolelewa,sio kitu Cha ajabu,
Ni jambo la kawaida TU,ila tamaduni,ni dynamic vitu vinabadirika,hata sie wahenga msipotupa salamu,Wala hatukwaziki,tunaona poa TU,
Huwa nacheka kimoyomoyo,unakuta kabinti ka secondary,kwenye daladsla kanakuambia "kaka naomba unishikie begi"unajiuliza hv haka ka dadaa akaoni hata hizi mvi za 40+,?hakajui kwamba mama ake anaweza nilicheza nae kombolela?au ma ready!!!ndio hivyo tena
 
Millennials wakianza kupata vipesa vinaanzaga kuwa vizungu mkuu....heshima kwao inapimwa kwa mafanikio...kujuliana hali ni kupoteza muda wa kutengeneza pesa zaidi...
Pesa gani waliyo nayo mpk wadharau watu .
Be the same hata kama ni nani una nini
Tena heshimu mitaa unayokaa
 
Habari za asubuhi Jambo Forums!

Wengi nimeshuhudia wakisemwa vibaya kwenye mikusanyiko mbali mbali kwa sababu ya kutosalimia aidha kwa bahati mbayaau makusudi.

Hivi kwa nini imefika kipindi ni bora Mtanzania umnyime chakula ila si salamu?
Yaani hata ukiwa ndani ya gari ukampita mtu bila kumsalimia atasambaza maneno mtaa wote na wote watakuona unajivuna.

Hata ukikuta tu 'wasela' wamekaa basi ukiwapa salamu wanaweza hata kutokukukaba kabisa.

Ingawa salamu ni nzuri ila ni kwa nini Watanzania wengi wanailazimisha na kuifanya kama chakula?

Mpaka kufikia watu kuchukiana na kujengeana husuda kwa ajili ya salamu si dalili nzuri. Tujithamini!.
Afadhali na wewe umeona
 
Kusalimiana ni utamaduni wa wa watanzania, ukimuona mtu hasalimii ujue ana changamoto kwenye makuzi yake! Mbona hata wageni kutoka nje wanasalimia hata akisema hi inatosha, kuna watu hawasalimii hata majirani yaani yy ni maisha yake binafsi tu haitaji kuzoeana na watu au majirani mara nyingi hawa ni watu wanaojifanya wapo bize wana kazi nzuri nk kiufupi ni wanajiona superior,
Niwambie kitu kusalimiana ni mwanzo wa mazungumzo, watu wasiosalimia kila mtu anaejitambua atakushangaa, nianyo mifano mingi ya kilichowakuta watu wasiosalimia
1. Alikuwa ni mdada Daktari kabisa huyu nikiri aliathiriwa na uhaya uaani hawezi kabisa kusalimia anakupita kama mnyama sio mara moja yaani ndo maisha yake hana rafiki , alipata mimba na akazaa mtoto alifariki baada ya muda ila kwa tabia ya kutosalimia hakuna hata jirani wala rafiki aliyefika kwenye msiba huo, anajua mwenyewe jinsi alivyozika !
2. Nomewaona watu wanaokuwa na viwanja wakijaga kujenga mara nyingi huja na mikwara ya kujiona wana hela hela ndo kila kitu basi watajishaua kwa jinsi wanavyojua lakini hawasalimii kisa utasikia mm sipendi uswahili swahili, kinachowakutaga wanakijua wenyewe maana majirani hubaki wanawatizama tu pale atakapohitaji huduma muhimu za kijamii ndo hujua kweli watanzania hawapendi ujinga, anaweza kuhitaji hata vitu vidogo dogo na akakosa katika masingira yale , anaweza kuibiwa au kuvamiwa na badi watu wasijisumbue kujua kuna nini? Mtoto wake anaweza kupata shida na watu wasijishughulishe, maisha yetu yanategemeana sana hivyo tusalimie tu , salamu haitupunguzii kitu na , sehemu yeyote ukipita salimia , utakutwa na jambo hutoamini wale uliowapita kama mbwa ndo utakuja kuwalilia tena
 
Back
Top Bottom