Tabia ya Watanzania wengi kupenda kusalimiwa!

Wrevta

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2023
Posts
1,442
Reaction score
1,733
Habari za asubuhi Jambo Forums!

Wengi nimeshuhudia wakisemwa vibaya kwenye mikusanyiko mbali mbali kwa sababu ya kutosalimia aidha kwa bahati mbayaau makusudi.

Hivi kwa nini imefika kipindi ni bora Mtanzania umnyime chakula ila si salamu?
Yaani hata ukiwa ndani ya gari ukampita mtu bila kumsalimia atasambaza maneno mtaa wote na wote watakuona unajivuna.

Hata ukikuta tu 'wasela' wamekaa basi ukiwapa salamu wanaweza hata kutokukukaba kabisa.

Ingawa salamu ni nzuri ila ni kwa nini Watanzania wengi wanailazimisha na kuifanya kama chakula?

Mpaka kufikia watu kuchukiana na kujengeana husuda kwa ajili ya salamu si dalili nzuri. Tujithamini!.
 
Kwani ukimsalimia unatumia gharama kiasi gani?
 
Huwa wanasema hivi mtaani:

1.Salimia Housegirl,,wife husafiri 😁
2.Salimia wauza mkaa,gesi huisha
 
Wengine wanaenda mbali zaidi "Wanasema we kwanini husalimii ukidondoka hapo Sasa hivi Nani atakusaidia kama husalimii watu"

Sometimes watu wanakua wanamsongo wa mawazo Kichwani.
Tunapishana na watu njiani lakini wengi wanakua na mawazo chungu mzima.
 
Kula chuma hiyo

Kumsaidia mtu akidondoka ni jukumu la mtu aliye karibu naye kwa wakati huo, iwe aliyeanguka alisalimia au hakusalimia. Mbali na hapo, huo utakuwa si msaada bali ni unafiki.

Yaani kumsaidia mtu aliyeanguka ni mpaka usalimiwe?
 
Kula chuma hiyo

Shukrani sana mzee!
 
Kumsaidia mtu akidondoka ni jukumu la mtu aliye karibu naye kwa wakati huo, iwe aliyeanguka alisalimia au hakusalimia. Mbali na hapo, huo utakuwa si msaada bali ni unafiki.

Yaani kumsaidia mtu aliyeanguka ni mpaka usalimiwe?
Hilo jukumu umempa huyo mtu aliye karibu wewe kama nani?
 
Utakuta wanakwambia....salamu haitii mimba..upuuzi tu aisee

hii ni moja ya mentality za masikini kukazia vitu ambavyo sio vya lazima...
 
Back
Top Bottom