ACHIKOYO
JF-Expert Member
- Mar 21, 2022
- 312
- 352
Mimi nakushauri iwe wewe ushauri hizo interview zifanyike siku ya ijumaa, kwa maana hawa Waislamu hawalalamiki kwa nini ijumaa ni siku ya majumuhisho ya ibada zao za wiki nzima lakini na ni siku ya kazi pia ...?Unajisumbua kuleta hoja hii hapa, majibu ya watu wanaosnesha hakuna anaejali sana sana wanajibu kwa kejeli, lakini siyo haki kuwatendea hivyo kutokana imani yao. Serikali inapaswa kuheshimu imani ya kila Mtanzania hata wanaoamini usabato ni watanzania kama wengine na wanahaki kama nyie mnao kejeli hapa. Usaili ni sehemu ya kazi hivyo ni bora ufanyika siku za kazi na zisiwe za ibada za watu na hata ijumaa hakuna haja ya kufanya hivyo kuna jumatatu mpaka alhamis haiingiliani na imani ya mtu. Kazi inayofanyika ni sehemu ya kazi na kuwaumizia wengine siyo haki.
Lakini pia hilo wazo wewe sio mtu wa kwanza, nakumbuka Magufuli alibadilisha siku ya uchaguzi kutoka siku ya jumapili ambayo ulikuwa unafanyika kila mwaka wa uchaguzi kabla ya yeye kuwa Rais, mwaka 2020 akasema uchaguzi ufanyike siku ya jumatano ili jumapili wakristo waende kanisani.
Mwalimu Nyerere, Mzee Mwinyi, BW Mkapa hata Dr. Kikwete hili hawakuliona, na watu walikaa kimya na kumpongeza Dr. Magufuli kwa alichokifanya cha kubadili siku ya uchaguzi, ila wasiwasi jambo kama lile lingefanywa na mtu kama Kikwete la kwasema siku ya ijumaa ni siku kuu ya ibada kwa Waislamu, watu waende makazini hadi saa 11 : 45 am kisha waende misikitini na saa 01 : 15 pm warudi maofisini ingekuwa ajenda kubwa sana sana.